Ni muda mrefu sana nahangaika juu ya ugonjwa huu unaitwa utango tango,kama ni madawa nimetumia mengi sana,zipo za kunywa na zingne za kupaka lakin unapotea na kurudi tena.
Inawezekana ikawa ni ugonjwa wa kurithi,sababu katika familia kuanzia baba na watoto wote wa kiume tunaathirika na ugonjwa
Mm inabid nihangaike sana,sababu bado ni kijana na pia sehem zingne inatafsirika kama ni uchafu,na ni kweli inachangia sana kuondoa utanashati wa mtu.
Najua wapo wenye tatizo kama langu,sasa kwa aliefanikiwa kuliondoa kabisa,tusaidiane katika hili..