Ujio wa Obama: Kashfa ya kupokwa ulinzi, vyombo vya habari vinavyoiona Tanzania

Ujio wa Obama: Kashfa ya kupokwa ulinzi, vyombo vya habari vinavyoiona Tanzania

"Muda umefika sasa wa kuweka hayo pembeni na kutafakari Ujio wa Rais ambaye anakuwa Considered wa dunia kaja hapa Tanzania. What do we expect? Kikwete anatuambia nini? Wamekubaliana nini? Sisi Watanzania tunanufaika vipi? Na kulia na kutafakari ile Conference Ikulu was it what it seems to be?"

Usirudie makosa unayotukataza!! hebu tudadavulie hayo unayotuhubiri tufanye kwenye quote hapo juu!?
 
Mkuu suala si kutetea... Suala ni kutambua nini wakati wake wa kujadili. Tupo hali mbaya ki nchi kuanza ku entertain masuala ambayo yanaweza kuwa na tija but si Msingi. Suala ni kuwa Wazalendo na kupunguza Ushabiki kwa vitu ambavyo vinatuathiri kama Watanzania bila kujalisha kuwa unashikilia Itikadi zipi na wala bila kujalisha chamba unachotoka! Tanzania kwanza, CHADEMA, CCM na Vyama vingine baadae!

Ukija suala la mifano ya Viongozi ambao wamewahi kuja nchini Ikiwemo Bush, Clinton na hata Bibi Clinton (Kama US Secretary of State). Hawa woote walikuja kabla ya event ya September 11. Baada ya terror hiyo iliyoshutua dunia na kuitikisa US Security imekuwa tight zaidi. Obama/US ina maadui zaidi (hiyo ni sababu ndani ya sababu za msingi), Technology na Science imekua na haichagui kuwa unaitumia kwa niya njema ama wewe ni gaidi.

Sasa hapo yapaswa kujiuliza.... Kunani? Clinton, Bush, na sasa Obana (tena na Bush) wamekuja katika hii nchi. We have to stop underestimating the power of our nation! [On top of Xi Jimping rais wa nchi ambayo inakuwa kwa kasi na ni tishio kwa US alikuja hapa] tha Kuna maswali ya msingi yanahitaji majibu na majibu so far mimi toka nimeanza kusoma articles hakuna yanayo ridhisha...

So inabaki kuwa tuanze kuhoji masuala ya Msingi ambayo yatakuwa na manufaa sisi kama Watanzania an Tanzania.

Naomba uangalie Diary yako kama hawa walikuja kabla au baada ya Sept 11.
 
Mkuu suala si kutetea... Suala ni kutambua nini wakati wake wa kujadili. Tupo hali mbaya ki nchi kuanza ku entertain masuala ambayo yanaweza kuwa na tija but si Msingi. Suala ni kuwa Wazalendo na kupunguza Ushabiki kwa vitu ambavyo vinatuathiri kama Watanzania bila kujalisha kuwa unashikilia Itikadi zipi na wala bila kujalisha chamba unachotoka! Tanzania kwanza, CHADEMA, CCM na Vyama vingine baadae!

Ukija suala la mifano ya Viongozi ambao wamewahi kuja nchini Ikiwemo Bush, Clinton na hata Bibi Clinton (Kama US Secretary of State). Hawa woote walikuja kabla ya event ya September 11. Baada ya terror hiyo iliyoshutua dunia na kuitikisa US Security imekuwa tight zaidi. Obama/US ina maadui zaidi (hiyo ni sababu ndani ya sababu za msingi), Technology na Science imekua na haichagui kuwa unaitumia kwa niya njema ama wewe ni gaidi.

Sasa hapo yapaswa kujiuliza.... Kunani? Clinton, Bush, na sasa Obana (tena na Bush) wamekuja katika hii nchi. We have to stop underestimating the power of our nation! [On top of Xi Jimping rais wa nchi ambayo inakuwa kwa kasi na ni tishio kwa US alikuja hapa] tha Kuna maswali ya msingi yanahitaji majibu na majibu so far mimi toka nimeanza kusoma articles hakuna yanayo ridhisha...

So inabaki kuwa tuanze kuhoji masuala ya Msingi ambayo yatakuwa na manufaa sisi kama Watanzania an Tanzania.

AshaDii
Jaribu kurudi katika diary yako (au maktaba yako) ili ukumbuke kuwa Bush ametembelea Tanzania mwaka 2008, miaka mingi tu baada ya milipuko ya September Eleven. Aliyekuja Tanzania kabla ya milipuko hiyo ni Raisi Bill Clinton aliyekuja Tanzania mwaka 1998.
 
Last edited by a moderator:
Ziara ya Obama kupokonya usalama ni kutoaminika vyombo vya usalama nchini?
Vyombo vya habari nchini Marekani licha ya kutoonyesha moja kwa moja chanzo cha vurugu nchini na kutonyoshea kidole vyama vya upinzani bali kuonyesha kuna kitu kisichokuwa sawa ndani ya mfumo wa vyombo vya usalama nchini, dalili ya kupokonywa haki za kulinda ziara ya Obama huenda inatokana na kile kinachoendelea vyombo vya dola kukandamiza wananchi na pengine kusababisha mtafaruku wa amani. Milipuko ya mabomu yakutupwa kwa mkono Arusha pamoja na kuacha maswali mengi yasiyojibika kwa uwazi kutoka vyombo vya usalama nchini ni dalili tosha kutoaminika 100%.
[/COLOR]
Wanaijua vema siasa ya hatari inayochezwa na CCM hapa nchini kwa kutumia vyomba vya "ulinzi na usalama".
 
Tatizo kubwa liko kwa serikali yenyewe kupitia Wizara ya Mambo ya Nje kwa kushindwa 'kuiuza' sawasawa ziara hii kwa wananchi kwa minajili ya manufaa ya msingi (kiuchumi ? ). Hii ikasababisha 'media' kuibeba ziara hii katika 'celebrity agenda' kwani hawakuwa na taarifa nyingine za msingi. Upungufu huu wa Wizara unaweza kuwa ulisababishwa na usiri ulioambatana na baadhi ya ajenda za ugeni huu. Kwa hiyo ugeni umekuja,umeondoka lakini faida hasa ('topline and bottomline') bado hazijafahamika sawasawa .Kuhusu suala la ulinzi imebidi wa 'overdo' kwani ikiwa (inavyoonekana kwao) vyombo vyetu vyote vya usalama vimeshindwa kubaini waliosababisha bomu la kanisani na katika mkutano wa kampeni kule Arusha, je wataweza kubaini njama ambazo ni za hali ya juu zaidi? Wakati mwingine kutoaminika tunajitengenezea wenyewe..
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Kwahiyo IGP Saidi Mwema alikuwa anakula dinner na nani siku hiyo? akili mnazo lakini saa nyingine sijui mnazitumiaje...
Huyo ni Mwalimu by Profesional kwahiyo asikushangaze, nadhani unajuwa sifa ya kujiunga na Ualimu.
 
Kweli Watanzania tunahitaji kujiangalia upya kama watanzania wazalendo, mm nimefuatilia kwa karibu coverage ya vyombo vyetu vya habari tangu kuwasili kwa Obama mpaka anaondoka kwa kweli hakuna kipya kilichoripotiwa kwa minajili ya kumfanya Mwananchi kuelewa nini hasa kimezungumzwa na viongozi hao (maudhui ya ziara ya Obama) sanasana nimeishia kuelimishwa watu wengi wamejitokeza kumpokea Obama, mara eti kiingereza,mara Watanzania watumie fursa ya ziara ya obama,mke was Obama ameeleza yeye ni alikuwa maskini na upuuzi mwingine mwingi tu. Hakuna wakati ambapo nimepata kuudhika na utendaji wa vyombo vya Habari kama hizi siku mbili.WATANZANIA TUBADILIKE TUACHE UZUZU TUJADILI MAUDHUI YA SAFARI SIO SUTI WALIZOVAA, CHAKULA WALICHOKULA N.K vYOMBO VYETU VYA HABARI NA WAANDISHI WAHABARI MJISAHIHISHE NAMNA YA KURIPOTI HABARI ZENU ACHENI USHABIKI.
Kuna ombwe kubwa sana katika tasnia ya uandishi wa habari hapa Tanzania mkuu...vumilia tu!Mimi sijashika gazeti la Tanzania hata moja baada ya hii ziara kwa sababu najua media yetu will just scratch the surface tu.Nalingoja "The East African" Jumamosi nadhani nitapata habari na uchambuzi wa kueleweka
 
kwani Candid Scope unataka kusema ni lazima watu wote ambao ni viongozi kwenda kumwona Obama?? kumbuka kwamba wakati obama yupo pia viongozi wengine wa nchi za nje walikuwepo na walihitaj mwenyeji. mfano kulikuwa na GLOBAL 2013 SMART PARTNERSHIP na watu kama Mfalme Mswati, waziri mkuu wa Malysia, vice president wa Botswana etc sasa je unafikiri hawa hawakutakiwa kuwa na company?? nijuavyo kwa wakubwa kama hawa hata dinner hupangiwa watu wa kula nao so to me nafikri kutokuwepo kwa baadhi ya viongozi sishangai.

Nakupa mfano mdogo tu Chissano siku anakuja Obama alikuwa na Dinner na baadhi ya watu katika hotel aliyofikia na najua baadhi ya watu ambao walidine naye so usishangae sana juu ya hili.

Nisingefikiria uwopo wa wingi wa wageni nchini kipindi ni kigezo cha utetezi wakati Marekani iliweka utaratibu wa kuchuja nani wa kukutana na Obama. Kama kusingekuwa na tatizo hilo ambalo Marekani iliona tusingeambiwa kuwa Marekani imeweka utaratibi wa mchujo nani wa kumpokea na kusalimiana na Obama na wengine ambao hawataonekana pale maana yeke wamechujwa.

Vinginevyo utaratibu wa kugawana majukumu ya wageni mbalimbali yangebaki na sisi wenyewe wazawa vinginevyo naona utetezi wako
gfsonwin hauna uzito stahiki.
 
"Muda umefika sasa wa kuweka hayo pembeni na kutafakari Ujio wa Rais ambaye anakuwa Considered wa dunia kaja hapa Tanzania. What do we expect? Kikwete anatuambia nini? Wamekubaliana nini? Sisi Watanzania tunanufaika vipi? Na kulia na kutafakari ile Conference Ikulu was it what it seems to be?"

Usirudie makosa unayotukataza!! hebu tudadavulie hayo unayotuhubiri tufanye kwenye quote hapo juu!?

Pamoja na kuangalia yaliyojilia ujio wa Obama, binafsi nimeshangazwa na suala la Richmond iliyorithishwa Dowans hatua kwa hatua hadi leo tuna SYMBION ambayo kimantiki ni kitu kile kile kilichobatizwa kisiasa kwa ujio wa Obama kama msaada wa Taifa la Marekani kuimarisha suala la umeme nchini. Kesho sitashangaa kuona mambo kama ilivyokuwa juzi, bora Wachina pamoja na mambo yao watafanya kitu kile cha kutukumbusha kwamba walikuwa nasi.

Soma makala haya toka Tanzania daima:

Obama azindua mitambo tata

RAIS wa Marekani, Barack Obama jana alizindua mitambo ya kufua umeme ambayo ilizua mtafaruku mkubwa na kusababisha mtikisiko mkubwa serikalini na bungeni. Mitambo aliyozindua Rais Obama ni ile iliyodaiwa kuwa mibovu na isiyofaa, mali ya Kampuni ya Dowans iliyorithi mkataba tete kutoka kampuni iliyozua sakata zito lililosababisha kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

Dowans Tanzania Limited ilirithi mkataba tata wa kampuni ya kufua umeme wa dharura ambao kampuni ‘hewa' ya Richmond Development Corporation iliingia na TANESCO Juni 23, mwaka 2006, kufua umeme wa dharura wa megawati 100 kwa kutumia gesi asilia.
Hata hivyo, Richmond ilishindwa kuleta mitambo hiyo, na ikaonekana baada ya uchunguzi wa Kamati ya Bunge iliyoundwa Novemba 2008 kuwa haikuwa imesajiliwa huko Marekani kama kampuni inayofua umeme.


Lowassa alilazimika kujiuzulu pamoja na mawaziri wawili, Nazir Karamagi na Ibrahim Msabaha kutokana na kashifa hiyo, kabla ya kampuni ya Dowans kuuziwa mkataba wa kufua umeme na Richmond katika hatua nyingine iliyozua sintofahamu serikalini.
Utata huo uliongezeka zaidi baada ya kubainika kuwa hadi Kampuni ya Richmond Development, ikijitoa na kuirithisha mkataba wake Dowans, kinyume cha maelezo yaliyowahi kutolewa bungeni na baadhi ya viongozi wakuu wa serikali, kwamba haikuwahi kupewa fedha za serikali, kampuni hiyo ilikuwa imechotewa zaidi ya sh bil. 30 (Dola 30,696,598 za Marekani). Kiasi hicho ni sawa na asilimia 35 ya gharama ya kodi ambayo msingi wake ulikuwa kufanikisha mchakato wa ufunguaji wa hati ya muamana (letter of credit) kati ya kampuni hiyo na Benki ya Biashara. Malipo hayo ya asilimia 35 ni utekelezaji wa makubalino yaliyofikiwa awali, kati ya serikali na wawakilishi wa Richmond Development.


Baada ya kupewa kitita hicho cha zaidi ya sh bil. 30, Richmond ilipewa masharti ya kurejesha fedha hizo serikalini katika malipo ambayo yangefanyika kwa dola 1,279,044 za Marekani (zaidi ya sh bil. 1.3) kila mwezi, lakini katika awamu tatu.
Malipo ya awali yalipaswa kuanza kufanyika Novemba 2007. Hata hivyo, kutokana na utata wa Richmond, hasa kwa upande wa uwezo wake kiteknolojia na utendaji, kampuni hiyo iliuza shughuli zake kwa Dowans.

Imebainika kuwa wakati mchakato wa uuzaji wa shughuli za kampuni hiyo kwa Dowans unafanyika, Richmond ilikuwa haijarejesha fedha ilizopewa na serikali na kwa kuwa Dowans ndiyo iliyobeba mikoba, ilipaswa kuendeleza urejeshaji huo.

Kutokana na hali hiyo ya fedha za serikali kubaki kwa 'wawekezaji' hao waliopasiana mpira wa uwajibikaji, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kupitia timu ya wataalamu wa sheria, ilichunguza mkataba kati yake na Richmond ambao ulirithiwa na Dowans.
Taarifa ya timu ya wanasheria wa TANESCO ilibaini kuwa mkataba huo hauna nguvu za kisheria na kuamuru uvunjwe. Ukavunjwa rasmi Agosti Mosi, 2008.


Imebainika kuwa fedha zilizorejeshwa hadi mkataba unavunjwa ni jumla ya dola 7,674,186 za Marekani (zaidi ya sh bil. 7.7), huku dola za Marekani 23,022,412 (zaidi ya sh bil. 23) zikibakia kwa Richmond na mrithi wake Dowans.

Dowans waliweza kuingiza nchini mitambo ya kufua umeme na kuanza kazi, lakini ilizuka vuta nikuvute kati ya wawekezaji hao na wabunge, baada ya kudaiwa kwamba mitambo hiyo ilikuwa mibovu na haikufaa kwa lolote.
Mbali na tuhuma za ubovu wa mitambo hiyo, bado kwa mujibu wa mkataba serikali ililazimika kuilipa kampuni hiyo kiasi kikubwa cha fedha kwa mujibu wa mkataba, ingawa haikuzalisha umeme wowote.

Kutokana na hali hiyo, na baada ya mvutano mkubwa, serikali iliamua kuvunja mkataba huo jambo lililoifanya Dowans kwenda mahakamani kudai fidia.
Dowans ilifungua kesi dhidi ya TANESCO katika Mahakama ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC) ambayo hukumu yake iliiamuru TANESCO kulipa faini ya sh bil. 94 kwa kukatisha mkataba huo.


Taarifa zinaeleza kuwa hukumu hiyo yenye kurasa 211 ilionesha kuwa mmiliki wake pia anatuhumiwa kuwa ndiye aliyeileta Kampuni ya Richmond ambayo mkataba wa Richmond kwenda Dowans ulifanyika nje ya TANESCO kinyume cha sheria ya manunuzi ya umma.
Ni katika kipindi hicho, Dowans iliamua kuuza mitambo hiyo kwa Kampuni Symbion Tanzania, ambayo imesifiwa na kuchukua sura ya kuwa mitambo bora na ya kisasa ya kufua umeme hapa nchini.


Obama awashukia viongozi, Waziri Muhongo ajitetea

Katika hatua nyingine Rais Obama amewatupia shutuma viongozi wa serikali za Bara la Afrika kwa tabia yao ya ubabaishaji na kushindwa kutekeleza miradi wanayofadhiliwa na ile ya ndani kwa wakati muafaka. Rais Obama ameyasema hayo jana wakati akizungumza na wanahabari jana, kwenye mtambo wa kufua umeme wa Symbion, ulioko Ubungo jijini Dar es Salaam mbele ya mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete. Bila kutaja majina ya viongozi hao, Rais Obama alidai kuwa baadhi ya viongozi wa serikali wamekuwa hodari sana wa kupanga mipango ya maendeleo, lakini wasiweze kuisimamia na hata kuitekeleza.

Kauli hiyo ilipokelewa kwa hisia tofauti miongoni mwa watendaji wa serikali walioyokuwepo kiasi cha kumlazimu Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo kuitolea maelezo.
Muhongo akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya Rais Obama kuondoka, alikiri kuwepo kwa tatizo katika wizara yake kabla ya yeye kuongoza wizara hiyo. "Wakati naingia madarakani nilikuta tatizo la kiwanda cha saruji cha Mtwara kikizungushwa kupewa kibali cha kuanza kazi kwa zaidi ya miaka miwili, lakini katika uongozi wangu nimetumia muda wa saa mbili kuhakikisha wanapata kibali hicho," alisema.


Muhongo aliwahakikishia Watanzania kwamba mradi wa umeme wa nchi za Afrika (Power Africa Initiative) watautekeleza kwa wakati kwa kufikisha kila mkoa umeme wa uhakika ili tatizo hilo libaki kuwa historia.
Alibainisha kuwa ili kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana wamepanga kuongeza mara mbili ya umeme wa sasa ambao ni megawatt 1438.24 na kufikia megawatt 2780 hadi kufikia mwaka 2015. Lakini pia nchi inakusudia kufikia megawatt 3000.


Akizungumzia faida nyingine ya Obama kwa kuja Tanzania alisema baada ya kufanya mazungumzo wamefanikiwa kuongeza megawatt 600 za uzalishaji wa umeme katika mradi wa Symbion na GE.
Katika hotuba yake Rais Obama alisema kuwa mradi huo utakaofaidisha Watanzania katika awamu ya kwanza utagharimu kiasi cha dola bilioni 7 na pia nchi nyingine zitakazonufaika nao ni Ethiopia, Kenya, Liberia, Nigeria, Uganda na Msumbiji. Alisema kuwa sababu kubwa ya kuchagua nchi hizo imechagizwa na kuwa na malengo kabambe ya kufanya mageuzi katika sekta ya nishati kwa ajili ya kuboresha uwekezaji na ukuaji wa uchumi.


Akizindua rasmi mpango huo Maalum wa Maendeleo ya Nishati alisema kuwa msaada huo umetoka katika sekta binafsi na serikali ya Marekani.
Alisema kuwa sababu nyingine ni kuhakikisha wakazi wengi hasa wa maneo yasiyokuwa na umeme ambao ni asilimia kubwa kupata huduma hiyo. Katika ziara yake hiyo Obama pia alizindua mpira wa miguu ambao waliucheza na Rais Kikwete ukiwa maalumu kwa kuchaji simu na kuwasha taa ambao umetengezwa na Kampuni ya Unchartered play.inc.

Hivyo basi Obama suala la mitambo ya Symbion pale Ubungo amedandia tu kisiasa badala ya hali halisi na pengine ni mbinu za kisiasa kujitangaza na kusafisha virus waliomo ukichunguza historia ya mitambo hiyo.
 
Nisingefikiria uwopo wa wingi wa wageni nchini kipindi ni kigezo cha utetezi wakati Marekani iliweka utaratibu wa kuchuja nani wa kukutana na Obama. Kama kusingekuwa na tatizo hilo ambalo Marekani iliona tusingeambiwa kuwa Marekani imeweka utaratibi wa mchujo nani wa kumpokea na kusalimiana na Obama na wengine ambao hawataonekana pale maana yeke wamechujwa.

Vinginevyo utaratibu wa kugawana majukumu ya wageni mbalimbali yangebaki na sisi wenyewe wazawa vinginevyo naona utetezi wako
gfsonwin hauna uzito stahiki.

sasa kama ndivyo why asking yourselves such questions ilihali mnajua kwamba Marekani walishaweka list ya nani amwone raisi wao na nani asimwone??

kipengele cha baadhi ya viongozi kutokushirikishwa kwenye dinner sidhan kama kina mantiki yyte as waliopanga wanajua kwann na walioachwa hawajalalamika.
 
Kama jamii iliyojikita kwenye tope la mikwamo na mikingamo kibao, uongozi umeendelea kufumbia macho kila aina ya wito kuwa tuna idara na taasisi dhaifu sana.

Hivyo kwa yote yaliyotokea ni matokeo tu.
Wamarekani wamefanya kilichosahihi kwao na kutokana na namna sisi kama taifa tunavyotaka dunia ituelewe kuwa ni
"watu tunaotaka kusaidiwa kwenye kila kitu".
 
FBI wakagua ofisi ya Kova kwa mbwa

kova.jpg


kv.jpg
Hii habari iko kwenye magazeti, ni aibu has ukilinganisha na tambo zilizokuwa zimetolewa hapo awali
 
Hii ni aibu kubwa sana kwa serikali na vyombo husika vya usalama.

Mbaya zaidi lugha aliyotoa yule Mwanausalama wa Marekani kwa mwanausalama mzawa kwamba: "Hivi ndivyo mnavyofundishwa katika uwajibikaji kazini,"ni aibu kubwa kiasi kwamba mwanausalama wa Marekani uvumilivu ulimshinda na kuamua kumwambia wazi na kumruhusu dada aendelee na shughuli iliyomfikisha pale Makumbusho.
 
Naomba tuwe wazi Mkuu Candid Scope,

Unataka kusema kuwa Tanzania ina uwezo wa kufikia US Intelligence? Habari za Obama na Usalama kuwa mikononi mwa The US Intelligence zimekua ni habari ulizozisikia sana Tanzania sababu ni nchi yako una access ya kila habari inayotolewa. Pia na udhaifu wa baadhi ya Waandishi kushabikia na kuweka headlines katika hilo katika Obama's visit katika vitu viiingi ambavyo si msingi badala ya yale yenye msingi na yenye manufaa kwa maslahi ya nchi.

Ni aibu sana... Wananchi Uzalendo haupo kabisa, mtu anajitazama yeye na Chama anacho shabikia. Raisi anatoa hotuba badala ya kujadili kile anacho ongea rais kama kina mantiki ama hakina mtu anajadili kiingereza Kibovu. So Sad. Mwambie sasa yeye aongee Kiingereza.

Imefika wakati suala linapo husu taifa la Tanzania liangaliwe kwa Uzalendo na Upendo juu ya nchi na si kwa Unafiki na Ubinafsi. Kuna suala ambalo wengi wanajidanganya juu ya sifa ya Tanzania.... Mtu anadhani kuwa Tanzania ikiongelewa vibaya pamoja na Serikali basi CCM ndiyo inachekwa! Si kweli... Sikilizeni vyombo vya habari, hakuna anae jua CCM ni nini Ki mataifa hasa nchi za Ughaibuni! Wao wanajua kuwa Tanzania ni nini.

Baadhi ya watu/taasisi/Wanaharakati/Wanasiasa wamekosa misimamo na mbaya zaidi kudhihirisha ubinafsi wa hali ya juu! Serikali ya Kikwete na CCM in general ni wazi imeshindwa kuingozoa nchi. Kikwete amekuwa akisemwa, tukanwa, kashifiwa kwa safari za ovyo ovyo kuwa anajipendekeza... Wakati hapo hapo wao Wasemaji, Watukanaji na watoa Kashfa wanawapongeza the other side kwa kwenda kulia nje ya nchi jinsi Kikwete na Serikali yake inashindwa kuiongoza nchi. Haya ni kati ya makundi pakee ambayo yanaweza kuwa mkombozi wa Mtanzania ambaye hajui hata pa kuanzia kuweza kuikomboa nchi... Hapo kuna matumaini kweli?

It is time Upinzani uache kushindana na CCM, It is time waache kuingia kwenye mitego wazi, Maana sasa hivi inakuwa kama wote wapo sawa na tofauti ni kuwa tu CCM ina nguvu ya dola na Jeshi la polisi na Upinzani hawana.

Ujio wa Obama kuna ya Msingi ambayo inapaswa kuhoji, kujadili na kuelewa. BUT habari zilizo jaa ni ambazo tayari zimepita na wala hazina tija; habari zimejaa za - Obama ndege yake hivi, Malia Obama kabinti kazuri sana, Obama na Jk wacheza mpira, Obama hivi, Obama vile, Obama pale na Obama kibao!

Muda umefika sasa wa kuweka hayo pembeni na kutafakari Ujio wa Rais ambaye anakuwa Considered wa dunia kaja hapa Tanzania. What do we expect? Kikwete anatuambia nini? Wamekubaliana nini? Sisi Watanzania tunanufaika vipi? Na kutulia na kutafakari ile Conference Ikulu was it what it seems to be?

Tujenge nchi jamani... Nchi haijengwi na viongozi pekee bali na wananchi pia.

binafsi nilibahatika kuhojiwa na DW redio siku Obama alipokuja,na niliulizwa swali linaloendana na hapo kwenye highlight,na nikasema kuwa Ujio wa Obama hauna tija kwa mtanzania wa kawaida,Obama anakuja Tanzania kwa ajili ya rasilimali zetu,mafuta,gas,uranium na madini mengine,Obama ni mwafrika ila ni rais wa amerika,yupo pale kwa maslah ya amerika,na haishii hapo,Obama anata Afrika iwe na umeme ili kwa amerika iwe rahis ku-exploit resources,je leo akija mu-amerika na mtaj wa kuwekeza kwenye madini,na umeme hakuna atachimba?so binafsi nasema tusitarajie jipya juu ya Ujio wa Obama,labda kwa watawala na si kwako ASHA Dii wala kwangu
 
Last edited by a moderator:
wamerekani wanaijua sana africa na akili zao:
nigeria - boko haram
somalia - alshabaab
tanzania/zanzibar- uamsho
kwani hawamtaki rais wao? hawakutaka kuja kutoa lawama baadae, kinga ni bora kuliko kutibu. mi naafiki maamuzi yao
 
binafsi nilibahatika kuhojiwa na DW redio siku Obama alipokuja,na niliulizwa swali linaloendana na hapo kwenye highlight,na nikasema kuwa Ujio wa Obama hauna tija kwa mtanzania wa kawaida,Obama anakuja Tanzania kwa ajili ya rasilimali zetu,mafuta,gas,uranium na madini mengine,Obama ni mwafrika ila ni rais wa amerika,yupo pale kwa maslah ya amerika,na haishii hapo,Obama anata Afrika iwe na umeme ili kwa amerika iwe rahis ku-exploit resources,je leo akija mu-amerika na mtaj wa kuwekeza kwenye madini,na umeme hakuna atachimba?so binafsi nasema tusitarajie jipya juu ya Ujio wa Obama,labda kwa watawala na si kwako ASHA Dii wala kwangu
hebu mwangalie Mkoroshokigoli, Mtanzania mwelewa kabisa. Natamani angalau asilimia 51 tungepata uelewa wa kiasi hiki.
 
Candid Scope, AshaDii Mwita Maranya na wengine,

Nafikiri mtakuwa mnafanya kosa sana kufikiri Secrety Service ya USA wametunyanyasa.

Wao kwa sasa na hasa Obama kama Rais, hawawezi kuruhusu likafanyika kosa na Obama akashambuliwa na kudhurika au kuuawa. Imeshawahi kutokea huko nyuma na hawawezi kuruhusu kitu kama hicho. Sababu kadhaa zinazosababisha hiyo hali ni kama hizi:

1. Obama hadi leo hapendwi kabisa na watu kama Donald Trump na hadi alishafikia kusema wazi ingawa alifanya kama utani kuwa "watu kama Trump walikuwa wanaombea akienda msitu wa Amazon basi apotelee huko Milele...."
Ukiacha hao, kuna wale wa WHITE POWER, KKK nk ambao walishajitangazia zamani na kujiapiza kuwa OBAMA lazima afe. Kundi hili halipo tu USA ila hadi Ulaya ambako makundi haya ya WHITE POWER, SKIN HEAD walishajitangazia na wao kama wakipata nafasi basi ni lazima Obama afe. Wengi walilaani sana mara tu ilipomshinda H. Clinton na wakaanza kuona kuwa Mjaluo anaweza kushinda. Wakasema wazi kabisa ndiyo itakuwa mwisho wa WHITE RACE.

2. Kifo cha Osama bin Laden, wafuasi wake hadi leo hawajafurahia kabisa na wanamuwinda usiku na mchana.

3. Israel hawakufurahia kushinda kwake na hasa Bibi Netanyahu ambaye aliweka vita ya wazi kabisa na Obama wakati wa kampeni na kwa bahati mbaya akashindwa. Netenyahu na hao Orthodox wenzake hawajafurahi kushinda kwake hadi leo.

4. Makundi yote ya kigaidi ambayo yamepoteza viongozi wao kwa kuuawa na Drone za USA, wanamuwinda kwa nguvu. Hapo ukiongeza na wale wa Mali na waliopigwa Libya pamoja na Ghadaffi.

Unaweza kuongeza sababu nyingi tu na utagundua kuwa Obama ni zaidi ya maadui wa J F Kennedy ambao mwisho waliweza kumuuwa. Na Usalama wa Taifa, FBI, CIA nk wanalijua hilo na hawawezi kufanya makosa.

Kuna jamaa yangu mmoja aliniambia kuwa Obama alipotembelea nchi yao huko Ulaya, basi barabara nzima ilifungwa na watu wakaondolewa siku hiyo mjini City Centre. Kwa sababu anakaa karibu na barabara inayotoka/kwenda Airport, alishangaa kuwaona Wababa na bunduki zao (Snipers) wakiwa juu ya majengo wamevalia nguo nyeusi na msafara ulivyopita, wakashuka. Pia huko Ulaya pamoja na kuwa na ulinzi wa hali ya juu sana, bado USA ilileta Walinzi 300 miezi mitatu kabla na wiki moja kabla wakaja wengine 300 na idadi kuwa hiyo ya 600 kama walivyokuja Tanzania.

Tuacheni Complex ya kudhani USA wanatudharau. Sababu kubwa ni MAADUI wa Obama na si hatuna ulinzi. Hata akienda UK au Israel, ni haohao 600 wanakwenda na mji siku hiyo unaingia kwa kibali maalumu na wanasema pia hivyohivyo na wazi kabisa kuwa kama unaweza basi safiri nje ya Mji. Na jamaa yangu anasema kweli mji ulikuwa umepungua sana watu siku hiyo.
 
kwani Candid Scope unataka kusema ni lazima watu wote ambao ni viongozi kwenda kumwona Obama?? kumbuka kwamba wakati obama yupo pia viongozi wengine wa nchi za nje walikuwepo na walihitaj mwenyeji. mfano kulikuwa na GLOBAL 2013 SMART PARTNERSHIP na watu kama Mfalme Mswati, waziri mkuu wa Malysia, vice president wa Botswana etc sasa je unafikiri hawa hawakutakiwa kuwa na company?? nijuavyo kwa wakubwa kama hawa hata dinner hupangiwa watu wa kula nao so to me nafikri kutokuwepo kwa baadhi ya viongozi sishangai.

Nakupa mfano mdogo tu Chissano siku anakuja Obama alikuwa na Dinner na baadhi ya watu katika hotel aliyofikia na najua baadhi ya watu ambao walidine naye so usishangae sana juu ya hili.

Kumbe we hujaelewa mada. Mwanzo wa haya yote, kukukumbusha tu, ni amri ya kuchambua nani awepo na nani asiwepo. Period! Haya sasa anza kufikiria upya.
 
Last edited by a moderator:
Natanguliza shukrani kama utajibu hoja zangu kiufasaha badala ya majibu ya kunipeleka huko unakonielekeza. Hii si nukuru niliyoleta bali ni picha niliyoipata kwa kusoma na kusikiliza vyombo mbalimbali vya habari hali kadhalika kuisoma na kuelewa ziara nzima ya Rais Obama hapa nchini.

Jaribu kunileta utetezi kwa hoja zangu nilizoziweka hapo kwenye mada si kimipasho vile ufanyavyo ndugu yangu. Nchi hii ni yetu sote na waadhirika kama leto mmoja katika familia yako hayajampata ipo siku tageuka na kuikumbuka hoja yangu na kuthamini utaifa zaidi ya itikadi.
Ndugu yangu, kwa maoni yangu thread yako inadhihirisha jinsi ulivyosukumwa zaidi na dhamira za kisiasa, kiasi cha kukuacha u mtupu na kipofu kuhusu uzalendo wako.
Wenyewe wamarekani wana msemo kuwa 'where ever air force one lands, its America' wakimaanisha kuwa popote inapotua dege linalombeba Rais wa Marekani ni America.
Kwa sababu hiyo jukumu la ulinzi na usalama wa kiongozi wao na ujumbe wake linakuwa chini ya vyombo vya usalama vya marekani; iwe London, Ujerumani hata nchi ndogo km za Kiafrika. Kwa hilo hatumwi wala kuaminiwa mtu baki, na hiyo ndiyo itifaki wanayotumia, na ina gharama kubwa...SABABU!! Siasa za mabavu, uvamizi, na mauaji ya watu wasio na hatia kwa visingizio mbalimbali, zimesababisha kuibuka kwa maadui lukuki duniani. Ili kukabiliana na njama za kugeuziwa kibao, Marekani inafanya gharama kubwa kulinda wao wenyewe viongozi wake wa juu, hususan wakiwa katika ziara za nje ya nchi.
 
Kabla ya kuja Obama katika hizi nchi Za kiafrika, vyombo vya ulinzi na usalama vya marekani viliweka wazi kuwa ulinzi wa rais wao wataufanya wao kwa 100%, sasa hapo ww ulichoa andika ni kipi?.

Kuna thread aliiandika humu ndani mwanakijiji itafute uisome ndipo utajua ulicho andika ni ----- na ni craaaaaap ndani ya JF.

Sijafika mbali nimekutana na comment yako ya kwanza tu na mimi naonelea niichangie kabla ya kusonga mbele, kama umemuaelewa mleta mada amesema kuwa ni kweli katika ziara alizofanya Obama katika nchi za kiafrika safari hii ulinzi uliimarishwa sana tu lakini hakuna nchi ambayo wanausalama wa Marekani walifanya ulinzi kwa asilimia 100% bila kushirikisha nchi husika kama Tanzania walivofanya.
Na pia katika ziara hizo hakuna sehemu ambayo mchujo wa viongozi waandamizi wa serikali wa kwenda kumkaribisha uwanjani ulifanyika mbali na Tanzania tu.Kwa hiyo akasema kuwa labda wametuona kuwa sisi ni dhaifu kwa kuwa usalama wetu wameshindwa kudeal na issues ndogo ndogo na nyingine kubwa
 
Back
Top Bottom