jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 36,197
- 29,717
Tunafurahi kwa diplomasia nzuri ya kufungua nchi kwa dunia. Jitihada kubwa inayofanywa na mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kurejesha mahusiano na mataifa mbalimbali hususani ya Magharibi sio ya kubezwa ...ni jitihada kubwa na leadership style ya kipekee ambayo inaleta manufaa.
Tumewahi kupata ugeni mbalimbali kutoka mataifa makubwa lakini napenda kurejea ugeni wa Rais wa Marekani Barack Obama ambapo "inasemekana" kuwa masuala ya kiulinzi yaliingilia mifumo yetu ya kiulinzi pengine kwa kutoaminiwa sana kwa wataalamu wetu wa maswala ya ulinzi na usalama.
Iwapo suala hilo ni kweli basi hatuna namna bali kutoa angalizo...kwamba vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ni imara na ni lazima viaminiwe kwa asilimia 100.Tusidanganywe kuwa hatuwezi bali discussion ifanyike kujua weak points ni zipi na hivyo zifanyiwe kazi.
Tunayo Ikulu mpya ya CHAMWINO Kamwe tusiruhusu mtoka mbali ndio ajidai kuwa ana uelewa wa kuilinda kuliko vyombo vyetu adhimu vya ulinzi na usalama.
Kamwe tusiruhusu details za Ikulu yetu mpya kuangukia mikononi mwa wageni, hili ni hatari sana na ni sawa na kuingilia uhuru na heshima ya nchi.
Otherwise karibu sana mgeni wetu na tuna value ujio wako.
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!