Ujio wa kocha mpya Simba SC hauna tofauti na kupika mchele wenye chuya

Ujio wa kocha mpya Simba SC hauna tofauti na kupika mchele wenye chuya

Alifukuzwa kutuliza hali ya hewa Wala hakuwa na kosa lolote....

Hata huyu naye atafukuzwa kutuliza hali ya hewa na kuendelea kudanganya mashabiki maandazi na kahawa kuwa kocha ndo tatizo kama kawaida yetu, wakati tulitakiwa tijifunze kitu tokea msimu wa 2021/22
NAKAZIA
 
Alifukuzwa kutuliza hali ya hewa Wala hakuwa na kosa lolote....

Hata huyu naye atafukuzwa kutuliza hali ya hewa na kuendelea kudanganya mashabiki maandazi na kahawa kuwa kocha ndo tatizo kama kawaida yetu, wakati tulitakiwa tijifunze kitu tokea msimu wa 2021/22
ZA NDANI KABISA MWAMBA KAAMUA KUSEPA BAADA YA KUONA KUNA MAGUMASHI NA USWAHILI NDANI YA KLABU YA SIMBA SC
 
NALIA NGWENA sitorudi nyuma kuandika ukweli japokua ni jipu chungu kwenye mioyo ya wanasimba.

Ukweli mtupu huu Kama utafanyiwa kazi Basi utaleta furaha na kukata kiu ya mtu alietoka jangwani baada ya kupigwa jua Kali.

Mpaka Sasa Simba sc kwa misimu miwili hii Ina makombe mawili tu kabatini yaani kombe la MAPINDUZI na NGAO YA JAMII na ukipiga tathimin hayo makombe siyo lolote siyo chochote.

Simba sc imeleta kocha mpya (BENCHKHA) lakini swali la kujiuliza je Simba sc wanabadili makocha je wao pia Wanaweza kusajili wachezaji wenye hadhi Kama makocha wanavyotaka?

Jibu hapana! Ukiangalia kuletwa kwa kocha Robertinho hakuna wachezaji wazuri walioletwa ili kwenda na Falsafa za kocha Robertinho Ila tu kilichofanyika ni ujanja ujanja na kununua wachezaji wa mafungu (Bei Chee).

Kwani Nani aliyemleta sawadogo, Nelson Okwa na wachezaji wengine walioonekana kabisa hawana hadhi ya kucheza Simba sc?

Hapo tunapata picha kuwa Kocha anapendekeza mchezaji huyu lakini viongozi (wazee wa ten percent) wanaleta wachezaji wanao wataka wao.

Ameletwa kocha mpya BENCHKHA kwa takwimu ni kocha mzuri lakini ukija kwenye timu aliyopewa hakuna wachezaji wazuri na timu ikifanya vibaya lazima atafukuzwa tu na atatafutwa kocha mwengine.

NALIA NGWENA nafungua ubongo wa msomaji kuwa mchele ni ngumu kupikwa na chuya Ina maana ujio wa kocha mpya akikabidhiwa timu yenye wachezaji Kama Saidoo ntibazonkiza, John Bocco, Chama n.k Basi itakua ni kazi ya kutwanga maji kwenye kinu.

Maoni Yangu: Simba sc isipoondoa wazee katika kikosi hata aje Morinho au Gadiola nao watafukwa tu baada ya mechi tatu.View attachment 2825495
Ulitabiri mkuu ....kumbe ni kweli
 
Back
Top Bottom