"Ujinai" wa Lulu katika "mauaji" ya Kanumba (R.I.P)


Huyo tabibu wa Kanumba ni Clinical Officer, Assistance Medical Officer au Medical Officer, maanake bongo kila mtu ni daktari.
 

Mkuu nimekupata. Kama ulivyosema ameshtakiwa chini ya kifungu cha 196 (Murder). Kwa vile uchunguzi bado unaendelea itabidi tusubiri tuone kama DPP ata-stick na murder au atabadilisha kuwa manslaughter au hata ku-withdraw case kulingana na ushahidi utakaopatikana.
 
yap. lakini withdrawal yake inakuwa kwa njia ya NOLLE PROSEQUI. state attorney anapoandika opinion yake (hawa wanamwakilisha dpp hasa through their incharge boss) huwa anafikia uamuzi mbalimbali ambao moja wapo ni kusuggest nolle, kusuggest certain charge etc. ila kwa kuliondoa huwa linaondolewa na nolle tu. hakuna njia nyingine. inatumika section 91(1) CPA....CAP 20.
 
Reactions: EMT
MSANIInyota wa filamu nchini, Steven Kanumba amefariki dunia kutokana na tatizo lamtikisiko wa ubongo linalojulikana kitalaamu kama Brain Concussion, taarifa zakitabibu zimeeleza.Taarifahizo za ndani, zilizopatikana jana baada ya jopo la madaktari bingwa watano waHospitali ya Taifa Muhimbili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu huyo,zimeeleza kuwa tatizo hilo linaweza kumfanya mtu apoteze maisha mara moja aubaada ya siku kadhaa. Mmoja wa madaktari hao ambaye aliomba jina lake lisitajwegazetini alisema waligundua tatizo hilo baada ya kumfanyia uchunguzi huo kwazaidi ya saa mbili.“Tulianza kuufanyia uchunguzi mwili wamarehemu kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 6:45 mchana na tukagundua kuwamarehemu alifariki kutokana na mtikisiko wa ubongo kwa kitaalamu, BrainConcussion,” alisema daktari huyo. Alisema Kanumba alipata mtikisiko wa ubongoambao husababisha kufeli kwa mfumo wa upumuaji (cardio-respiratory failure)“Kilichomuua hasa ni mtikisiko wa ubongo, ambao endapo unatokea katika sehemuya nyuma ya ubongo (cerebrum), huua kwa haraka” alisema daktari huyo nakuongeza kuwa mtikisiko wa ubongo wa nyuma, husababisha matatizo ya mfumo waupumuaji na hilo limeonekana katika mwili wake.
“Baada ya ubongo wake kutikiswa kwa nguvu,mfumo wa upumuaji ulifeli na ndiyo maana tumekuta kucha za Kanumba zikiwa narangi ya bluu, huku mapafu yake yakiwa yamevilia damu na kubadilika kuwa kamamaini, hizo ndizo dalili za kufeli kwa mfumo wa upumuaji.”
“Mtu aliyepatamtikisiko wa ubongo huweza kutokwa na mapovu mdomoni na hukoroma kabla yakukata roho na ndivyo ilivyokuwa kwa Kanumba kabla hajafariki.”(Kutokagazeti la mwananchi)

Kutokana na vitabu mbalimbali vya medicine...kwa kifupi, concussionni traumatic brain injury. Kwa maneno mengine, external physical force ambayo inaweza kutokana na kupigwa na kitukizito kichwani, kuangukia kichwa, accident, sports etc husababisha head injury ambayo husababisha brain injury (concussion).Watoto wadogo wanaweza kupata traumatic brain injury (concussion) kwa kutikiswakwa nguvu - ‘shaken baby syndrome’.

Kuna non traumatic brain injuries ambazo husababishwa na vitu kama stroke, infections eg meningitis, tumors, poisoning including alcohol poisoning na mengineyo mengi...ila hii aina ya brain injury haiwezi kuwa diagnosed as concussion kwa sababu hakuna trauma involved.

Traumatic brain injury (concussion) na non traumatic brain injury zinaweza kutafautishwa kwa kuangalia1. history eg je kulikuwa na accident, sports,violence, ugonjwa, uvimbe kichwani etc? 2. Symptoms,3. head CT/MRI pia huonyesha tofauti katika ya hizi brain injuries. Japo kulikuwana ugomvi/violence bado sielewi inakuwaje mtu anapata severe concussion iliyosababisha kifo baada ya muda mfupi bila jeraha au uvimbe wowote kichwani...

Kutoka povu kidogo mdomoni ni kitu cha kawaida mtu anapokufa kwa sababu yoyote ile, ila povu jingi ni moja ya symptom za matatizo kwenye mfumo wa chakula(gastrointestinal) zaidi kuliko concussion.

Kwa mtazamo wangu vigezo walivyotoa madaktari bado havitoshi kusema cause of death ni concussion...head imaging investigations zinaonyesha nini? aina zote za brain injury huweza kusababisha kufeli kwamfumo wa upumuaji. Kwanini hawakusubiri kupata majibu ya vipimo vyote (maini etc)kabla ya kuzika?. Tusubiri taarifa rasmi, maana hii ni kutoka "taarifa za ndani"...

 
Kaka umenigusa sana nimeshakaribia gombana na marafiki zangu juu ya Lulu, tumwache mahakama ifanye uchunguzi na naimani She is innocent kwani hajampa sumu labda katika kujiokoa ikawa vile. Mungu Atampigania kwani yeye ndo mpanga tarehe.

mungu atamjalia kwani ambao wanamshutumu wengi wao ni ambao wanachuki binafsi juu yake na wengine kutokana na ujinga tu!
 
taarifa ya daktari pekee (au expert opinion ya mtu yeyote yule), si pekee inayoamua ujinai wa mtu na sio binding, kama kuna ushahidi mwingine mzuri taarifa ya daktari inaweza wekwa hata pembeni. pia kumbuka tunasubiri pia majibu ya government chemisty(mkemia mkuu). nakushauri usisikilize au kuingiza ushabiki wa waandishi wa habari, utalala mlango wazi. waandishi wengi wa habari tz ni makanjanja, wanawezashabikia habari fulani utafikiri wanaelewa kitu chenyewe kumbe ni mambumbumbu wa kutupwa. angalia wale wa clouds fm kina kibonde.....hii ni issue ya kisheria, sheria ni profession ambayo ni nyeti sana kama huzijui principles zake, unaweza kuchangia kitu ukajianika ujinga wako vibaya mno. Napendekeza sana mimi siku zote, waandishi wa habari waende wakasome shule, na pia vyombo vya media viwe vinaajiri waandishi wa habari wenye profession tofautitofauti ili matu anapotoa au kuchunguza habari ili aitoe aende kiprofession. mfano: vyombo vingine ulaya, vinaajiri wanasheria na wanauchumi etc kuwa waandishi wa habari, hii ni baada ya labda mtu kuwa mwanasheria lakini anaenda pia kusomea uandishi wa habari etc. sasa ikitokea kuchunguza jambo la kiuchumi ili walitoe hewani yule mwanauchumi ndo nafasi yake hiyo, na habari itakayotolewa itakuwa bora kuliko habari ambayo Efrahim kibonde angeitoa...hahaha, hivyo hivyo na kwa wanasheria....basi nendeni mkasomee hata certificate tu jamani ili mpate walau basic principles tu...mnaongea utumbo kwenye magazeti na mnachafua jamiii kwa kuwaambukiza ujinga wenu!
 

Umesahau hii.....
"Majeraha kutokana na kufumaniwa na Mume wa mtu kabla hajakwenda kwa SK"
 
Daktari hawezi kudeclare kifo bila scientific proof weweeeeeee. hii inapatikana hospitali kwenye vipimo sahihi. Acheni mambo yaliyotokea Argentina ambako mtoto aliingizwa mochuari kumbe yu mzima!
 
Nakubaliana na womanofsubstance ni kweli na penda sana kazi ya Kanumba na hata nilitokwa na machozi nilipopata habari hii, lakini kabisa sikubali Kama Lulu amekusudia kumuua kwanza Hawa watu wanaonekana walikuwa wapenzi kwasababu wangekuwa hawana mahusiano Huyo binti asingekuwa kwa marehemu usiku ule mpaka wawe chumbanipamoja. Mimi kweli naomba wanasheria wamsaidie huyu binti hata Kama Ana tabia mbaya kwenye jamii. Pili ninaomba wachunguzi wa case hii wawe fair na watoe majibu yaliyo sahihi kwa Watanzania na sio kuangalia umaarufu wa marehemu na kuingiza hisia. Lulu bado ni mdogo na Ana nafasi ya kubadilika.
 
Brain concussion ambapo hakuna jiraha wala uvimbe kichwani kwa kanumba uliyo onekana! ...... Hapo napo kuna utata! Uchunguzi wa kina unahitajika! Kwa mtizamo wangu katika hali ya kawaida unapoanguka au kusukumwa mara nyingi viungo vya mwili(mikono, shingo nk) hulinda kichwa kisitangulie kufika chini.
Na je kama alijigonga kwanini kusiwepo na jiraha kichwani! Ni wengi ungekuta hatupo dunia kama kwa kuanguka na kujigonga unafariki.
 
minaona achunguzwe lulu,seth,dokta na aliyempigia simu lulu usiku labda kdg tutaanza kupata mwanga ktk hili tukio,pole kwa familia the great kanumba
 
Uko sahihi mkuu,suala hili hakuna anayelifahamu zaidi ya Lulu na polisi sisi wengine tuna shoia tu. Tupunguze ny*ge..tutajua ukweli tu.
 
Umesahau hii.....
"Majeraha kutokana na kufumaniwa na Mume wa mtu kabla hajakwenda kwa SK"


au majeraha kutoka kwa 'waukwee' yule dada aliyekuwa anasagana naye mpaka akamfanyia party, anayekaa sinza pia, yote yawezekana!
 
Mods Msiiondoe Hii Thread Please....
Kuna blog Flan imeandika some information kuhusu kilichotokea baada ya lulu Kuondoka nyumbani kwa Kanumba,
japokuwa n​i Blog ya Umbea lakini inaonekana kuna some few basic Question we have To weight and analyze....
both from our source and other informations,heb tuangalie point zifuatazo hapa chini,
  • Kwa mujibu wa Lulu...Kanumba alifikia hatua ya hadi Kutoa Panga Ili lulu amtaje ni nani alikua anongea nae kwenye Simu..(Hapa Lulu anasema ndipo Kanumba alipoanguka).
  • Lulu alikutwa Coco Beach na msanii fulani wa Nyimbo na kukamatwa na askari kanzu baada ya kanumba kudondoka (actually she was partying like nothing happened)
  • inadaiwa kuna baadhi ya watu walifika pale mapema na kuuondoa mwili wake hapo mapema(wataalamu wa forensic wataunganisha dots hapa) na baadhi ya mmoja wa watu hao inasemekana walikua hata hawaongei.
  • Post mortem inaonyesha ubongo ulikua umevimba na mapafu yamevilia damu (hapa dokta Riwa atatusaidia

Hii ni story ya upande mmoja tu,ukiangalia kwa umakini unaweza kuhisi kuna kitu,lakini wataalamu wanasema hakuna murder without motive...hapa naomba wale wataalam wa Criminal Investigation wanijengee hoja kwann isiwe huyu mtu alikua murdered au kuna posibilities za kuwa alikua murdered.

points to note:mwendazake alikua anakunywa pombe kali wakati tukio linatokea....
 
KOSA LA LULU NI KUWA KTK ENEO LA TUKIO LA KIFO . KWANZA HAKUNA USHAHIDI KAMA ALITUMIA RUNGU KUMPIGA KANUMBA, KIUKUBWA LULU ALIKUWA MWILI NA UZITO MDOGO KULIKO WA KANUMBA WAKATI WA TUKIO. HAKUNA USHAHIDI KAMA KANUMBA ALIKUWA MGONJWA WAKATI KIFO KINAMFIKA. LULU NI UNDER-AGE. KWA BAHATI MBAYA WATU WANATOA HUKUMU KWA LULU ON THE BASIS OF SYMPATHY OF THEIR BELOVED ACTOR. SUPPOSE INGEKUWA KINYUME CHAKE HALI INGEKUWAJE NADHANI WATU WANGESYMPATHISE NA KANUMBA NA KUMUONA LULU KAJITAKIA. LET US GIVE A FAIR GROUND IN THIS CASE NOT BASED ON OUR MENTAL INCLINATION TOWARDS KANUMBA AND AGAINST ELIZABETH MICHAEL. AFTERALL THE EVENT WAS JUST ACCIDENTAL AND NOT DELIBERATE ON THE GROUND THAT LULU KNOWING THE APPARENT SITUATION SHE WANTED TO RUN AWAY BUT KANUMBA WOULD HOLD HER BACK. NOW HOW DOES LULU COME INTO RESPONSIBLENESS TO THE DEATH OF KANUMBA?
OTHERWISE KUNA MAMBO YAMEJIFICHA NYUMA YA PAZI AMBAYO YANAPASWA KUANGALIWA KWA KINA ILI KUTOA CONCLUSIVE JUDGEMENT.Kifo hiki kimesikitisha watu wengi na kufanya udadisi wa kutaka kujua ukweli ulio objective iwe vigumu. Watu wamebakia kushusha lawama ZOTE kwa Lulu tu bila kutaka kujua haswa ilitokea nini hadi kifo hicho kikatokea.

 
Leo ni imetimia miaka 10, toka kifo cha nyota huyu wa Bongo Movies, Steven Kanumba, na mpaka Leo, sio tuu pengo lake halijazibika, bali hajapatikana star mwingine yoyote wa kuvaa viatu vyake vikamfiti.

RIP Steven Kanumba, tutakukumbuka milele!.
Paskali
 
Leo ni imetimia miaka 10, toka kifo cha nyota huyu wa Bongo Movies, Steven Kanumba, na mpaka Leo, sio tuu pengo lake halijazibika, bali hajapatikana star mwingine yoyote wa kuvaa viatu vyake vikamfiti.

RIP Steven Kanumba, tutakukumbuka milele!.
Paskali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…