MSANIInyota wa filamu nchini, Steven Kanumba amefariki dunia kutokana na tatizo lamtikisiko wa ubongo linalojulikana kitalaamu kama Brain Concussion, taarifa zakitabibu zimeeleza.Taarifahizo za ndani, zilizopatikana jana baada ya jopo la madaktari bingwa watano waHospitali ya Taifa Muhimbili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu huyo,zimeeleza kuwa tatizo hilo linaweza kumfanya mtu apoteze maisha mara moja aubaada ya siku kadhaa. Mmoja wa madaktari hao ambaye aliomba jina lake lisitajwegazetini alisema waligundua tatizo hilo baada ya kumfanyia uchunguzi huo kwazaidi ya saa mbili."Tulianza kuufanyia uchunguzi mwili wamarehemu kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 6:45 mchana na tukagundua kuwamarehemu alifariki kutokana na mtikisiko wa ubongo kwa kitaalamu, BrainConcussion," alisema daktari huyo. Alisema Kanumba alipata mtikisiko wa ubongoambao husababisha kufeli kwa mfumo wa upumuaji (cardio-respiratory failure)"Kilichomuua hasa ni mtikisiko wa ubongo, ambao endapo unatokea katika sehemuya nyuma ya ubongo (cerebrum), huua kwa haraka" alisema daktari huyo nakuongeza kuwa mtikisiko wa ubongo wa nyuma, husababisha matatizo ya mfumo waupumuaji na hilo limeonekana katika mwili wake."Baada ya ubongo wake kutikiswa kwa nguvu,mfumo wa upumuaji ulifeli na ndiyo maana tumekuta kucha za Kanumba zikiwa narangi ya bluu, huku mapafu yake yakiwa yamevilia damu na kubadilika kuwa kamamaini, hizo ndizo dalili za kufeli kwa mfumo wa upumuaji.""Mtu aliyepatamtikisiko wa ubongo huweza kutokwa na mapovu mdomoni na hukoroma kabla yakukata roho na ndivyo ilivyokuwa kwa Kanumba kabla hajafariki."(Kutokagazeti la mwananchi) Kutokana na vitabu mbalimbali vya medicine...kwa kifupi, concussionni traumatic brain injury. Kwa maneno mengine, external physical force ambayo inaweza kutokana na kupigwa na kitukizito kichwani, kuangukia kichwa, accident, sports etc husababisha head injury ambayo husababisha brain injury (concussion).Watoto wadogo wanaweza kupata traumatic brain injury (concussion) kwa kutikiswakwa nguvu - ‘shaken baby syndrome'. Kuna non traumatic brain injuries ambazo husababishwa na vitu kama stroke, infections eg meningitis, tumors, poisoning including alcohol poisoning na mengineyo mengi...ila hii aina ya brain injury haiwezi kuwa diagnosed as concussion kwa sababu hakuna trauma involved. Traumatic brain injury (concussion) na non traumatic brain injury zinaweza kutafautishwa kwa kuangalia1. history eg je kulikuwa na accident, sports,violence, ugonjwa, uvimbe kichwani etc? 2. Symptoms,3. head CT/MRI pia huonyesha tofauti katika ya hizi brain injuries. Japo kulikuwana ugomvi/violence bado sielewi inakuwaje mtu anapata severe concussion iliyosababisha kifo baada ya muda mfupi bila jeraha au uvimbe wowote kichwani...Kutoka povu kidogo mdomoni ni kitu cha kawaida mtu anapokufa kwa sababu yoyote ile, ila povu jingi ni moja ya symptom za matatizo kwenye mfumo wa chakula(gastrointestinal) zaidi kuliko concussion.Kwa mtazamo wangu vigezo walivyotoa madaktari bado havitoshi kusema cause of death ni concussion...head imaging investigations zinaonyesha nini? aina zote za brain injury huweza kusababisha kufeli kwamfumo wa upumuaji. Kwanini hawakusubiri kupata majibu ya vipimo vyote (maini etc)kabla ya kuzika?. Tusubiri taarifa rasmi, maana hii ni kutoka "taarifa za ndani"...