Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,925
- Thread starter
- #41
Candid Scope, AshaDii Mwita Maranya na wengine,
Nafikiri mtakuwa mnafanya kosa sana kufikiri Secrety Service ya USA wametunyanyasa.
Wao kwa sasa na hasa Obama kama Rais, hawawezi kuruhusu likafanyika kosa na Obama akashambuliwa na kudhurika au kuuawa. Imeshawahi kutokea huko nyuma na hawawezi kuruhusu kitu kama hicho. Sababu kadhaa zinazosababisha hiyo hali ni kama hizi:
1. Obama hadi leo hapendwi kabisa na watu kama Donald Trump na hadi alishafikia kusema wazi ingawa alifanya kama utani kuwa "watu kama Trump walikuwa wanaombea akienda msitu wa Amazon basi apotelee huko Milele...."
Ukiacha hao, kuna wale wa WHITE POWER, KKK nk ambao walishajitangazia zamani na kujiapiza kuwa OBAMA lazima afe. Kundi hili halipo tu USA ila hadi Ulaya ambako makundi haya ya WHITE POWER, SKIN HEAD walishajitangazia na wao kama wakipata nafasi basi ni lazima Obama afe. Wengi walilaani sana mara tu ilipomshinda H. Clinton na wakaanza kuona kuwa Mjaluo anaweza kushinda. Wakasema wazi kabisa ndiyo itakuwa mwisho wa WHITE RACE.
2. Kifo cha Osama bin Laden, wafuasi wake hadi leo hawajafurahia kabisa na wanamuwinda usiku na mchana.
3. Israel hawakufurahia kushinda kwake na hasa Bibi Netanyahu ambaye aliweka vita ya wazi kabisa na Obama wakati wa kampeni na kwa bahati mbaya akashindwa. Netenyahu na hao Orthodox wenzake hawajafurahi kushinda kwake hadi leo.
4. Makundi yote ya kigaidi ambayo yamepoteza viongozi wao kwa kuuawa na Drone za USA, wanamuwinda kwa nguvu. Hapo ukiongeza na wale wa Mali na waliopigwa Libya pamoja na Ghadaffi.
Unaweza kuongeza sababu nyingi tu na utagundua kuwa Obama ni zaidi ya maadui wa J F Kennedy ambao mwisho waliweza kumuuwa. Na Usalama wa Taifa, FBI, CIA nk wanalijua hilo na hawawezi kufanya makosa.
Kuna jamaa yangu mmoja aliniambia kuwa Obama alipotembelea nchi yao huko Ulaya, basi barabara nzima ilifungwa na watu wakaondolewa siku hiyo mjini City Centre. Kwa sababu anakaa karibu na barabara inayotoka/kwenda Airport, alishangaa kuwaona Wababa na bunduki zao (Snipers) wakiwa juu ya majengo wamevalia nguo nyeusi na msafara ulivyopita, wakashuka. Pia huko Ulaya pamoja na kuwa na ulinzi wa hali ya juu sana, bado USA ilileta Walinzi 300 miezi mitatu kabla na wiki moja kabla wakaja wengine 300 na idadi kuwa hiyo ya 600 kama walivyokuja Tanzania.
Tuacheni Complex ya kudhani USA wanatudharau. Sababu kubwa ni MAADUI wa Obama na si hatuna ulinzi. Hata akienda UK au Israel, ni haohao 600 wanakwenda na mji siku hiyo unaingia kwa kibali maalumu na wanasema pia hivyohivyo na wazi kabisa kuwa kama unaweza basi safiri nje ya Mji. Na jamaa yangu anasema kweli mji ulikuwa umepungua sana watu siku hiyo.
Nakubaliana na hoja zako zenye kuakisi ukweli kutokana na dondoo ulivyozifafanua. Jambo ambalo limepitiliza mbali ya mazuri mengi uliyoyaainisha hapa ni ule mchujo wa viongozi waandamizi serikalini, maana yake hata hawa viongozi wetu wachaguliwa kuna ambao wanatiliwa shaka na usalama wa Wamarekani. Sishangai wao kuchukua jukumu la usalama wa kiongozi wao kwa 99%, lakini mchujo wa viogozi waandamizi serikalini wakiwemo mawazi hata baadhi ya makamu wa marais wetu ni jambo linaloshtua kidogo maana si la kawaida.