"Ujinai" wa Lulu katika "mauaji" ya Kanumba (R.I.P)

"Ujinai" wa Lulu katika "mauaji" ya Kanumba (R.I.P)

angalau kuna mtu alienda kumuona huyu mtoto!
Halima mdee amefanya la maana sana,ningekua dar ningeenda pia
ningekua mwanasheria ningeisubiri kama kuna "kesi/tuhuma" baada ya upelelezi kwa huyu mtoto

ngoja tuone mwisho wake!!
 
Duh, Namuonea huruma sana huyu binti., I wish ningekuwa mwanasheria nikamtetee hadi mwisho.Hii kesi sio ngumu sana kwa Lulu kama akipata mwanasheria mzuri.
hiii kesi ni ngumu, usiseme sio ngumu, ni kwamba tukio hili limemweka lulu katika hali ya kuharibiwa maisha, hata akitoka leo hii itamwathiri maisha yake yote, cha kuelewa ni kwamba, kuanzia sasaivi hadi siku upelelezi utakapokamilika na yeye kufungiwa PI (to be committed to the High court), itachukua muda kwa wapelelezi wa hapa tz, hata miaka miwili, muda wote huo atakuwa ndani. jalada likipelekwa kwa state attorney wakaangalia aina ya kosa la kumshitaki kulingana na maelezo ya mashahidi basi hapo ndo ataweza kupata dhamana kupitia high court kama itakuwa proposed kwamba ashitakiwe kwa manslaughter. baada ya hapo, atafungw amiaka michache tu, wkasababu kwa mazingira halisi, hii ilikuwa bahati mbaya na labda ilitokana na kupigana ambako kisheria huishia kwenye manslaughter. lakini kwa sasa, naweza sema uyu mtoto atatumikia jela si chini ya miaka minne kuanzia sasa, kusubiria upelelezi hadi kesi kusikilizwa. miaka hii kuishi jela si michache. akitoka future yote imeharibika. namwonea huruma sana.
 
Kaka hapa ndo uwezo wa jeshi la polisi unapopimwa, kama kzi yao ni kufyatua mabomu ya machozi tu au wanaweza kutafuta haki iliyofichika pia!

Sidhani kama polisi wana hao wataalamu; angalau ofisi ya chief/district medical examiner , kama ipo, inaweza kufanya hiyo kazi.
 
Tumeambiwa na hata kusoma kwamba:

1. Lulu alienda kwa Kanumba usiku mkali mishale ya saa 6, kusudi watoke kwenda kucheza muziki kwa msanii Chaz baba – Mashujaa band ( Kanumba alishapiga simu kutaka andaliwe viti na sehemu maalum ya kukaa yeye na marafiki zake na pia akiomba hata wimbo maalum atakapofika)
2. Lulu alitoka nje kusikiliza simu – Kanumba akamfuata na kumrudisha ndani ili aeleze anaongea na nani.( Hapa tunaona kabisa Kanumba akianzisha shari yeye mwenyewe badala ya kuepuka shari)
3. Kanumba alimfungia Lulu ndani wakawa wanagombana. Aggressor hapa ni Kanumba na siyo Lulu.Kelele za ugomvi ziliashiria vurugu na kwa vile mlango ulifungwa na ufunguo, ilikuwa vigumu Lulu kukimbia tena au hata watu nje kuja kutoa msaada.
4. Lulu alitoka nje kwenda kumwita Seth na kumwambia Kanumba kaanguka.Lulu alikimbia akiwa na majeraha.Hii haionyeshi kuwa Lulu aliua vinginevyo angetoka kimya kimya akatokomea.
WoS.

WoS,

Nafikiri tatizo kubwa tulilo nalo ni kwamba hatuna facts za kesi. Facts tulizonazo ni speculations tuu na hatuwezi ku-rely on them ili angalao tuanze ku-formulate issues na kuangalia sheria ipi ambayo inaweza kutumika. Kwa hiyo, unless we get all the necessary facts hatutaweza kujua ni sheria ipi ambayo itamukika.

Kuna watu tayari wameshaanza kuongelea sijui murder or maslaughter bila hata kuangalia principles za causation. Kama tungeweza kupata fact za kesi hii, nafikiri kitu cha kwanza ni kuangalia ni nani hasa aliyesabisha kifo cha Kanumba. Hapa ndipo principles of causation zinapoingia. Did Lulu caused his death? Hapa itatubidi tuangalie the causation in fact and causation in law.

Causation in fact, ndipo panapokuja the "but for" test (whether Lulu in fact caused the death). Then, uje kwenye causation in law ( mambo ya operative and substantial cause, reasonable foreseeablity, etc). Lakini kwa hizi speculations facts tulizo nazo ni vigumu sana ku-rely on them kujaribu hata ku-determine whether she caused the death in fact.
 
Nashukuru sana kwa kufafanua haswa kwenye swala la umri kwa kuwa mimi @Sirbasjoe nilitofautiana sana na twitterers kwenye hilo swala la umri japo sikuwa na data lakini niliamini miaka kumi na saba si mdogo kwa makosa ya jinai.
Bila kupinga maelezo yeyote uliyoyatoa kwa kuwa sijui mazingira mazima ya tukio hili lakini nikichukulia ndiyo yaliyotokea lakini kwa kuwa hatujui kiukweli nini kilimuua Kanumba basi hata hayo mazingira hayatoshi kwa yeyote kutoa majumuisho.
Hivyo Sisi tunachopenda ni kuwa sheria ifuatwe au in english..."Due process" ili haki itendeke maana kama sheria isipofuatwa vizuri Kanumba na familia wanaweza wasipate haki yako au tukapata victim mwingine yaani mtu akabeba kesi isiyokuwa yake.
Uchunguzi wa kesi ya mauaji ni mrefu (Tanzania huchukua hadi miaka mitano kesi kufika mahakama kuu).. na hivyo jukumu letu pia ni kutumia hii nafasi kudai haki za watuhumiwa zizingatiwe, uchunguzi ufanyike mapema, ucheleweshwaji uondolewe, utaratibu ufuatwe. hizo ni sehemu ya mabadiliko tunayoyataka Tanzania.
@Sirbasjoe
 
angalau kuna mtu alienda kumuona huyu mtoto!
Halima mdee amefanya la maana sana,ningekua dar ningeenda pia
ningekua mwanasheria ningeisubiri kama kuna "kesi/tuhuma" baada ya upelelezi kwa huyu mtoto

ngoja tuone mwisho wake!!
Na usije kushangazwa kama weekend ijayo mtakutana naye Ngwasuma maana nchi kila kitu kina wezekani.......labda kama alikuwa mchoyo kwa Wazee wa System, lakini kama aliwahi kutoa tunda angalau kwa raia mmoja wa pale magogoni basi nakuhakikishia she is out without any charge
 
Wakati gani sasa walimvisha marehemu? Kabla au baada ya polisi kuja?(i am just curious)
Biashara ya polisi imefanyika asubuhi!. By the time daktari wa K anafika pale, he was no more long ago alimkuta cold!, eti aliogopa kusema the game is over ili watu wasi panic. Tukio limeripotiwa polisi baada ya mwili kufikishwa Muhimbili na kukataliwa kupokelewa kwanza bila PF.3.

Hao polisi walifika nyumbani asubuhi ndio kukuta hiyo JD kwenye glass.

Kuikweli kwenye investigation, polisi wetu ni bure kabisa!, sio tuu wana uwezo duni, bali hata interest hawana!. Ingekuwa ni polisi makini, hao wanaosema sema saa hizi mbona wangekuwa wanasemea pengine!.

Udhaifu huu wa polisi wetu ni good loophole kwa learned brothers and sisters wetu ku knock down PP kirahisi sana huko mahakamani ukijumlisha na majaji wetu hawa!. Wanaokwenda jela ni wale masikini ambao can't afford good lawyers. Ulipozuka ule ubishani kuhusu kesi ya kina Yona, Mramba na Mgonja, niliwaambia pale hakuna kesi, ni drama scene tuu wanatuletea!.

Hata sile za EPA za wenye fedha zao, mtaniambia!
 
We have to be very careful. Hapa tumesimama kumsemea Lulu ambaye yupo na anajua alichokifanya. Tunasahau kuna victim ambaye kwa sasa ni marehemu hana wa kumsemea. It can be fare before the eyes of the law but remember there is God who knows what exactly did happen. I tend to be neutral but remember watu wa karibu wametumika sana katika kutekeleza mauaji. Mimi na wewe tulimpnda sana Kanumba. Lakini kama yeye mwenyewe alivyoandika ktk blog yake wanadamu tuna wivu sana. Wewe unadhani hakuwa na rivals? Kwenye mafanikio yake au kwenye mahusiano? Kwa upande mwingine Lulu kwa umri wake na mambo yake haviendeani kabisa. Yaani huyu mtoto alishachakachuliwa kwenye hizo hizo shughuli zao za usanii. Umekomaa kabla hajakua. Kisaikologia huenda hayuko normal. Kwa hali hiyo hakuwa na kusudi la kuua hata kama alimgonga na kitu au alimsukuma. Baada ya hapo ndipo amechanganyikiwa zaidi kuona matokeo. possibility ya kufanya kwa kukusudia ipo kwa asilimia fulani ndogo, na uwezekano kuwa hakukusudia upo. Na inawezekana pia tena kwa marehemu alikuwa kanywa kama inavyodaiwa hivyo aka lose balance kirahisi akaangukia pabaya. Maadamu yote yanawezekana tusihukumu tusubiri sheria ifanye ichakachue mambo maana ndivyo inavyokuwa
 
Mkuu Pasco,
Kwanza thanks kwa hizi info ni useful kwa JF updates, ila ninakushangaa wewe kuwashangaa hao wasanii kupiga picha dead body, wakati wewe huna tofauti yeyote na hao kwa kitendo chako cha kupalamia makaburi ya watu kule Kilombero ili upate picha ya Dr Slaa na JK!
Kweli nimeamini Nyani halioni kundule!!....
Mkuu Matola, kosa langu ni kuwa very frank!, huwezi kuhudhuria maziko yoyote hapa mjini na ukajipenyeza mpaka makaburini bila kupita juu ya makaburi mengine!. Wana sio tuu wanakanyaga, infact ndio viti pekee kwa kina mama wengi ambao huwa hawawezi kusimama muda mrefu pale mazikoni. Kosa langu ni kusema nimepanda juu ya kaburi.
Ukweli umeisha wahi kunigharimu sana, na mpaka sasa bado napokea baadhi ya malipo hayo!.

Wakati Princes Diana anafariki nilikuwa UK as a young journalist, nami pia nilitamani nizione zile picha za wale paparatsi thinkingn itv was right, they are brave and they did their job well!. Wakati wa Rwandan Genocide tumeonyeshwa floating and dilapidated bodies kwenye CNN. Wakati wa September 11, jaribu kukumbuka uliweza kushuhudia any dead body zaidi ya zile black bags?, au kwenye Iraq war au Afghanistan, umeona miili yoyote ya hawa wenzetu?. Nakubali lazima tu set our own moral standard, mwili ni mwili, na kaburi ni kaburi!.
 
Biashara ya polisi imefanyika asubuhi!. By the time daktari wa K anafika pale, he was no more long ago alimkuta cold!, eti aliogopa kusema the game is over ili watu wasi panic. Tukio limeripotiwa polisi baada ya mwili kufikishwa Muhimbili na kukataliwa kupokelewa kwanza bila PF.3.

Hao polisi walifika nyumbani asubuhi ndio kukuta hiyo JD kwenye glass.

Kuikweli kwenye investigation, polisi wetu ni bure kabisa!, sio tuu wana uwezo duni, bali hata interest hawana!. Ingekuwa ni polisi makini, hao wanaosema sema saa hizi mbona wangekuwa wanasemea pengine!.

Udhaifu huu wa polisi wetu ni good loophole kwa learned brothers and sisters wetu ku knock down PP kirahisi sana huko mahakamani ukijumlisha na majaji wetu hawa!. Wanaokwenda jela ni wale masikini ambao can't afford good lawyers. Ulipozuka ule ubishani kuhusu kesi ya kina Yona, Mramba na Mgonja, niliwaambia pale hakuna kesi, ni drama scene tuu wanatuletea!.

Hata sile za EPA za wenye fedha zao, mtaniambia!
Unaona sasa!!! Hao ndo madaktari mnategemea eti watatibu watu mahtuti pai hata kuwa na PF3? Yaani badala ya kutoa taarifa polisi kwanza yeye akaona awafiche waliokuwepo....ridiculous

Aaah mi nina maswali mia mia hapa usije ukaona nakuhoji bure muhishimiwa Pasco.

Hawa polisi wetu nao ndo hivyo...hakuna chochote nadhani kilichokusanywa kusaidia hii kesi maana eneo husika lilitibuka long before manjagu kufika.

Ukijumlisha na factors nyingine za miunddombinu basi hapo kweli ni ngumu kuona haki ikitendeka...

Anyway enough with tiring my brain cells with specs...Kenyela kasema wanakusanya ushaidi kisha 'mtuhumiwa no moja' Lulu atafikishwa kwa pilato
 
kwa nini hatuonyeshi interest za kujua aliyemigia simu lulu, alimpigia kwa sababu za;
a)mapenzi
b) au ndo plan na lulu dhidi ya kanumba
 
Naungana na wewe matola. Yaani hali imeshaanza kuelekea huko. Huenda kuna mnene amaingizwa kwenye mfungo kwa Lulu kuwa cell. kuhusu umri inavyoonekana kuna mpango wa kuchakachua au ndo ushachakachuliwa tayari maana nchi hii kila kitu kinawezekana. Si alishasherehekea kutimiza 18 tena akahojiwa uhusu hilo? mtu anajaa kwenye macasino na kula kinjwaji, na kubeba wakubwa kwa hiari yake ana udogo tena? anajua atendalo.
 
kazi ipo! binafsi sina uhakika kama ukweli utatutosheleza!
 
Na usije kushangazwa kama weekend ijayo mtakutana naye Ngwasuma maana nchi kila kitu kina wezekani.......labda kama alikuwa mchoyo kwa Wazee wa System, lakini kama aliwahi kutoa tunda angalau kwa raia mmoja wa pale magogoni basi nakuhakikishia she is out without any charge

ni kweli hii nchi ina viroja
 
ah! kizunguzungu, ngoja niongeze chupa ya pili nikamuwai kwa ma'yoyo! but athought she z manslaughter! kulingana na mazingira yenyewe. Mr S. C. Kanumba (R.I.P) hakika umeacha mchango mkubwa kwa vjana, hajira na mioyo ya kimapinduzi, bongo movie inaheshima kutokana na mchango wake na ubunifu wa hali ya juu. (R .I .P) bro.
 
Biashara ya polisi imefanyika asubuhi!. By the time daktari wa K anafika pale, he was no more long ago alimkuta cold!, eti aliogopa kusema the game is over ili watu wasi panic. Tukio limeripotiwa polisi baada ya mwili kufikishwa Muhimbili na kukataliwa kupokelewa kwanza bila PF.3.

Hayo ndiyo matatizo ya kukosa emergency system(s) na watu kutojua wakati wa dharula wafanye nini.

Daktari wa marehemu akifika pale baada ya muda gani?

Na huyo daktari ana ujuzi wa huduma ya kwanza? Na alienda hapo na vifaa gani vya huduma ya kwanza?

Hivi hata hizo namba za dharula (112/111?) zina dispatchers wanaofanya kazi masaa 24 kweli?
 
dah, nashkuru sana Womanofsubstance,
nakubalia na ujumbe wako kwa asilimia 100% kwamba ni ngumu sana kumuita lulu muuaji kuendana na hayo mazingira na hata kama atakua kwa njia moja amehusika na kifo cha kanumba naamini si kwa makusudi bali ni katika jitihada za kujinusuru!!
siamini kwamba lulu alitoka huko kote usiku kwa nia ya kwenda kuua jamani.....
Nilimpenda sana kanumba na kazi zake ila Mungu amempenda zaidi
Nampenda sana lulu, pamoja na ukorofi alonao bado anahitaji kutendewa haki katika hili
Umenena kweli kijana hapa inahitajika hekima na uchunguzi wakina.
 
Hayo ndiyo matatizo ya kukosa emergency system(s) na watu kutojua wakati wa dharula wafanye nini.

Daktari wa marehemu akifika pale baada ya muda gani?

Na huyo daktari ana ujuzi wa huduma ya kwanza? Na alienda hapo na vifaa gani vya huduma ya kwanza?

Hivi hata hizo namba za dharula (112/111?) zina dispatchers wanaofanya kazi masaa 24 kweli?
[h=6]Nipo kwenye msiba wa kanumba inabidi uje na parachut maana hamna pa kupita... sare ni, kope za kubandika, les wigs, madira trasparent,funguo za gari hata za kabati njoo nazo tu..!![/h]
 
Ngabu unaongelea saa 24? Ungeongelea hata saa 12 bado ingekuwa tatizo...

Halafu daktari aligundua Kanumba kafa ilikuwaje akaacha mwili ubebwe tu upelekwe muhimbili ukizingatia mazingira ya kifo?
Unakumbuka suala la PF3 na madaktari kukataa kuhudumia wagonjwa wasionayo?
 
Back
Top Bottom