Ujio wa Yesu mara 2

Neno limefadanua wazi,

Unyakuo utatokea kwanza, Yesu atakuja bila kuikanyaga ardhi ya Dunia akiwa hapo juu mawinguni na kuwanyakua WATAKATIFU wake,

Walioachwa duniani bila kunyakuliwa, watapitia taabu chini ya utawala wa shetani duniani chini ya mwanaye aitwaye mpinga Kristo.

Watashuka duniani Malaika wa kuhubiri injili duniani Kwa walioachwa, Elia pia atashuka pia na kuonyesha ukuu wa Mungu duniani.

Wapo baadhi watakataa kumtii shetani kama mfalme na kuendelea kumkubali Yesu/Mungu kama mfalme wao, hao watakatwa vichwa na kuuwawa Kwa mateso MAKALI. Wakati huo WATAKATIFU watakuwa mapumzikoni.

Baada ya WATAKATIFU kukatwa vichwa watazikwa, Elia atauwawa Kisha baada ya siku tatu atafufuka na Kupata Mbinguni, Shetani atakusanya jeshi lake la mapepo Walio katika form ya WANADAMU Kisha watakusanyika Kwa vita iitwayo almagedon, Yesu atashuka akiwa na WATAKATIFU wake walionyakuliwa na wale waliokuwa Mbinguni baada ya kufa katika unyofu na HAKI ya Mungu, waliookolewa na kuwaangamiza vita ya kimwili iitwayo almagedon.

Hapo ndipo makaburi yatafunguka, WATAKATIFU watatoka na kumlaki mawinguni na Kila jicho litamwona.

Vitabu vitafunguliwa, HUKUMU itafanywa Kwa waovu wema Kwa Uzima WA milele na waovu watu wasiookoka, mapepo na shetani jehanum. Dunia itachomeka na vyote vilivyomo.

Baada ya hapo ndipo umilele utaanza itakuja mbingu mpya na Nchi mpya.

Hayo ni Kwa ufupi ingawa sijaandika Kwa mtiririko sahihi.

Aamen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…