Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,925
United in remembrance: The two presidents bowed their heads as a Marine placed the wreath of red,
white and blue flowers in front of the large stone memorial to the Tanzanian victims of the
simultaneous attacks at the U.S. embassies here and in Kenya masterminded by Osama bin Laden
Mara kadhaa tumetembelewa na Viongozi wa juu wa Taifa la Marekani, lakini hatujapata kuona mfumo wa ulinzi na usalama wa viongozi hao kuwa wa pekee na kufikia kutoaminika kwa vyombo vya usalama nchini. Mara zote ulinzi ulikuwa shirikishi tofauti na ulinzi wa Obama ambapo hata tu viongozi wa juu serikalini kama mawaziri kuambiwa watachujwa watakaokaribia na kusalimiana na Obama. Nini nyuma ya pazia kwa vigezo vipya kwa ulinzi na usalama wa viongozi wa Marekani kuwepo nchini kipindi hiki tofauti na miaka ya nyuma? Wingi wa baraza la mawaziri nchini umechangia kuchujwa?
Vyombo vya usalama vya Marekani kupokonya majukumu ya vyombo vya usalama vya Tanzania
Ilielezwa kwamba vyombo vya usalama kutoka marekani vilipokonya jukumu la ulinzi wa viongozi wa msafara wa Rais Obama na delegates wake hapa nchini na kuonyesha kila dalili ya kutoamini vyombo vya usalama vya nchi mwenyeji Tanzania. Pamoja na Rais Obama kuanzia ratiba ya huko West Afrika na kisha South Afrika jambo la vyombo vya usalama vya huko kupokonywa haki za kukendesha usalama hazikusikika kama ilivyotokea hapa.
Mapokezi ya viongozi wa awali wa Marekani kutembelea hapa nchini hapakuwa na hali iliyojitokeza safari hii kwani kulikuwepo ushirikiano zaidi na kuaminiana zaidi. Jambo kubwa na la msingi serikali kulitathmini kwa nini imetokea hivyo leo tofauti na siku za nyuma. Rais Obama anapokeleka zaidi ulimwenguni kuliko ilivyokuwa Rais wa zamani wa marekani George Bush, lakini kwa nini itokee hivyo kwa Obama tena Mwafrika mwenzetu?
Mchujo wa viongozi wa Serikali kumpokea na kumwaga Obama
Habari ambazo hazikufichwa kwenye mafaili maofisini juu ya jopo la viongozi wa kumpokea Obama uwanjani ni kwamba vyombo vya usalama vya Marekani kuiwekea ngumu Serikali katika orodha ya viongozi wa kujumuika kumpokea Obama. Mbali zaidi kwamba orodha ya viongozi watakaojumuika kumpokea itatolewa na Wamarekani wenyewe na kwamba hata mawaziri so wote watakaobahatika kumshika Mkono Obama atakapotua uwanjani. Kiwango hicho si cha kawaida, pengine Wamarekani kuwa na hisia mbaya kwa baadhi ya viongozi waandamizi serikalini na hivyo kuwawekea ngumu?
Utekelezaji wa mpango huko unaonekana kufana kutokana na baadhi ya viongozi waandamizi serikalini waliozoeleka kuwa karibu na Mkulu latika mtukio kama haya kutoonekana, sina maana waliwekwa kando na vyombo vya usalama Marekani, labda waliamua kuondokana na udhia huo. Hata katika safu ya utambulisho wa viongozi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Makamu wa Kwanza wa Rais hakujumuishwa, labda tu ratiba ziliingiliana kwa tafsiri nyepesi.
Mood ya uwajibikajia vyombo vya usalama Marekani tofauti na vya hapa nchini vinavyokandamiza raia
Tukio ambalo limeanikwa hadharani na chombo kimojawapo cha habari nchini juu la purukushani iliyotoka Makumbusho kwa Mwanausalama mzawa kumdhalilisha mwandishi wa Gazeti la Uhuru, na kisha dada huko mwandishi kuokolewa na Mwanausalama wa Marekani kwa kumtetea na kulinda haki zake za msingi kama binadamu na mwandishi akiwa kazini ni jambo ambali limezidi kuvichafua vyombo vya usalama nchini katika kile kilichozoeleka juu ya udhalilishaji.
Mbaya zaidi lugha aliyotoa yule Mwanausalama wa Marekani kwa mwanausalama mzawa kwamba: "Hivi ndivyo mnavyofundishwa katika uwajibikaji kazini," ni aibu kubwa kiasi kwamba mwanausalama wa Marekani uvumilivu ulimshinda na kuamua kumwambia wazi na kumruhusu dada aendelee na shughuli iliyomfikisha pale Makumbusho.
Vyombo vya kimataifa vinanyoshea kidole CCM na Serikali na kuisafisha CHADEMA
Uwepo wa Rais Obama nchini kwa vile anatoka Taifa kubwa duniani, vyombo mbalimbali vya habari vikubwa duniani vilikuwepo nchini. Kama ilivyo ada vyombo hivyo havifutatilii ziara hiyo tu, ila pia kuisoma nchi yetu kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni nk.
Pamoja na vyombo hivyo kuisifia Tanzania katika makaribisho ya Rais Obama yasiyo ya kawaida na kuzidi sehemu nyingine alizotembelea hapa Afrika, vyombo hivyo vya habari havikuchelea kusoma hali ya kisiasa nchini na matukio ya uvunjaji wa amani ikiwa ni pamoja na matukio ya mabomu Arusha kwenye kanisa na mkutano wa Chadema. Vyombo hivyo tofauti na mtazamo wa serikali ya Tanzania pamoja na CCM inavyoitazama Chadema na vyama vingine vya upinzania, vimeonyesha dalili ya kwamba vyama vya upinzani vinakandamizwa. Vyombo hivyo vimegusia kuhusu kufungiwa Gazeti la Mwanahalisi, Kuuawa Mwangosi, Kutekwa na kuteswa Mwenyekiti wa madaktari nchini na Mwandishi wa Habari Kibanda.
Magazeti mbalimbali ya Marekani New York Time, Washington Post, USA Today, na mengineyo, Magazeti ya UK, vyombo vya habari vingine kama CNN, BBC, FOX, Yahoo, Microsoft, ABC, Nk vimeonyesha jinsi demokrasia inavyokandamizwa nchini kwa njia mbalimbali na kuonyesha dalili ya serikali ya Tanzania kuifanyia kazi ili kulinda amani ya nchi.
Obama receives a pass from Tanzanias President Jakaya Kikwete during the demonstration at the Ubungo Power Plant
Marekani imeacha ujumbe serikali inatakiwa kufunguka kuuelewa ujumbe huo
Nchi zilizoendelea huwa hazitoi jumbe zao kama kufundisha chekechea, hutumia mfumo wa kifalsafa zaidi iwe kimatendo, maoni ya vyombo vya habari na hotum\ba za viongozi wao.
Rais Obama
Pamoja na kutumia sana diplomatic language, amesema wazi maendeleo Afrika yataletwa na Waafrika wenyewe si na wageni. Ujumbe huo ni mzito ingawa tunaujadili mara kwa mara. Pengine misafara ya viongozi wetu kuzungukia dunia kila kukicha kusingepewa uhimu zaidi, bora kutulia nchini na kuwa karibu zaidi na wananchi ili kujadiliana namna bora ya kuleta maendeleo kwa kutumia zaidi tulicho nacho kuliko pesa tunayopata toka nje wakati tunapoenda kuitafuta tunatumia gharama kubwa kuliko pesa tunayopata.
Vyombo vya kumataifa kuanika madudu ya hapa nchini
Muhimu serikali ikatafakari juu ya kinachoendelea nchini hasa amani na utulivu ambao unaelekea ukingoni. Matumizi ya nguvu kutoka vyombo vya usalama, kauli tata za viongozi ni moja na viashiria vya kuchochea vurugu kama:
[*=2]Rais Kikwete Mkutano Mkuu Dodoma - Nitahakikisha na kufanya kila niwezalo nakabidhi kiti cha urais kwa CCM
[*=2]Waziri Mkuu Pinda Bungeni - Tumeagiza vyombo vya usalama viwapige wananchi tumechoka kuvumilia
[*=2]Tamko kwa Tanzania Daima Jeshi la Wananchi - Tumeagizwa na serikali kuwachapa wananchi kulinda amani
Serikali itafakari kurejesha amani kidipolomasia badala ya matumizi ya nguvu
Serikali itafakari kwa nini inapofanyika mikutano ya vyama vya upinzani nchini bila uwepo wa jeshi la polisi hapajatokea mtafaruku wa uvunjaji amani. Hali kadhalika kuna ugumu gani kukaa na wananchi kuwasilikiza wanachokitaka kama suala ya gas ya Mtwara, maana hawa wananchi ndio wenye serikali, hawa viongozi wanapita, na ipo siku wananchi watatumia haki zao kuwatosa kwa vile hawawasikilizi.
Kikwete amemshauri Rais Wa Rwanda Kagame akae chini pamoja na wapinzani na kujadiliana ili kurejesha amani nchini humo, jambo hilo analiona zaidi Rwanda lakini hapa nchini haoni sababu ya kufanya hivyo ila kutuma vyombo vya usalama kuwapiga wananchi anakubaliana nalo?
Ziara ya Obama kupokonya usalama ni kutoaminika vyombo vya usalama nchini?
Vyombo vya habari nchini Marekani licha ya kutoonyesha moja kwa moja chanzo cha vurugu nchini na kutonyoshea kidole vyama vya upinzani bali kuonyesha kuna kitu kisichokuwa sawa ndani ya mfumo wa vyombo vya usalama nchini, dalili ya kupokonywa haki za kulinda ziara ya Obama huenda inatokana na kile kinachoendelea vyombo vya dola kukandamiza wananchi na pengine kusababisha mtafaruku wa amani. Milipuko ya mabomu yakutupwa kwa mkono Arusha pamoja na kuacha maswali mengi yasiyojibika kwa uwazi kutoka vyombo vya usalama nchini ni dalili tosha kutoaminika 100%.