Ujerumani yenyewe imeweka solidarity fund, hii ni kwa ajili ya wale wenye uwezo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
"Nchi yetu imeshuka kiuchumi tangu lilipoanza janga la #Corona. Tulikuwa tunaingiza Trilion 6 na zaidi kwenye utalii ila kwa sasa mapato yameshuka mpaka trilion 2" Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu.

"Ujerumani yenyewe imeweka solidarity fund hii ni kwa ajili ya wale wenye uwezo kutoa ili kuwasaidia wale wenye uwezo mdogo. Ukikatwa usijiwaze wewe, waza wale ambao wanahali ya chini kuliko wewe"

"Hii kodi tumeiweka kwa ajili ya watu wenye uwezo. Kati ya watu Milioni 50 wanaomiliki line za simu, watu Milioni 20 tumewatoa hawalipi hii kodi. Wanaolipa ni Milioni 30 ambao tunaamini wanauwezo kiasi. Na tunajuaje wana uwezo ni kwa kupitia TCRA"

"Kuwa na ada ya simu ni uzalendo leo hatuandiki barua, hatuna gharama ya sempu, leo mtu yupo Mwanza anauliza Soko la Pugu ni shilingi ngapi, anauliza soko la samaki ni shilingi ngapi. Hii ni nafasi nzuri tuwe na kodi ya uzalendo"
 
Huyu bogus kabisa Tz na Germany wapi na wapi.
LiBunge mzigo kabisa hili.
 
mbona wenyewe wabunge ambao ni miongoni mwa kundi la watu matajiri hawalipi kodi kwenye mishahara naposho wanazolipwa bungeni?
 
Ujerumani na Tanzania tunafanana? Jobless hulipwa monthly allowance na serikali wakulima hupewa subsidy kwenye bei ya kuuza mazao ili wasiuze kwa hasara bei ikiwa mbaya pia wakulima serikali huwakatia bima hali ya hewa ikiwa mbaya mazao yakawa duni bima huwalipa

Kwa nini alinganishe kodi tu bila kulinganisha mapato ya majority ya wananchi wakiwemo jobless wa Tanzania na Ujerumani?
 
Kwanini katika ile nch ya uchumi wa kati Afrika Mashariki haya hayafanyiki.
 
Zungu sio mtanzania nadhani ni mtu wa visiwa vya comoro ndio maana hana huruma na watanzania
 
Kununua vocha ya 2000/- kwa mwezi haimaanishi nina uwezo, aache ujinga huyo zungu
 
"Nchi yetu imeshuka kiuchumi tangu lilipoanza janga la #Corona. Tulikuwa tunaingiza Trilion 6 na zaidi kwenye utalii ila kwa sasa mapato yameshuka mpaka trilion 2" Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu.

"Ujerumani yenyewe imeweka solidarity fund hii ni kwa ajili ya wale wenye uwezo kutoa ili kuwasaidia wale wenye uwezo mdogo. Ukikatwa usijiwaze wewe, waza wale ambao wanahali ya chini kuliko wewe"

"Hii kodi tumeiweka kwa ajili ya watu wenye uwezo. Kati ya watu Milioni 50 wanaomiliki line za simu, watu Milioni 20 tumewatoa hawalipi hii kodi. Wanaolipa ni Milioni 30 ambao tunaamini wanauwezo kiasi. Na tunajuaje wana uwezo ni kwa kupitia TCRA"

"Kuwa na ada ya simu ni uzalendo leo hatuandiki barua, hatuna gharama ya sempu, leo mtu yupo Mwanza anauliza Soko la Pugu ni shilingi ngapi, anauliza soko la samaki ni shilingi ngapi. Hii ni nafasi nzuri tuwe na kodi ya uzalendo"
Kwa hali hii bado tunasafari ndefu sana.
 
Kwanini katika ile nch ya uchumi wa kati Afrika Mashariki haya hayafanyiki.
Nchi ziizoendelea zenye uchumi wa juu ndio hulipa jobless na ruzuku kwenye bei za mazao na bima ya kilimo
Hata upandishe miamala sio issue ana income toka serikalini hata kama ni jobless.
 
wenye uwezo ni wabunge na mwaziri na mishahara ayo haikatwi hata mia.
Pambaf kabisa.
 
Huyu hana akili hivyo anadhani sote ni wajinga kama yeye!
wananchi tuungane tuwaongo'e wabunge wote wa CCM ambao ni kero kwetu sisi wanyonge.kwa kuwa wao waliishatuibia sana leo hii wanatudharau kwa kura zetu.
 
Wakati mzuri sasa wa kuwakata wao na mihela yao,
Wameshakubali uzalendo kwanza hakuna namna
 
Back
Top Bottom