Hat-Trick
Senior Member
- Jun 15, 2020
- 117
- 382
Kiwanda kikubwa cha uzalishaji soda za Pepsi, Seven Up, Mirinda, Mountain Dew n.k ambacho ni cha kanda ya kusini nyanda za juu SBC Mbeya Plant (Pepsi) kinaudumia takribani mikoa 3 au 4 yani Ruvuma, Iringa, Njombe na Mbeya yenyewe.
Vibarua wa kutwa wanalipwa 4,600/ kwa masaa 12 ya kazi wanaingia saa 07:00 asubuhi na kutoka saa 06:30 jioni.
Majukumu ya vibarua hawa muhimu,
1. Wanakagua na kuchambua chupa iliyotoka sokoni kama inafaa tena kutumika yani kwa walaji kabla ya kuoshwa kwenye mashine.
2. Wanazikagua na kuchambua chupa baada ya kuoshwa kwenye mashine kama zinafaa kutiwa soda tayari kwenda kwa walaji.
3. Wanakagua kila soda inayozalishwa kama ina muhuli wa TRA.
4. Wanakagua na kuchambua soda ambazo zipo tayari zinaoenda sokoni kama ni safi na salama hazina hitilafu kama vile ujazo,uchafu n.k
5. Kupanda kreti za soda kwenye pareti kwa ajili ya kuifadhiwa store.
Hayo ni majukumu muhimu zaidi kwa hawa wanaitwa vibarua wa "Production" bila uwepo wao kazi haziendi ni muhimu sana lakini maslahi yao ni madogo kwa mda wanaofanya kazi.
Wito kwa Mbunge wa jimbo la Mbeya tembelea Kiwandani ujionee wapiga kura wako kwa macho jinsi watu wanavyofanya kazi huku wakilalama si vibarua, si waajiriwa ni ujira wa chini sana hauridhishi, haukidhi kabisa tofauti kabisa viwanda vya jirani kama Cocacola na TBL.
4,600 ukiichambua inatumika hivi 2,000/ kula mchana na jioni,1,000 nauli kwenda na kurudi.
Balance Tsh.1,600/=