Naam! Remote
William Sami Grigahcine maarufu kama DJ Snake ni raia wa Ufaransa (France) mwenye asili kutoka Algeria.
DJ Snake ni DJ, Recording Producer (Mtayarishaji Muziki), mtaalamu wa upangaliaji nyimbo, mtunzi wa nyimbo pia mjasiriamali/mfanyabishara yaani entrepreneur.
DJ Snake ni moja kati ya watayarishaji muziki na DJ anayelipwa fedha nyingi kutokana na shows, uandishi, utayarishaji pia mikataba na mirabaha yaani endorsements na royalties kutoka kampuni kubwa na ndogo duniani kote inayomfanya kuwa katika nafasi 15 za juu.
DJ Snake anafahamika vizuri kwa kutoa/kuachia, kutayarisha, kuandika au kuchakata nyimbo za kukata na mundu, mfano wa nyimbo hizo ni;-
Taki Taki Ft. Ozuna muimbaji na muandishi kutoka Dominica Republic akiwa na sauti kutoka Nibiru. Selena Gomez mrembo mwenye mvuto mithili ya taifa la Namibia na mdada machachali Cardi B mweye flows za kuvunja chaga.
Fuego Ft. Sean Paul wenyewe wanamuita King wa Dancehall. Anitta mdada flani wa KiBrazil mwenye figure matata ya kilatin na Tainy mtayarishaji wa muziki mwenye ubora kama?! Baba lao.
Loco Contigo Ft. J Balvin sema Babvi'meen huyu ni Prince wa Reggaeton nyuma ya King Daddy Yankee pia Tyga akiwa katika wimbo huu.
DJ Snake amefanya kazi na Record Labels tofauti ikiwemo Spinnin, Sony, WEPLAY Group chini ya "Weplay Music na TONSPIEL", Columbia na Interscope kwa uchache.
DJ Snake ni mmoja kati ya wamiliki (Joint Ventures) na brand identity ya PARDON MY FRENCH.
Huyu anatambulika vyema kwa miondoko ya Dance/Electronic, Deep House (EDM). Huyu ndiye DJ Snake.