Ujio wa Obama: Kashfa ya kupokwa ulinzi, vyombo vya habari vinavyoiona Tanzania

"Muda umefika sasa wa kuweka hayo pembeni na kutafakari Ujio wa Rais ambaye anakuwa Considered wa dunia kaja hapa Tanzania. What do we expect? Kikwete anatuambia nini? Wamekubaliana nini? Sisi Watanzania tunanufaika vipi? Na kulia na kutafakari ile Conference Ikulu was it what it seems to be?"

Usirudie makosa unayotukataza!! hebu tudadavulie hayo unayotuhubiri tufanye kwenye quote hapo juu!?
 

Naomba uangalie Diary yako kama hawa walikuja kabla au baada ya Sept 11.
 

AshaDii
Jaribu kurudi katika diary yako (au maktaba yako) ili ukumbuke kuwa Bush ametembelea Tanzania mwaka 2008, miaka mingi tu baada ya milipuko ya September Eleven. Aliyekuja Tanzania kabla ya milipuko hiyo ni Raisi Bill Clinton aliyekuja Tanzania mwaka 1998.
 
Last edited by a moderator:
Wanaijua vema siasa ya hatari inayochezwa na CCM hapa nchini kwa kutumia vyomba vya "ulinzi na usalama".
 
Tatizo kubwa liko kwa serikali yenyewe kupitia Wizara ya Mambo ya Nje kwa kushindwa 'kuiuza' sawasawa ziara hii kwa wananchi kwa minajili ya manufaa ya msingi (kiuchumi ? ). Hii ikasababisha 'media' kuibeba ziara hii katika 'celebrity agenda' kwani hawakuwa na taarifa nyingine za msingi. Upungufu huu wa Wizara unaweza kuwa ulisababishwa na usiri ulioambatana na baadhi ya ajenda za ugeni huu. Kwa hiyo ugeni umekuja,umeondoka lakini faida hasa ('topline and bottomline') bado hazijafahamika sawasawa .Kuhusu suala la ulinzi imebidi wa 'overdo' kwani ikiwa (inavyoonekana kwao) vyombo vyetu vyote vya usalama vimeshindwa kubaini waliosababisha bomu la kanisani na katika mkutano wa kampeni kule Arusha, je wataweza kubaini njama ambazo ni za hali ya juu zaidi? Wakati mwingine kutoaminika tunajitengenezea wenyewe..
 
Reactions: SMU
Kwahiyo IGP Saidi Mwema alikuwa anakula dinner na nani siku hiyo? akili mnazo lakini saa nyingine sijui mnazitumiaje...
Huyo ni Mwalimu by Profesional kwahiyo asikushangaze, nadhani unajuwa sifa ya kujiunga na Ualimu.
 
Kuna ombwe kubwa sana katika tasnia ya uandishi wa habari hapa Tanzania mkuu...vumilia tu!Mimi sijashika gazeti la Tanzania hata moja baada ya hii ziara kwa sababu najua media yetu will just scratch the surface tu.Nalingoja "The East African" Jumamosi nadhani nitapata habari na uchambuzi wa kueleweka
 

Nisingefikiria uwopo wa wingi wa wageni nchini kipindi ni kigezo cha utetezi wakati Marekani iliweka utaratibu wa kuchuja nani wa kukutana na Obama. Kama kusingekuwa na tatizo hilo ambalo Marekani iliona tusingeambiwa kuwa Marekani imeweka utaratibi wa mchujo nani wa kumpokea na kusalimiana na Obama na wengine ambao hawataonekana pale maana yeke wamechujwa.

Vinginevyo utaratibu wa kugawana majukumu ya wageni mbalimbali yangebaki na sisi wenyewe wazawa vinginevyo naona utetezi wako
gfsonwin hauna uzito stahiki.
 

Pamoja na kuangalia yaliyojilia ujio wa Obama, binafsi nimeshangazwa na suala la Richmond iliyorithishwa Dowans hatua kwa hatua hadi leo tuna SYMBION ambayo kimantiki ni kitu kile kile kilichobatizwa kisiasa kwa ujio wa Obama kama msaada wa Taifa la Marekani kuimarisha suala la umeme nchini. Kesho sitashangaa kuona mambo kama ilivyokuwa juzi, bora Wachina pamoja na mambo yao watafanya kitu kile cha kutukumbusha kwamba walikuwa nasi.

Soma makala haya toka Tanzania daima:

Hivyo basi Obama suala la mitambo ya Symbion pale Ubungo amedandia tu kisiasa badala ya hali halisi na pengine ni mbinu za kisiasa kujitangaza na kusafisha virus waliomo ukichunguza historia ya mitambo hiyo.
 

sasa kama ndivyo why asking yourselves such questions ilihali mnajua kwamba Marekani walishaweka list ya nani amwone raisi wao na nani asimwone??

kipengele cha baadhi ya viongozi kutokushirikishwa kwenye dinner sidhan kama kina mantiki yyte as waliopanga wanajua kwann na walioachwa hawajalalamika.
 
Kama jamii iliyojikita kwenye tope la mikwamo na mikingamo kibao, uongozi umeendelea kufumbia macho kila aina ya wito kuwa tuna idara na taasisi dhaifu sana.

Hivyo kwa yote yaliyotokea ni matokeo tu.
Wamarekani wamefanya kilichosahihi kwao na kutokana na namna sisi kama taifa tunavyotaka dunia ituelewe kuwa ni
"watu tunaotaka kusaidiwa kwenye kila kitu".
 
Hii ni aibu kubwa sana kwa serikali na vyombo husika vya usalama.

 

binafsi nilibahatika kuhojiwa na DW redio siku Obama alipokuja,na niliulizwa swali linaloendana na hapo kwenye highlight,na nikasema kuwa Ujio wa Obama hauna tija kwa mtanzania wa kawaida,Obama anakuja Tanzania kwa ajili ya rasilimali zetu,mafuta,gas,uranium na madini mengine,Obama ni mwafrika ila ni rais wa amerika,yupo pale kwa maslah ya amerika,na haishii hapo,Obama anata Afrika iwe na umeme ili kwa amerika iwe rahis ku-exploit resources,je leo akija mu-amerika na mtaj wa kuwekeza kwenye madini,na umeme hakuna atachimba?so binafsi nasema tusitarajie jipya juu ya Ujio wa Obama,labda kwa watawala na si kwako ASHA Dii wala kwangu
 
Last edited by a moderator:
wamerekani wanaijua sana africa na akili zao:
nigeria - boko haram
somalia - alshabaab
tanzania/zanzibar- uamsho
kwani hawamtaki rais wao? hawakutaka kuja kutoa lawama baadae, kinga ni bora kuliko kutibu. mi naafiki maamuzi yao
 
hebu mwangalie Mkoroshokigoli, Mtanzania mwelewa kabisa. Natamani angalau asilimia 51 tungepata uelewa wa kiasi hiki.
 
Candid Scope, AshaDii Mwita Maranya na wengine,

Nafikiri mtakuwa mnafanya kosa sana kufikiri Secrety Service ya USA wametunyanyasa.

Wao kwa sasa na hasa Obama kama Rais, hawawezi kuruhusu likafanyika kosa na Obama akashambuliwa na kudhurika au kuuawa. Imeshawahi kutokea huko nyuma na hawawezi kuruhusu kitu kama hicho. Sababu kadhaa zinazosababisha hiyo hali ni kama hizi:

1. Obama hadi leo hapendwi kabisa na watu kama Donald Trump na hadi alishafikia kusema wazi ingawa alifanya kama utani kuwa "watu kama Trump walikuwa wanaombea akienda msitu wa Amazon basi apotelee huko Milele...."
Ukiacha hao, kuna wale wa WHITE POWER, KKK nk ambao walishajitangazia zamani na kujiapiza kuwa OBAMA lazima afe. Kundi hili halipo tu USA ila hadi Ulaya ambako makundi haya ya WHITE POWER, SKIN HEAD walishajitangazia na wao kama wakipata nafasi basi ni lazima Obama afe. Wengi walilaani sana mara tu ilipomshinda H. Clinton na wakaanza kuona kuwa Mjaluo anaweza kushinda. Wakasema wazi kabisa ndiyo itakuwa mwisho wa WHITE RACE.

2. Kifo cha Osama bin Laden, wafuasi wake hadi leo hawajafurahia kabisa na wanamuwinda usiku na mchana.

3. Israel hawakufurahia kushinda kwake na hasa Bibi Netanyahu ambaye aliweka vita ya wazi kabisa na Obama wakati wa kampeni na kwa bahati mbaya akashindwa. Netenyahu na hao Orthodox wenzake hawajafurahi kushinda kwake hadi leo.

4. Makundi yote ya kigaidi ambayo yamepoteza viongozi wao kwa kuuawa na Drone za USA, wanamuwinda kwa nguvu. Hapo ukiongeza na wale wa Mali na waliopigwa Libya pamoja na Ghadaffi.

Unaweza kuongeza sababu nyingi tu na utagundua kuwa Obama ni zaidi ya maadui wa J F Kennedy ambao mwisho waliweza kumuuwa. Na Usalama wa Taifa, FBI, CIA nk wanalijua hilo na hawawezi kufanya makosa.

Kuna jamaa yangu mmoja aliniambia kuwa Obama alipotembelea nchi yao huko Ulaya, basi barabara nzima ilifungwa na watu wakaondolewa siku hiyo mjini City Centre. Kwa sababu anakaa karibu na barabara inayotoka/kwenda Airport, alishangaa kuwaona Wababa na bunduki zao (Snipers) wakiwa juu ya majengo wamevalia nguo nyeusi na msafara ulivyopita, wakashuka. Pia huko Ulaya pamoja na kuwa na ulinzi wa hali ya juu sana, bado USA ilileta Walinzi 300 miezi mitatu kabla na wiki moja kabla wakaja wengine 300 na idadi kuwa hiyo ya 600 kama walivyokuja Tanzania.

Tuacheni Complex ya kudhani USA wanatudharau. Sababu kubwa ni MAADUI wa Obama na si hatuna ulinzi. Hata akienda UK au Israel, ni haohao 600 wanakwenda na mji siku hiyo unaingia kwa kibali maalumu na wanasema pia hivyohivyo na wazi kabisa kuwa kama unaweza basi safiri nje ya Mji. Na jamaa yangu anasema kweli mji ulikuwa umepungua sana watu siku hiyo.
 

Kumbe we hujaelewa mada. Mwanzo wa haya yote, kukukumbusha tu, ni amri ya kuchambua nani awepo na nani asiwepo. Period! Haya sasa anza kufikiria upya.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu yangu, kwa maoni yangu thread yako inadhihirisha jinsi ulivyosukumwa zaidi na dhamira za kisiasa, kiasi cha kukuacha u mtupu na kipofu kuhusu uzalendo wako.
Wenyewe wamarekani wana msemo kuwa 'where ever air force one lands, its America' wakimaanisha kuwa popote inapotua dege linalombeba Rais wa Marekani ni America.
Kwa sababu hiyo jukumu la ulinzi na usalama wa kiongozi wao na ujumbe wake linakuwa chini ya vyombo vya usalama vya marekani; iwe London, Ujerumani hata nchi ndogo km za Kiafrika. Kwa hilo hatumwi wala kuaminiwa mtu baki, na hiyo ndiyo itifaki wanayotumia, na ina gharama kubwa...SABABU!! Siasa za mabavu, uvamizi, na mauaji ya watu wasio na hatia kwa visingizio mbalimbali, zimesababisha kuibuka kwa maadui lukuki duniani. Ili kukabiliana na njama za kugeuziwa kibao, Marekani inafanya gharama kubwa kulinda wao wenyewe viongozi wake wa juu, hususan wakiwa katika ziara za nje ya nchi.
 

Sijafika mbali nimekutana na comment yako ya kwanza tu na mimi naonelea niichangie kabla ya kusonga mbele, kama umemuaelewa mleta mada amesema kuwa ni kweli katika ziara alizofanya Obama katika nchi za kiafrika safari hii ulinzi uliimarishwa sana tu lakini hakuna nchi ambayo wanausalama wa Marekani walifanya ulinzi kwa asilimia 100% bila kushirikisha nchi husika kama Tanzania walivofanya.
Na pia katika ziara hizo hakuna sehemu ambayo mchujo wa viongozi waandamizi wa serikali wa kwenda kumkaribisha uwanjani ulifanyika mbali na Tanzania tu.Kwa hiyo akasema kuwa labda wametuona kuwa sisi ni dhaifu kwa kuwa usalama wetu wameshindwa kudeal na issues ndogo ndogo na nyingine kubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…