Ujinga mwingine nikudhani kila jambo unaweza kulitolea ufafanuzi

Ujinga mwingine nikudhani kila jambo unaweza kulitolea ufafanuzi

fact only

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2024
Posts
2,481
Reaction score
4,014
Hellow wana JF.

Hivi sasa kwenye jamii kunazidi kuibuka vijitabia vya mtu/watu kudhani kila jambo wanaweza kulizungumzia au kujadili hata kama hawana ujuzi wa jambo hilo(hata hapa JF kuna watu wanadhani wanaweza kuzungumzia kila jambo).

Hivyo vijitabia vichafu chafu vinapelekea watu kutukana tukana hovyo, kuenezwa kwa taarifa za uongo, kuharibu jamii, kuchelewesha maendeleo, kusambaza chuki, kuteketeza watu kiakili na kiroho, lakini pia tunazidi kuonekana kama taifa hili ni la watu wajinga wajinga kupindukia.

Kama jambo hauna maarifa nalo tulia ujifunze kwa wenye ujuzi nalo, punguzeni/acheni hivyo vitabia vichafu chafu vyakujifanya kila jambo mnalijua mnapoteza jamii.
 
Basi sawaa

5314BA4D-22E6-4C99-81AF-ABAFA2940ACB.jpeg
 
Kuna mambo yapo kwenhe uwezo wako na mengine hayapo kwenye uwezo wako ikkwemo kuzuia mtu asiongee kitu hili lipo nje ya uwezo wako you can not control it even if you are a president

Alishindwa jiwe mwenye nguvu wewe menzangu na mimi utaweza?
 
Mkuu inawezekana wewe haujaona maana.

Of course slogan inasema"where dare talk openly" haija sema "where dare talk lies openly"
kinachobaki kwa wewe msomaji nikuchambua ni kipi ni uongo na kipi ni cha kweli.
 
Kuna mambo yapo kwenhe uwezo wako na mengine hayapo kwenye uwezo wako.
Hicho ndicho nilikuwa namaanisha kama jambo halipo kwenye uwezo wako jaribu kupisha wenye uwezo wao waelimishe jamii.

Usisambaze uongo wako ni ustaarabu tu kwa mwenye akili.
 
hutaki tujadili habari ya manchester united kufungwa na chelsea au unamanisha cku 40 zakufiwa
 
kinachobaki kwa wewe msomaji nikuchambua ni kipi ni uongo na kipi ni cha kweli.
Mkuu naona na wewe hauelewi nini unazungumzia.

Unasema mtu achambue uongo wako? Anachambua Vipi wakati jambo hilo halijui kabisa anahitaji ukweli wa jambo na wewe unazungumza uongo. Unazani mtu huyo atachambua vipi?

Solution ni wewe kuacha kuongea uongo ili mtu asipate tabu kuchambua uongo wako kaa kimya kabisa na ujifunze kwa wanao jua jambo hilo ili kesho usieneze uongo wako.
 
Back
Top Bottom