Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Kuna vitu vinatokea kwa namna ya kipekee na ajabu kabisa. Ujio wa Lissu kurejea nyumbani akiwa bukheri wa afya una mengi ya kusimulia
Lissu aliyeondoka mahututi hajitambui kwenye machela baada ya kunusurika kifo cha risasi 36, anarejea nchini akiwa mwenye tabasamu na matumaini mengi.
Mtuhumiwa wake kwenye shambulio husika wakati huo alikuwa mwenye mamlaka na nguvu nyingi akiivinjari nchi atakavyo huku akifanya atakayo bila kuguswa na yeyote yule.
Leo hii Lissu anaporejea nchini mtuhumiwa wake si lolote si chochote tena(labda huko mbeleni) mtuhumiwa wake sasa ni mwananchi wa kawaida kabisa mwenye msongo wa mawazo huku sintofahamu ikimtawala kuhusu future yake. Anachosubiri kwasasa ni huruma ya mkulu kama kwa bahati mbaya wakiweza kufanya figisu.
Imagine leo hii Lissu anapokaribia kabisa kurudi mwana bado angekuwa na yale maguvu yake, sipati picha ingekuwaje. Kuna maanguko huja kwa hatua. Wazungu wanasema: A day when everything went wrong. Waswahel wanasema siku imeanza vibaya, na siku ya kufa nyani miti yote huteleza.
Umeteleza wa ubunge kwenye kura za wajumbe, unaweza kuteleza kwenye uteuzi, ama kwenye viti maalum.
Mambo huja kinyume. Wakati Lissu atakapokuwa kwenye msafara wa hiari, mwana atakuwa kajificha mahali na remote mkononi akiangalia kwa uchungu live updates za mbaya wake mwenye na uso wa tabasamu kubwa.