toobiter
JF-Expert Member
- Dec 22, 2017
- 1,441
- 2,877
Kuna kiongozi Mmoja ndani ya Afrika mashariki aliwahi mwambia kiongozi wa Nchi yetu nyakati hizo kwamba anaongoza "maiti".
Ilikuwa lugha ya kuuzi,kukera,kudhalilisha na kushusha utu wetu.lakini ndani kabisa ya Ile kauli kulikuwa na ukweli ulio wazi. Watanzania tunadhani kuletewa maendeleo na viongizi kwa kujenga miundombinu kama shule,hospitali,maji,barabara na huduma nyingine ni kama "neema" na sio wajibu wa msingi kwa viongozi.Huu ndo "UJINGA" hasa.
Hivi ukiwanunulia watoto nguo,ukawapa chakula,ukawapeleka shule ,ukawapa mahali pa kulala ndo utataka familia ikuabudu?Jibu ni hapana maana huu ni wajibu wa msingi wa "ubaba"
Kadri ujinga unavyopungua Nchi hii na watu wakaanza kuhoji na kupata uelewa basi wanaonekana "wahalifu na waharibifu".Maiti nyingi zimeanza kufufuka na nyingine zimegoma kuzikwa zinauliza zilipoteza vipi uhai na kwa mazingira yapi? Hapa ndipo watawala wanapotaharuki.
UOGA.hakuna kitu kibaya kama uoga au kuwa na hofu.nilipata kusafiri na basi na pembeni yangu kulikuwa na abiria mwanamke.Baada ya mwendo wa saa nzima nilianza kusikia harufu ya mkojo na yule mama alipoteza ujasiri hata wa kunitazama usoni.kwa upole ikabidi nimuulize nini tatizo mama mpaka unafikia Hali hii?Jibu lake lilinishangaza sana,eti anaogopa kumwambia dereva asimamishe gari ili akapate huduma ya haja ndogo.Amelipa nauli,ni abiria kikanuni na konda na dereva ni watumishi wake kwa muda atakaokuwa kwenye gari ila bado anaona hofu kueleza shida yake.
Hawa ndio watanzania wengi.Ni waoga na katika uoga kumezaliwa ujinga.
Mwisho.Nyerere alipotangaza maadui watatu wa taifa:UJINGA,UMASIKINI na MARADHI bila shaka alisahau UOGA.