"Ujinai" wa Lulu katika "mauaji" ya Kanumba (R.I.P)

"Ujinai" wa Lulu katika "mauaji" ya Kanumba (R.I.P)

nimeshashudia mtu akinyimwa huduma tena akiwa hoi bin taaban baada ya kukatwa mapanga akidhaniwa ni mwizi....
Na hakupata tiba mpaka ilipoendewa pf3

Anyway japo sitaweza kwa sasa kutoa kifungu cha sheria husika ila hilo hitaji lipo ILA hata juzi nilipojibu post mojawapo humu nilisema labda zipo exceptions na kuna baadhi ya watu walikuja waksema hivyo.

Sasa point yangu ni kuwa unaweza kuona hata uelewa wa hao madaktari kwenye sheria na taratibu za namna hii ulivyo...
Chukulia mfano wa huyu tabibu wa kanumba, alipoona hali kama ile yeye aliona cha muhimu ni kukimbiza mwili muhimbili? Regadless ya mazingira ya kifo chenyewe?
Sasa huyu kesho akinitimua niko hoi kisa sina pf3 sitashangaa...
btw: ntapekua juu ya kifungu husika bt not now. Au wataalam wakipita hapa pia wanaweza kunikosoa au kunisaidia

Huyo tabibu wa Kanumba ni Clinical Officer, Assistance Medical Officer au Medical Officer, maanake bongo kila mtu ni daktari.
 
Mkuu still hapo bado naona kama vile bado umeshikilia pale pale. Naamini defenses including self defence huwa zinakuja baada mshtakiwa kukubali kuwa ali-commit hiyo offence lakini alifanya hivyo kujilinda. Kuna umuhimu mkubwa wa kutofautisha kati ya plea of substantive defense and challenges made against factual evidence presented by the prosecution. Ni vitu viwili tofauti.

Kwa mfano, mtu akishtakiwa kwa assault causing GBH, mshtakiwa anaweza kukataa kuwa hakufanya hivyo by relying on an alibi or kudai kuwa kuna mistake of identify on the prosecution evidence. Hii ni tofauti na pale mshtakiwa anavyokubali kuwa s/he struck the victim but claims that s/he did so because the victim had been about to attack him/her. Hapo ndipo anapokuwa ana-raise the substantive defense of self-defence.

Wewe kama vile unaongelea plea ya self-defence to challenges against factual evidence presented by the prosecution. Hata kama ulikuwa unamaanisha the plea of substantive self-defense, ni kama vile tayari unakubali the fact that kuwa she actually struck the the victim. Did she? We don't know. Tumeambiwa tuu kulikuwa na arguments kati ya yeye na victim.

Whether kwenye hizo arguments waligusana to the extent ya kuanza kusukumana au hata kupigana, hatujui. Hata hii fact wanayosema alikimbilia nje, wanamaanisha nini by "nje"? Nje ya chumba, nje ya nyumba, au nje ya geti?

Mimi bado sijafika hata kwenye stage ya yeye kuraise the substantive defence of self-defense. Bado nipo kwenye preliminary issue ya did she cause the death in fact and in law? The prosecution must show this, ena beyond reasonable doubt. If not, lazima awe acquitted. If so, ndiyo zinakuja issues nyingine za aina ya homicide aliyo-commit and if there are any defenses she can rely on.

Mkuu nimekupata. Kama ulivyosema ameshtakiwa chini ya kifungu cha 196 (Murder). Kwa vile uchunguzi bado unaendelea itabidi tusubiri tuone kama DPP ata-stick na murder au atabadilisha kuwa manslaughter au hata ku-withdraw case kulingana na ushahidi utakaopatikana.
 
Mkuu nimekupata. Kama ulivyosema ameshtakiwa chini ya kifungu cha 196 (Murder). Kwa vile uchunguzi bado unaendelea itabidi tusubiri tuone kama DPP ata-stick na murder au atabadilisha kuwa manslaughter au hata ku-withdraw case kulingana na ushahidi utakaopatikana.
yap. lakini withdrawal yake inakuwa kwa njia ya NOLLE PROSEQUI. state attorney anapoandika opinion yake (hawa wanamwakilisha dpp hasa through their incharge boss) huwa anafikia uamuzi mbalimbali ambao moja wapo ni kusuggest nolle, kusuggest certain charge etc. ila kwa kuliondoa huwa linaondolewa na nolle tu. hakuna njia nyingine. inatumika section 91(1) CPA....CAP 20.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
MSANIInyota wa filamu nchini, Steven Kanumba amefariki dunia kutokana na tatizo lamtikisiko wa ubongo linalojulikana kitalaamu kama Brain Concussion, taarifa zakitabibu zimeeleza.Taarifahizo za ndani, zilizopatikana jana baada ya jopo la madaktari bingwa watano waHospitali ya Taifa Muhimbili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu huyo,zimeeleza kuwa tatizo hilo linaweza kumfanya mtu apoteze maisha mara moja aubaada ya siku kadhaa. Mmoja wa madaktari hao ambaye aliomba jina lake lisitajwegazetini alisema waligundua tatizo hilo baada ya kumfanyia uchunguzi huo kwazaidi ya saa mbili.“Tulianza kuufanyia uchunguzi mwili wamarehemu kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 6:45 mchana na tukagundua kuwamarehemu alifariki kutokana na mtikisiko wa ubongo kwa kitaalamu, BrainConcussion,” alisema daktari huyo. Alisema Kanumba alipata mtikisiko wa ubongoambao husababisha kufeli kwa mfumo wa upumuaji (cardio-respiratory failure)“Kilichomuua hasa ni mtikisiko wa ubongo, ambao endapo unatokea katika sehemuya nyuma ya ubongo (cerebrum), huua kwa haraka” alisema daktari huyo nakuongeza kuwa mtikisiko wa ubongo wa nyuma, husababisha matatizo ya mfumo waupumuaji na hilo limeonekana katika mwili wake.
“Baada ya ubongo wake kutikiswa kwa nguvu,mfumo wa upumuaji ulifeli na ndiyo maana tumekuta kucha za Kanumba zikiwa narangi ya bluu, huku mapafu yake yakiwa yamevilia damu na kubadilika kuwa kamamaini, hizo ndizo dalili za kufeli kwa mfumo wa upumuaji.”
“Mtu aliyepatamtikisiko wa ubongo huweza kutokwa na mapovu mdomoni na hukoroma kabla yakukata roho na ndivyo ilivyokuwa kwa Kanumba kabla hajafariki.”(Kutokagazeti la mwananchi)

Kutokana na vitabu mbalimbali vya medicine...kwa kifupi, concussionni traumatic brain injury. Kwa maneno mengine, external physical force ambayo inaweza kutokana na kupigwa na kitukizito kichwani, kuangukia kichwa, accident, sports etc husababisha head injury ambayo husababisha brain injury (concussion).Watoto wadogo wanaweza kupata traumatic brain injury (concussion) kwa kutikiswakwa nguvu - ‘shaken baby syndrome’.

Kuna non traumatic brain injuries ambazo husababishwa na vitu kama stroke, infections eg meningitis, tumors, poisoning including alcohol poisoning na mengineyo mengi...ila hii aina ya brain injury haiwezi kuwa diagnosed as concussion kwa sababu hakuna trauma involved.

Traumatic brain injury (concussion) na non traumatic brain injury zinaweza kutafautishwa kwa kuangalia1. history eg je kulikuwa na accident, sports,violence, ugonjwa, uvimbe kichwani etc? 2. Symptoms,3. head CT/MRI pia huonyesha tofauti katika ya hizi brain injuries. Japo kulikuwana ugomvi/violence bado sielewi inakuwaje mtu anapata severe concussion iliyosababisha kifo baada ya muda mfupi bila jeraha au uvimbe wowote kichwani...

Kutoka povu kidogo mdomoni ni kitu cha kawaida mtu anapokufa kwa sababu yoyote ile, ila povu jingi ni moja ya symptom za matatizo kwenye mfumo wa chakula(gastrointestinal) zaidi kuliko concussion.

Kwa mtazamo wangu vigezo walivyotoa madaktari bado havitoshi kusema cause of death ni concussion...head imaging investigations zinaonyesha nini? aina zote za brain injury huweza kusababisha kufeli kwamfumo wa upumuaji. Kwanini hawakusubiri kupata majibu ya vipimo vyote (maini etc)kabla ya kuzika?. Tusubiri taarifa rasmi, maana hii ni kutoka "taarifa za ndani"...

 
Kaka umenigusa sana nimeshakaribia gombana na marafiki zangu juu ya Lulu, tumwache mahakama ifanye uchunguzi na naimani She is innocent kwani hajampa sumu labda katika kujiokoa ikawa vile. Mungu Atampigania kwani yeye ndo mpanga tarehe.

mungu atamjalia kwani ambao wanamshutumu wengi wao ni ambao wanachuki binafsi juu yake na wengine kutokana na ujinga tu!
 
MSANIInyota wa filamu nchini, Steven Kanumba amefariki dunia kutokana na tatizo lamtikisiko wa ubongo linalojulikana kitalaamu kama Brain Concussion, taarifa zakitabibu zimeeleza.Taarifahizo za ndani, zilizopatikana jana baada ya jopo la madaktari bingwa watano waHospitali ya Taifa Muhimbili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu huyo,zimeeleza kuwa tatizo hilo linaweza kumfanya mtu apoteze maisha mara moja aubaada ya siku kadhaa. Mmoja wa madaktari hao ambaye aliomba jina lake lisitajwegazetini alisema waligundua tatizo hilo baada ya kumfanyia uchunguzi huo kwazaidi ya saa mbili."Tulianza kuufanyia uchunguzi mwili wamarehemu kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 6:45 mchana na tukagundua kuwamarehemu alifariki kutokana na mtikisiko wa ubongo kwa kitaalamu, BrainConcussion," alisema daktari huyo. Alisema Kanumba alipata mtikisiko wa ubongoambao husababisha kufeli kwa mfumo wa upumuaji (cardio-respiratory failure)"Kilichomuua hasa ni mtikisiko wa ubongo, ambao endapo unatokea katika sehemuya nyuma ya ubongo (cerebrum), huua kwa haraka" alisema daktari huyo nakuongeza kuwa mtikisiko wa ubongo wa nyuma, husababisha matatizo ya mfumo waupumuaji na hilo limeonekana katika mwili wake."Baada ya ubongo wake kutikiswa kwa nguvu,mfumo wa upumuaji ulifeli na ndiyo maana tumekuta kucha za Kanumba zikiwa narangi ya bluu, huku mapafu yake yakiwa yamevilia damu na kubadilika kuwa kamamaini, hizo ndizo dalili za kufeli kwa mfumo wa upumuaji.""Mtu aliyepatamtikisiko wa ubongo huweza kutokwa na mapovu mdomoni na hukoroma kabla yakukata roho na ndivyo ilivyokuwa kwa Kanumba kabla hajafariki."(Kutokagazeti la mwananchi) Kutokana na vitabu mbalimbali vya medicine...kwa kifupi, concussionni traumatic brain injury. Kwa maneno mengine, external physical force ambayo inaweza kutokana na kupigwa na kitukizito kichwani, kuangukia kichwa, accident, sports etc husababisha head injury ambayo husababisha brain injury (concussion).Watoto wadogo wanaweza kupata traumatic brain injury (concussion) kwa kutikiswakwa nguvu - ‘shaken baby syndrome'. Kuna non traumatic brain injuries ambazo husababishwa na vitu kama stroke, infections eg meningitis, tumors, poisoning including alcohol poisoning na mengineyo mengi...ila hii aina ya brain injury haiwezi kuwa diagnosed as concussion kwa sababu hakuna trauma involved. Traumatic brain injury (concussion) na non traumatic brain injury zinaweza kutafautishwa kwa kuangalia1. history eg je kulikuwa na accident, sports,violence, ugonjwa, uvimbe kichwani etc? 2. Symptoms,3. head CT/MRI pia huonyesha tofauti katika ya hizi brain injuries. Japo kulikuwana ugomvi/violence bado sielewi inakuwaje mtu anapata severe concussion iliyosababisha kifo baada ya muda mfupi bila jeraha au uvimbe wowote kichwani...Kutoka povu kidogo mdomoni ni kitu cha kawaida mtu anapokufa kwa sababu yoyote ile, ila povu jingi ni moja ya symptom za matatizo kwenye mfumo wa chakula(gastrointestinal) zaidi kuliko concussion.Kwa mtazamo wangu vigezo walivyotoa madaktari bado havitoshi kusema cause of death ni concussion...head imaging investigations zinaonyesha nini? aina zote za brain injury huweza kusababisha kufeli kwamfumo wa upumuaji. Kwanini hawakusubiri kupata majibu ya vipimo vyote (maini etc)kabla ya kuzika?. Tusubiri taarifa rasmi, maana hii ni kutoka "taarifa za ndani"...
taarifa ya daktari pekee (au expert opinion ya mtu yeyote yule), si pekee inayoamua ujinai wa mtu na sio binding, kama kuna ushahidi mwingine mzuri taarifa ya daktari inaweza wekwa hata pembeni. pia kumbuka tunasubiri pia majibu ya government chemisty(mkemia mkuu). nakushauri usisikilize au kuingiza ushabiki wa waandishi wa habari, utalala mlango wazi. waandishi wengi wa habari tz ni makanjanja, wanawezashabikia habari fulani utafikiri wanaelewa kitu chenyewe kumbe ni mambumbumbu wa kutupwa. angalia wale wa clouds fm kina kibonde.....hii ni issue ya kisheria, sheria ni profession ambayo ni nyeti sana kama huzijui principles zake, unaweza kuchangia kitu ukajianika ujinga wako vibaya mno. Napendekeza sana mimi siku zote, waandishi wa habari waende wakasome shule, na pia vyombo vya media viwe vinaajiri waandishi wa habari wenye profession tofautitofauti ili matu anapotoa au kuchunguza habari ili aitoe aende kiprofession. mfano: vyombo vingine ulaya, vinaajiri wanasheria na wanauchumi etc kuwa waandishi wa habari, hii ni baada ya labda mtu kuwa mwanasheria lakini anaenda pia kusomea uandishi wa habari etc. sasa ikitokea kuchunguza jambo la kiuchumi ili walitoe hewani yule mwanauchumi ndo nafasi yake hiyo, na habari itakayotolewa itakuwa bora kuliko habari ambayo Efrahim kibonde angeitoa...hahaha, hivyo hivyo na kwa wanasheria....basi nendeni mkasomee hata certificate tu jamani ili mpate walau basic principles tu...mnaongea utumbo kwenye magazeti na mnachafua jamiii kwa kuwaambukiza ujinga wenu!
 
kuumizwa kwa lulu(majeraha) kulitokana na nini?
Kipigo kutoka kwa kanumba?
Kipigo kutoka kwa seth?
Kipigo kutoka kwa polisi wakati wa mahojiano?
Kipigo kutoka kwa majirani au mashabiki wa kanumba?
Majeraha ya kujipandikiza(self inflicted)?
Majeraha kabla ya kufika kwa kanumba(labda wazazi walimpiga)?
................
Hapa ndipo tutakapoona weledi wa forensic investigators nchini kwetu.

Umesahau hii.....
"Majeraha kutokana na kufumaniwa na Mume wa mtu kabla hajakwenda kwa SK"
 
Daktari hawezi kudeclare kifo bila scientific proof weweeeeeee. hii inapatikana hospitali kwenye vipimo sahihi. Acheni mambo yaliyotokea Argentina ambako mtoto aliingizwa mochuari kumbe yu mzima!
 
Nakubaliana na womanofsubstance ni kweli na penda sana kazi ya Kanumba na hata nilitokwa na machozi nilipopata habari hii, lakini kabisa sikubali Kama Lulu amekusudia kumuua kwanza Hawa watu wanaonekana walikuwa wapenzi kwasababu wangekuwa hawana mahusiano Huyo binti asingekuwa kwa marehemu usiku ule mpaka wawe chumbanipamoja. Mimi kweli naomba wanasheria wamsaidie huyu binti hata Kama Ana tabia mbaya kwenye jamii. Pili ninaomba wachunguzi wa case hii wawe fair na watoe majibu yaliyo sahihi kwa Watanzania na sio kuangalia umaarufu wa marehemu na kuingiza hisia. Lulu bado ni mdogo na Ana nafasi ya kubadilika.
 
Brain concussion ambapo hakuna jiraha wala uvimbe kichwani kwa kanumba uliyo onekana! ...... Hapo napo kuna utata! Uchunguzi wa kina unahitajika! Kwa mtizamo wangu katika hali ya kawaida unapoanguka au kusukumwa mara nyingi viungo vya mwili(mikono, shingo nk) hulinda kichwa kisitangulie kufika chini.
Na je kama alijigonga kwanini kusiwepo na jiraha kichwani! Ni wengi ungekuta hatupo dunia kama kwa kuanguka na kujigonga unafariki.
 
minaona achunguzwe lulu,seth,dokta na aliyempigia simu lulu usiku labda kdg tutaanza kupata mwanga ktk hili tukio,pole kwa familia the great kanumba
 
Amini usiaminni, huwezi kujadili jambo hili bila kupata maelezo ya Lulu na seth toka kwenye jalada kule polisi ukalisoma. Na hayo maelezo ndiyo yatakayopelekwa kwa mawakili wa serikali ili kulingana na maelezo hayo ya yale ya mashahidi wengine, wadetermine kama itakuwa murder or manslaughter.

However, it is most likely kuwa maslaughter kwa mtazamo wa juu juu, hata hivyo hatuwezi kusema chochote bila kusoma maelezo ya cautioned statements na yale ya mashahidi ambayo yapo kule polisi. zaidi ya hapo, kujadili jambo ambalo hujui facts zake vizuri, ni kutwanga maji kwenye kinu.
Uko sahihi mkuu,suala hili hakuna anayelifahamu zaidi ya Lulu na polisi sisi wengine tuna shoia tu. Tupunguze ny*ge..tutajua ukweli tu.
 
Umesahau hii.....
"Majeraha kutokana na kufumaniwa na Mume wa mtu kabla hajakwenda kwa SK"


au majeraha kutoka kwa 'waukwee' yule dada aliyekuwa anasagana naye mpaka akamfanyia party, anayekaa sinza pia, yote yawezekana!
 
Mods Msiiondoe Hii Thread Please....
Kuna blog Flan imeandika some information kuhusu kilichotokea baada ya lulu Kuondoka nyumbani kwa Kanumba,
japokuwa n​i Blog ya Umbea lakini inaonekana kuna some few basic Question we have To weight and analyze....
both from our source and other informations,heb tuangalie point zifuatazo hapa chini,
  • Kwa mujibu wa Lulu...Kanumba alifikia hatua ya hadi Kutoa Panga Ili lulu amtaje ni nani alikua anongea nae kwenye Simu..(Hapa Lulu anasema ndipo Kanumba alipoanguka).
  • Lulu alikutwa Coco Beach na msanii fulani wa Nyimbo na kukamatwa na askari kanzu baada ya kanumba kudondoka (actually she was partying like nothing happened)
  • inadaiwa kuna baadhi ya watu walifika pale mapema na kuuondoa mwili wake hapo mapema(wataalamu wa forensic wataunganisha dots hapa) na baadhi ya mmoja wa watu hao inasemekana walikua hata hawaongei.
  • Post mortem inaonyesha ubongo ulikua umevimba na mapafu yamevilia damu (hapa dokta Riwa atatusaidia

Hii ni story ya upande mmoja tu,ukiangalia kwa umakini unaweza kuhisi kuna kitu,lakini wataalamu wanasema hakuna murder without motive...hapa naomba wale wataalam wa Criminal Investigation wanijengee hoja kwann isiwe huyu mtu alikua murdered au kuna posibilities za kuwa alikua murdered.

points to note:mwendazake alikua anakunywa pombe kali wakati tukio linatokea....
 
KOSA LA LULU NI KUWA KTK ENEO LA TUKIO LA KIFO . KWANZA HAKUNA USHAHIDI KAMA ALITUMIA RUNGU KUMPIGA KANUMBA, KIUKUBWA LULU ALIKUWA MWILI NA UZITO MDOGO KULIKO WA KANUMBA WAKATI WA TUKIO. HAKUNA USHAHIDI KAMA KANUMBA ALIKUWA MGONJWA WAKATI KIFO KINAMFIKA. LULU NI UNDER-AGE. KWA BAHATI MBAYA WATU WANATOA HUKUMU KWA LULU ON THE BASIS OF SYMPATHY OF THEIR BELOVED ACTOR. SUPPOSE INGEKUWA KINYUME CHAKE HALI INGEKUWAJE NADHANI WATU WANGESYMPATHISE NA KANUMBA NA KUMUONA LULU KAJITAKIA. LET US GIVE A FAIR GROUND IN THIS CASE NOT BASED ON OUR MENTAL INCLINATION TOWARDS KANUMBA AND AGAINST ELIZABETH MICHAEL. AFTERALL THE EVENT WAS JUST ACCIDENTAL AND NOT DELIBERATE ON THE GROUND THAT LULU KNOWING THE APPARENT SITUATION SHE WANTED TO RUN AWAY BUT KANUMBA WOULD HOLD HER BACK. NOW HOW DOES LULU COME INTO RESPONSIBLENESS TO THE DEATH OF KANUMBA?
OTHERWISE KUNA MAMBO YAMEJIFICHA NYUMA YA PAZI AMBAYO YANAPASWA KUANGALIWA KWA KINA ILI KUTOA CONCLUSIVE JUDGEMENT.Kifo hiki kimesikitisha watu wengi na kufanya udadisi wa kutaka kujua ukweli ulio objective iwe vigumu. Watu wamebakia kushusha lawama ZOTE kwa Lulu tu bila kutaka kujua haswa ilitokea nini hadi kifo hicho kikatokea.

Naanza na kutoa Pole kwa watanzania wote, hasa ndugu jamaa na marafiki wa karibu wa Kanumba The Great (R.I.P) kabla sijatoa mchango wangu kuhusu hili jambo zito na nyeti ambalo limetawala maongezi katika kipindi hiki cha Sikukuu ya Pasaka. Mengi yamesemwa na pia kuna mengi pia hayajasemwa, moja wapo likiwa "ujinai" wa Lulu katika kifo cha Kanumba.

Katika mukatadha wa sheria, tunaona kwamba Tanzania ni moja ya nchi zenye kuuweka uwajibikaji kijinai kuwa chini ya UMRI wa miaka 18 kwa kuweka miaka 10 kama umri ambapo mtu anaweza kushtakiwa kwa kosa la jinai. (Linganisha na Kenya miaka 8, Zimbabwe -7,Zambia 8,Africa Kusini 10) n.k. Ina maana kwamba mtu (mtoto) aliye chini ya umri huu hawezi kushtakiwa labda ithibitishwe kuwa alikua anajua kabisa anachokifanya. Lulu hafit kwenye kundi hili hata kama ana umri wa miaka 17 kama ambavyo Mh Halima Mdee ame tweet leo baada ya kumtembelea LuLU Oysterbay Polisi.

Tukiacha sheria na matakwa yake, kwa kuzingatia yale yanayosemwa kuhusu mkasa huu wa kifo cha Kanumba (R.I.P), inatupasa tuone kuwa kila hadithi ina pande mbili. Hadithi ya Kanumba ambaye kwa sasa hayupo kuelezea, na hadithi ya Lulu aliye mahabusu. Inasikitisha sana kwamba kifo kimetokea katika mazingira ya kutatanisha. Kifo hiki kimesikitisha watu wengi na kufanya udadisi wa kutaka kujua ukweli ulio objective iwe vigumu. Watu wamebakia kushusha lawama ZOTE kwa Lulu tu bila kutaka kujua haswa ilitokea nini hadi kifo hicho kikatokea.

Kama watanzania wengine napenda niseme kwamba , nahuzunika kama wengine kumpoteza Kanumba na pia kuona ndoto zake kama msanii zikizimwa ghafla. Aidha wapenzi wake wamekatishwa ile raha ya kuendelea kuburidika na filamu zake. Pamoja kuwa na huzuni kuu, pia najaribu kuangalia upande wa pili – Lulu! Huyu binti wa miaka 17/18 kijamii bado ni msichana mdogo japo kisheria hasamehewi kuwajibishwa kijinai. Lakini uwajibishwaji huo utakuja pale upelelezi utakapokamilika. Kufuatana na waliobahatika kumuona huyu binti, ana majeraha kuashiria kuwa alipigwa na kuumizwa na marehemu. Ingekuwa marehemu hakufa, basi nadhani kesi hii ingekuwa ya aina yake kama ingefika kunakohusika. Wote walijeruhiana. Lakini mazingira ya kujeruhi huko ni yepi?

Tumeambiwa na hata kusoma kwamba:

1. Lulu alienda kwa Kanumba usiku mkali mishale ya saa 6, kusudi watoke kwenda kucheza muziki kwa msanii Chaz baba – Mashujaa band ( Kanumba alishapiga simu kutaka andaliwe viti na sehemu maalum ya kukaa yeye na marafiki zake na pia akiomba hata wimbo maalum atakapofika)
2. Lulu alitoka nje kusikiliza simu – Kanumba akamfuata na kumrudisha ndani ili aeleze anaongea na nani.( Hapa tunaona kabisa Kanumba akianzisha shari yeye mwenyewe badala ya kuepuka shari)
3. Kanumba alimfungia Lulu ndani wakawa wanagombana. Aggressor hapa ni Kanumba na siyo Lulu.Kelele za ugomvi ziliashiria vurugu na kwa vile mlango ulifungwa na ufunguo, ilikuwa vigumu Lulu kukimbia tena au hata watu nje kuja kutoa msaada.
4. Lulu alitoka nje kwenda kumwita Seth na kumwambia Kanumba kaanguka.Lulu alikimbia akiwa na majeraha.Hii haionyeshi kuwa Lulu aliua vinginevyo angetoka kimya kimya akatokomea.

Sasa ndugu zanguni, kwanini Lulu anaonekana alifanya mauaji ya kukusudia? Ikiwa Kanumba alianguka katika purukushani na kuponda kichwa na kufa, Lulu kaua vipi? Kukamatwa na polisi na kushikiliwa ili kusaidia uchunguzi ni utaratibu wa kawaida sana. Nimewahi kushuhudia mtu kajiua, ndugu yake na mkewe waliomgundua kajining'iniza walikamatwa wakakaa ndani ili wasaidie uchunguzi Ilahali mtu kajiua mwenyewe. Ilisikitisha sana kwa maana wafiwa walitiwa misukosuko kwa kifo ambacho marehemu alijiletea kwa kujitundika. Walikaa masaa kadhaa kabla ya ndugu kwenda kuwatetea na kushinikiza waachiwe!

Kwenye hii kesi ya Lulu, bahati mbaya sana Lulu ana sifa mbaya kwenye jamii kiasi kwamba hakuna mtu anathubutu kumtetea na kumsaidia angalau aweze kujipanga kukabiliana na siku za kusubiri hatma baada ya upelelezi. Kibaya zaidi kuna statements za watu wazito ndani ya jamii, statements ambazo zenyewe tu zimeshapasisha kwamba Lulu ndio muuaji. Kibaya zaidi, unyeti wa hali inayozunguka msanii maarufu kipenzi cha wengi utaathiri hata mwenendo mzima wa upelelezi na kitakachojiri to the detriment of Lulu.

Nadhani kwa vile hii haijawa kesi ya kimahakama, na kwa vile jamii inazungumzia hiki kifo, hakuna ubaya tukawa na scenario zote.

Sijaandika haya kwa vile nataka kumsemea Lulu asiwajibike kama anahusika kijinai bali najaribu kupanua mjadala.

Nawasilisha.
WoS.
 
WOS, asante kwa hii.
Leo nimefanikiwa kufika msibani na kuzungumza 3rd witness at the scene, kiukweli kinachoripotiwa kumhusu huyu binti, sicho kilichotokea!. Rest assured hicho nilichosikia kama sio uwongo mwingine, then huyu binti ni innocent victim wa male aggression na Kanumba ameanguka mwenyewe!. Lets wait and see!.
Leo ni imetimia miaka 10, toka kifo cha nyota huyu wa Bongo Movies, Steven Kanumba, na mpaka Leo, sio tuu pengo lake halijazibika, bali hajapatikana star mwingine yoyote wa kuvaa viatu vyake vikamfiti.

RIP Steven Kanumba, tutakukumbuka milele!.
Paskali
 
Kanumba alipoanguka, alizimika there and then it was all over, hiyo JD aliinywea nyumbani aliporudi ili atoke, kabla ya hapo alikuwa mahali pengine na alikunywa pombe nyingine hivyo wakati ugomvi unatokea, alikuwa heavily intoxiticated!.

Kwanza alitoka kama alivyo kuripoiti Kanumba kaanguka, wakati wakihangaika ni mwili, alichukua nguo zake akatafuta mahali muafa ku dress up and run away ikiwa ni pamoja na kuzima simu. News za kifo zilipofika asubuhi, akawasha na kumtextia someone kuwa anataka kujiua, huyo mtu akawanotify police, wakamtumia kumzuga zunga huku akimwahidi msaada ndipo akawaelekeza alipo, jamaa akafika na police na kumdaka.

Nimeongea na huyu jamaa, pia jamaa aliye mdress Kanumba, end of the game ilikuwa ni pale pale, wale wasanii walijua he was dead na bado waliendelea kupiga picha his dead body, shame on them!q1
Leo ni imetimia miaka 10, toka kifo cha nyota huyu wa Bongo Movies, Steven Kanumba, na mpaka Leo, sio tuu pengo lake halijazibika, bali hajapatikana star mwingine yoyote wa kuvaa viatu vyake vikamfiti.

RIP Steven Kanumba, tutakukumbuka milele!.
Paskali
 
Back
Top Bottom