Ujio wa SGR tishio kwa mabasi? Inabeba abiria 4000 sawa na trip 70 za mabasi

Hofu ya nini?
 
Binafsi nahisi itaongeza usafiri wa mabasi,yatakuwa efficient sana sasa hivi na watayaendesha kisasa, ni kubadili namna walivyojipanga sasa.

Kila tatizo lina fursa kubwa ndani yake.

Hata biashara ya mizigo kwa matruck naona itaongeeka, siyo mizigo yote inaishia inaposhusha na kupakia reni, hali kadhalika kwa abiria.
 
Dunaini kote usafiri wa kila aina upo na wote wanapata riziki zao
Huku nilipo mpaka meli zipo
Ukitaka ndege pia kwenda nchi jirani ni rahisi kuliko kwenda mji mwingine ndani ya nchi
Wapo watakaopanda bus na wapo wa train na hata ndege
Acha na mimi nianzishe route za boat kwenye mito
Maana naona mito yetu ni kwa ajili ya mamba na viboko tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…