- Tunachokijua
- Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika Januari 19, 2025 ulimpitisha kuwa mgombea wa nafasi ya Urais huku Dkt. Hussein Mwinyi kuwa mgombea Urais wa Zanzibar.
Wanu Hafidh Ameir mtoto wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ni mwanasiasa wa CCM ambaye amekuwa ni mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar katika Bunge la Taifa la Tanzania tangu mwaka 2005. Aidha kuelekea uchaguzi mkuu 2025 Wanu alichukua fomu ya kuwania Ubunge Jimbo la Makunduchi, Mkoa wa Kusini Unguja Visiwani Zanzibar.
Madai
Kumekuwepo na Picha inayosambazwa mtandaoni ikiwa na ujumbe unaodaiwa kuchapishwa na Rais Samia kwenye mtandao wa X akiomba wana Makunduchi wamchague Wanu Hafidh Ameir
"Wana Makunduchi naomba Tarehe 29 Oktoba mnichagulie mwanangu Wanu Hafidh Ameir msiniangushe Kazi na Utu"
Uhalisia
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key words search) umejiridhisha kuwa ujumbe huo haujachapishwa kwenye ukurasa rasmi wa Rais Samia kupitia mtandao wa X.
Aidha ujumbe huo una mapungufu yanayodhihirisha kuwa ni wa kutengenezwa na wapotoshaji. Picha yenye ujumbe huo haiakisi uhalisia kama ilivyo katika mtandao wa X, mfano kutumika kwa tiki ya bluu (blue checkmark) badala ya tiki yenye rangi ya kijivu (Grey checkmark) ambayo inatumiwa na Rais Samia.
Kukosekana kwa alama ya Grok, nukta tatu upande wa juu kulia, umbo la picha katika sehemu zenye kona ni tofauti na machapisho kutoka mtandao wa X, muonekano wa picha ya wasifu. Pia kwenye mtandao wa X Rais Samia anatumia 'Samia Suluhu' na si Samia Suluhu Hassan kama inavyoonena