UONGOZI wa Simba unachapia nyufa badala ya KUJENGA ukuta, na hakika safari hii NYUMBA yenyewe imegoma na mafuriko ni mazito kiasi kwamba wakiendelea kukaza SHINGO basi tujiandae na mfuatano wa majanga...
Kufanikiwa kunahitaji kijikana kwakweli, hili linalotokea leo lilikuwa lazima lifike kwasababu klabu zetu zipo kwa ajili ya leo... Simba iko na uwanja Bunju miaka 10 inaenda lakini mpaka muda hakuna hata mtoto mmoja anayetokea pembeni ya uwanja hata wa kujua kudaka na tunaoyeshana Ndoto za mafanikio Afrika...
Haya kutengeneza cha kwetu tumeshindwa, sasa huko kununua nako tunabebana na sagula sagula za mwisho maana hata mtumba nao una grade zake, halafu tukishakusanyana na hayo magalasa tunayapamba kwenye magazeti ili kuhalalisha udhalimu wetu, halafu bila aibu TAJIRI tunamdanganya kuwa tumetumia Bilioni 3 kusajili [emoji1787][emoji1787][emoji1787], lakini ukichukua kalkuleta na peni Kila ukipiga hesabu huziona hizo Bil 3 zimeishia kwa nani?? [emoji23][emoji23][emoji23] Hapo MHINDI tushampiga kwa kumuuzia JUMBA LA UDONGO LILOCHAPWA PLASTA ambalo soon litavimba tu...
Na Sasa ndo limeanza kuvimba [emoji1787][emoji1787][emoji1787] maana wakati tunamwongezea MHINDI sifuri kwenye hesabu tunasahau kuwa mwisho wa siku yooote yanaishia uwanjani,,,, hapo ndo tunabaki na mazoea kuwa kwa "MKAPA HATOKI MTU" [emoji23][emoji23][emoji23].... huku chini ya VITI tunacheka tu [emoji23][emoji23][emoji23] tunasubiria dirisha dogo....