Uchaguzi 2020 Ujue utaratibu wa kuwasilisha, kushughulikia na kukata rufaa malalamiko kamati ya kitaifa ya maadili

Uchaguzi 2020 Ujue utaratibu wa kuwasilisha, kushughulikia na kukata rufaa malalamiko kamati ya kitaifa ya maadili

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2007
Posts
18,772
Reaction score
8,939
Kwa mujibu wa GAZETI LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA la Tarehe 5 Juni, 2020 SEHEMU YA TANO Ukururasa wa 15. Angalia Kiambatisho.

5.4 Uwasilishaji wa Malalamiko

Mgombea yeyote, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Serikali au chama kilichosaini Maadili ya Uchaguzi na kuweka
mgombea endapo kinaamini kwamba Maadili ya Uchaguzi yamekiukwa kitawasilisha malalamiko yake kwa
Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Uchaguzi katika ngazi husika kwa maandishi.


5.5 Muda wa kuwasilisha malalamiko ya ukiukwaji wa Maadili

Malalamiko yoyote yatakayotokea yatawasilishwa kwa maandishi kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili
ya Uchaguzi ya ngazi husika ndani ya saa sabini na mbili (72) tangu kutokea kwa tukio linalolalamikiwa.


5.6 Kuitisha kikao cha Maadili ya Uchaguzi

Mwenyekiti wa Kamati husika baada ya kupokea malalamiko anatakiwa kuitisha kikao ndani ya saa arobaini
na nane (48).


5.7 Utaratibu wa kushughulikia Malalamiko

Utaratibu wa kushughulikia malalamiko dhidi ya ukiukwaji wa maadili utakuwa kama ifuatavyo-
(a) malalamiko yote yatajadiliwa na kuamuliwa katika kikao cha Kamati ya Maadili ya Uchaguzi kwenye
ngazi husika;
(b) Kamati itashughulikia malalamiko na kutoa uamuzi wake mapema iwezekanavyo;
(c) baada ya kupokea malalamiko, Kamati itamtaka anayelalamikiwa kuwasilisha utetezi wake kwa
maandishi ndani ya saa arobaini na nane (48) tangu kupokea taarifa ya malalamiko dhidi yake;
(d) katika kushughulikia malalamiko, Kamati inaweza kumuita mtu yeyote kutoa maelezo ili kusaidia
Kamati kufikia maamuzi ya haki;
(e) akidi ya kikao cha Kamati husika itakuwa zaidi ya nusu ya wajumbe wote wa Kamati;


(f) Kamati itaamua malalamiko yote ndani ya muda wa saa arobaini na nane (48) baada ya kusikiliza au
kupata maelezo ya utetezi kutoka kwa pande zote mbili ambazo ni mlalamikaji na mlalamikiwa;
(g) maamuzi yatakayofikiwa na Kamati ya Maadili ya Uchaguzi yatatekelezwa na pande zinazohusika na
maamuzi hayo;
(h) ikitokea kuna umuhimu wa kufanya maamuzi kwa kupiga kura, wawakilishi wa mlalamikaji na
mlalamikiwa wasiruhusiwe kupiga kura juu ya maamuzi hayo;
(i) malalamiko yatakayoshughulikiwa na Kamati ya Maadili ya Uchaguzi ni yale ya kipindi cha kampeni
za uchaguzi tu;
(j) malalamiko yatakayotokea siku ya upigaji kura yatashughulikiwa na msimamizi wa kituo cha kupigia
kura, Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, Msimamizi wa Uchaguzi au Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa
mujibu wa sheria za uchaguzi;
(k) Kamati itakuwa na mamlaka ya kuchunguza malalamiko yote yatakayowasilishwa kabla ya kufanya
maamuzi; na
(l) Kamati inaweza kuelekeza malalamiko mengine kupelekwa kwenye mamlaka husika kama itakavyoona
inafaa.


5.8 Rufaa dhidi ya maamuzi ya Kamati

Upande ambao hautaridhika na uamuzi wa Kamati ya Maadili ya Uchaguzi una haki ya kukata rufaa kwa
taratibu zifuatazo-
(a) kama ni malalamiko yaliyoshughulikiwa katika ngazi ya kata husika, rufaa itakatwa kwenda kwa
Msimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili husika ndani
ya saa ishirini na nne (24) tangu uamuzi unaokatiwa rufaa ulipotolewa;
(b) uamuzi utakaotolewa na Kamati ya Jimbo utakuwa ni wa mwisho kwa malalamiko yote yaliyoanzia
ngazi ya Kata;
(c) iwapo malalamiko yaliyoshughulikiwa ni kutoka ngazi ya Jimbo, rufaa itakatwa kwenda kwa
Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Kitaifa ndani ya saa 48 tangu uamuzi husika ulipotolewa;
(d) uamuzi wa Kamati ya Kitaifa utakuwa ni wa mwisho kwa malalamiko yote yaliyoanzia ngazi ya
Jimbo;
(e) iwapo malalamiko yaliyoshughulikiwa ni kutoka Kamati ya Kitaifa, rufaa itakatwa kwenda Kamati
ya Rufaa ndani ya saa arobaini na nane (48) baada ya uamuzi wa Kamati ya Kitaifa kutolewa;
(f) endapo kuna umuhimu wa kufanya maamuzi kwa kupiga kura, wawakilishi wa mlalamikaji na
mlalamikiwa hawataruhusiwa kupiga kura ya maamuzi; na
(g) upande usioridhika na maamuzi ya Kamati kwenye hatua ya mwisho ya rufaa husika unaweza kufungua
malalamiko ya Uchaguzi Mahakamani kwa mujibu wa Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 au
Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura ya 292.
 

Attachments

MY TAKE:
Kwa mtizamo wangu mimi wajumbe ni kuw aTume imechemka tena kwani nilivyoelewa mimi ni kuwa :-

1. Mlalamikaji yeyote awe mgombea, Serekali, Tume yenyewe au Chama chenye mgombea anapaswa kuwasilisha malalakiko kwenye Kamati kwanza kabla ya masaa 72 kuisha.

2. Kamati inapaswa kuitishwa ijadili na ijiridhishe kuwa kuna kosa limetendekaa , then ndipo mlalamikiwa atumiwe malala miko ayajibu.

3. Akijibu mamammiko ndani ya saa 48 ndipo sas amaamuzi yanwqeza kufanyika.

Je kwanini mwenyekiti huyu kakimbiulia kumuita Lissu Dar Es Salaam wakakti hata kamti haijaitishwa na ikakaa ikajadili na kujirisha kuwa mashtaka yanamashiko ?


Naamini Mwenyekiti alishinikizwa ndio maana alikuja amepanic na kutufokea, Hata leo nimemsikiliza na ukisikiliza alichokiongea jana lissu( nahisi pia alikosea kusema ni 48hrs tu, hii kitu ni mlolongo mrefu sana) bado amekosea tena mwenyekiti huyu.
 
Kama makosa ya Lissu yana wiki moja nyuma, tayari tume imeshachelewa, maana wanatakiwa wapeleke malalamiko yao tume ya maadili ndani masaa 72 baada ya matendo wanayolalamikia kutokea.

Lissu akifika hapo kwenye kikao anawauliza swali rahisi tu.

Haya makosa mnayosema nilitenda niliyatenda tarehe ngapi na wapi?

Ushahidi uko wapi?

Basi anawaambia kuwa kwa mujibu wa kanuni kwamba "matendo yenyewe ninayotuhumiwa kwayo yalitokea wiki kadhaa nyuma, na hivyo basi muda wa kunishtakia kwayo umeshapita, naomba tume iachane na shauri hili maana ni kinyume cha kanuni na hivyo ninkinyume cha sheria!"
 
Back
Top Bottom