Ujerumani yatikiswa na mgomo mkubwa wa usafiri wa Umma

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mamilioni ya wasafiri nchini Ujerumani leo Jumatatu wanalazimika kutafuta njia mbadala ya usafiri baada ya kushuhudiwa kwa mgomo katika sekta ya uchukuzi.

Viwanja vya ndege,vituo vya mabasi na treni njia za majini kote nchini vinatazamiwa kuwa vitupu kufuatia mgomo huo unaotajwa kuwa mkubwa zaidi tangu miaka ya 1990.

Katika mgomo huo utakaodumu kwa saa 24 kuanzia Jumatatu wafanyikazi milioni 2.5 wa shirikisho na manispaa, chama cha wafanyikazi Verdi na chama cha wafanyikazi wa ummadbb wanadai nyongeza ya asilimia 10.5 ya mshahara.

Treni za masafa marefu zimeahirisha safari zake,hatua iliosababisha usumbufu kwa mamilioni ya watumiaji wa huduma hiyo muhimu,hasa katika majimbo kadhaa makubwa.

msururu wa magari ya madogo yakitumika kama mbadala wa usafiri umeshuhudiwa wenye matokeo ya uchelewaji barabarani kama matokeo ya mgomo wa siku ya Jumatatu.

Wawakilishi wa Verdi na dbb wanatarajiwa kukutana tena na maafisa wa serikali leo Jumatatu kwa duru ya tatu ya mazungumzo.

Ndani ya mwezi huu pekee migomo ya hapa na pale imeshuhudiwa na kuwaathiri mamilioni ya wakaazi.

DW Swahili
 
Kunapokuwa na Inflation lazima watu wadai nyongeza za mishahara. Kwa sasa Ulaya inasumbuliwa na tatizo la Inflation. Kwa hiyo, maandamano lazima yawepo tu.

Na serikali kuongeza mishahara inakuwa ni burden kwao. Na Inflation huwezi kui solve kwa kuongeza mishahara zaidi - zaidi ndio kuongeza matatizo...
 
hapo ndo tunakuja kujua nan alikua anaendesha dunia na anafanya maisha yawd cheap.
.
IMG_20230305_121255.jpg
 
Kunapokuwa na Inflation lazima watu wadai nyongeza za mishahara. Kwa sasa Ulaya inasumbuliwa na tatizo la Inflation. Kwa hiyo, maandamano lazima yawepo tu.

Na serikali kuongeza mishahara inakuwa ni burden kwao. Na Inflation huwezi kui solve kwa kuongeza mishahara zaidi - zaidi ndio kuongeza matatizo...
Hiyo inflation imesababishwa na nin mkuu
 
Russia effect
 
Hiyo inflation imesababishwa na nin mkuu
Kuna vitu viwili hapo vilivyopelekea hiyo inflation... Energy and Food

Kwenye Energy, EU wameshindwa kutafuta Energy ambayo ni cheap kama ile waliyokuwa wanapata toka Russia. Hii imepelekea uzalisha na gharama za maisha kuwa juu.

Food inflation iliwasumbua ila wameshaituliza.
 
Mamilioni ya wasafiri nchini Ujerumani leo Jumatatu wanalazimika kutafuta njia mbadala ya usafiri baada ya kushuhudiwa kwa mgomo katika sekta ya uchukuzi.

Viwanja vya ndege,vituo vya mabasi na treni njia za majini kote nchini vinatazamiwa kuwa vitupu kufuatia mgomo huo unaotajwa kuwa mkubwa zaidi tangu miaka ya 1990.

Katika mgomo huo utakaodumu kwa saa 24 kuanzia Jumatatu wafanyikazi milioni 2.5 wa shirikisho na manispaa, chama cha wafanyikazi Verdi na chama cha wafanyikazi wa ummadbb wanadai nyongeza ya asilimia 10.5 ya mshahara.

Treni za masafa marefu zimeahirisha safari zake,hatua iliosababisha usumbufu kwa mamilioni ya watumiaji wa huduma hiyo muhimu,hasa katika majimbo kadhaa makubwa.

msururu wa magari ya madogo yakitumika kama mbadala wa usafiri umeshuhudiwa wenye matokeo ya uchelewaji barabarani kama matokeo ya mgomo wa siku ya Jumatatu.

Wawakilishi wa Verdi na dbb wanatarajiwa kukutana tena na maafisa wa serikali leo Jumatatu kwa duru ya tatu ya mazungumzo.

Ndani ya mwezi huu pekee migomo ya hapa na pale imeshuhudiwa na kuwaathiri mamilioni ya wakaazi.

DW Swahili
Ufaransa maandamano, ujerumani maandamano..na hizo ndo vinara wa EU. Chanzo ni ugumu wa maisha. Kisa.. kupanda kwa gharama ya maisha kunakotokana na kususia gas, mafuta, chakula cha urusi. Kazi wanayo
 
Back
Top Bottom