Ujio wa Rais wa Ujerumani Serikali itumie fursa

Ujio wa Rais wa Ujerumani Serikali itumie fursa

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
12,675
Reaction score
25,924
1. Wajerumani ndio waliojenga reli ya kati, na ile ya Dar es Salaam, Tanga, Moshi, tukiongea nao vizuri wanaweza kuboresha Dar, Tanga, Moshi, Arusha kuwa SGR.

2. Ujerumani wapo vizuri sana kwenye miundombinu ya majiji, tukiongea nao vizuri wanaweza kutoa ushirikiano au hata ufadhili kwenye usafiri wa mijini, mfano, Dodoma na Dar inafaa kabisa isiwe na mabasi tu, iwe na trams tena za umeme.

Miji mikubwa yote duniani ina trams, hadi moroko wanazo hapahapa Afrika. hizo huwa zinasaidia sana hasa shida ya mafuta ikitokea kwasababu hazitumii mafuta, na zinatembea humohumo katikati ya barabara hizihizi ambazo magari yanatumia.

3. Ujerumani wapo vizuri kwenye sekta ya afya, ufadhili wanafunzi wetu wakasome huko tupate madaktari bingwa.

4. Ujerumani wapo vizuri sana kwenye viwanda vya magari, hata wasipofungua assembly plants hapa, vijana wachukue hata spareparts au used sio mbaya.

5. Ujerumani wapo vizuri kwenye shirika la ndege, lianze kuja hapa lilete utalii.

6. Ujerumani ni nchi ya kwanza kwa utajiri Ulaya, watu wake wana kipato, hivyo utalii wanaweza kutufaa.

7. Ujerumani ni mshirika mkubwa sana wa EU, ukimkamata umekamata EU yote.
 
yaani badala ya kujadiliana naye suala la msingi, tujadiliane mjusi?
Kwa hiyo mjusi unaona siyo swala la msingi, unajua wanaingiza mabilioni kiasi gani kwa utalii wa huyo mjusi?
 
Daah mueshimiwa rais akiweza amualike ndugu Ruto wajadili na huyo mjerumani uwezekano wa kufufua reli ya kihostoria iliyopo moshi kwenda mombasa ili wakenya wafanyabiashara na wakulima watanzania wa mazao wanufaike pia
 
Tatizo wamatumbi hamjui kutunza vitu. Shule, reli, hospital zote alizoacha mjerumani zote mmeshindwa kuziendesha zimechoka kuliko maelezo. Wakijenga hivyo vitu walete na watu wao wasimamie.
 
Kwa hiyo mjusi unaona siyo swala la msingi, unajua wanaingiza mabilioni kiasi gani kwa utalii wa huyo mjusi?
Umeshindwa kuingiza mabilioni kwenye madini,gas na mbuga ulizonazo ndio uje kupata kwa Mjusi mmoja?
 
Back
Top Bottom