Ujumbe kutoka kwa Askofu Mwamakula: Haki haiwezi kufa

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,767
Reaction score
288,340
SAUTI YA ASKOFU KWA WATETEZI WA HAKI KATIKA JAMII!

Haki haiwezi kufa! Mtu anaweza kuwaua watetezi wa haki, lakini hawezi kufanikiwa kuiua haki! Haki haiwezi kununuliwa! Mtu anaweza kuwanunua wapigania haki, lakini hawezi kuinunua haki yenyewe! Haki haitishwi! Mtu anaweza kuwatisha watetezi wa haki, lakini hawezi kuitisha haki yenyewe! Haki hainyamazishwi! Mtu anaweza kuwanyamazisha watetezi wa haki, lakini haki itaendelea kupiga kelele! Haki hazeeki na hachoki. Watetezi wa haki wanaweza kuchoka na kuzeeka, lakini haki hachoki na wala hazeeki, na badala yake huwainua wengine walio na ujasiri kuliko wa mwanzo!

Mtu anaweza kudhoofisha na kubomoa majengo, taasisi, vyombo, na vifaa vinavyotumika katika kupaza sauti ya Haki, lakini hawezi kufanikiwa kuidhoofisha na kuibomoa haki! Haki ni ushahidi wa uwepo wa Mungu aliye hai katika jamii! Ukisikia kelele, sauti, vilio na miito ya haki usipambane nayo! Ujue kuwa hizo ni kelele za Mungu mwenyewe! Hizo ni sauti kutoka kwa Mungu aliye Haki! Haki ndiye Hekima mwenyewe anayetajwa katika Biblia Takatifu kitabu cha Mithali 8:1-36.

Ewe mtu unayetetea na kupigania haki mahali popote, katika taasisi ye yote na katika mazingira ye yote! Usikatishwe tamaa unapoona sauti ulizozitegemea zikinyamaza; na wala usiogope kuona uovu ukijiimarisha zaidi katika jamii. Haki hahitaji umati wa watu katika kushinda mapambano na wala hahitaji jeshi ili kuwanyamazisha madui zake! Yeye Haki ni Wakati! Wakati wake ukifika, Haki hupita katikati ya matusi, kejeli, dharau, watesi, majeshi na umma wa watu na kisha kuanza kuhesabu mateka na kuitweka bendera ya ushindi! Wakati wa Haki ukifika, hata wale waliomtweza, waliopambana katika kumtusi, waliowaua na kuwanyamazisha watetezi wa Haki; wote kwa pamoja watapaza sauti zao kumshangilia Haki! Haki hana dini ingawa anawatumia watu wa dini na wasio wa dini katika kutangaza uwepo wake!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki
 
Huyu Askofu na mwenzie Bagonza nawapenda sana kwa kutomuhofia huyo dikteta na kusema ukweli bila kuficha.

Imagine Nchi yetu ingekuwa wapi leo hii kama Mapadri na Masheikh wote Nchini wangeacha UNAFIKI wao wa kuwakumbatia hawa wahuni wa ccm wanaondeleza maovu ya kutisha Nchini.

Madini tuuu kama yale ya Laizer
 
Haki unayozungumzia ni hii anayoitenda Rais John Pombe Magufuli. Kwa mfano ya kukomboa mali asili zetu na kusimamia maendeleo ya wa Tanzania kwa umakini na weledi.

Kinyume cha haki ni kile kinacho hubiliwa na watu kama Lissu - mali asili yetu ibakie kwa wazungu (rec. ACACIA) na kututishia kuadhibiwa tukiwaadabisha! Hiyo si haki. Kukumbatia watesi wetu ambao hawatambui utu wetu! Ni kinyume cha haki.
 
Angekuwa anatenda haki Ben Saanane asingepotea, Azory Gwanda asingepotea, Lissu asingeshambuliwa, Kabendera na wengi wengine WASINGEBAMBIKIWA kesi FAKE. Angekuwa anatenda HAKI angeheshimu katiba, bunge na mahakama na pia ANGEKUMBATIA Uchaguzi HURU na wa HAKI. Mkapa anataka Uchaguzi wetu uwe HURU na wa HAKI, Kwanini dikteta ANAHOFIA Uchaguzi HURU na wa HAKI kwanini anahofia TUME HURU kama anatenda haki? Kwanini ccm inahofia TUME HURU?

2451764_ERFcWLLW4AIVOAq.jpg

Haki unayozungumzia ni hii anayoitenda Rais John Pombe Magufuli. Kwa mfano ya kukomboa mali asili zetu na kusimamia maendeleo ya wa Tanzania kwa umakini na weledi.
Kinyume cha haki ni kile kinacho hubiliwa na watu kama Lissu - mali asili yetu ibakie kwa wazungu (rec. ACACIA) na kututishia kuadhibiwa tukiwaadabisha! Hiyo si haki. Kukumbatia watesi wetu ambao hawatambui utu wetu! Ni kinyume cha haki.
 
Haki unayozungumzia ni hii anayoitenda Rais John Pombe Magufuli. Kwa mfano ya kukomboa mali asili zetu na kusimamia maendeleo ya wa Tanzania kwa umakini na weledi.

Kinyume cha haki ni kile kinacho hubiliwa na watu kama Lissu - mali asili yetu ibakie kwa wazungu (rec. ACACIA) na kututishia kuadhibiwa tukiwaadabisha! Hiyo si haki. Kukumbatia watesi wetu ambao hawatambui utu wetu! Ni kinyume cha haki.
Jaribu kupanua uelewa wako itakusaidia kuacha kupayuka hovyo usio na uhakika nayo. AMEN

The Multilateral Investment Guarantee Agency (MIGA) is an international financial institution which offers political risk insurance and credit enhancement guarantees. These guarantees help investors protect foreign direct investments against political and non-commercial risks in developing countries.[2] MIGA is a member of the World Bank Group and is headquartered in Washington, D.C. in the United States.
 
SAUTI YA ASKOFU KWA WATETEZI WA HAKI KATIKA JAMII!

Haki haiwezi kufa! Mtu anaweza kuwaua watetezi wa haki, lakini hawezi kufanikiwa kuiua haki! Haki haiwezi kununuliwa! Mtu anaweza kuwanunua wapigania haki, lakini hawezi kuinunua haki yenyewe! Haki haitishwi! Mtu anaweza kuwatisha watetezi wa haki, lakini hawezi kuitisha haki yenyewe! Haki hainyamazishwi! Mtu anaweza kuwanyamazisha watetezi wa haki, lakini haki itaendelea kupiga kelele! Haki hazeeki na hachoki. Watetezi wa haki wanaweza kuchoka na kuzeeka, lakini haki hachoki na wala hazeeki, na badala yake huwainua wengine walio na ujasiri kuliko wa mwanzo!

Mtu anaweza kudhoofisha na kubomoa majengo, taasisi, vyombo, na vifaa vinavyotumika katika kupaza sauti ya Haki, lakini hawezi kufanikiwa kuidhoofisha na kuibomoa haki! Haki ni ushahidi wa uwepo wa Mungu aliye hai katika jamii! Ukisikia kelele, sauti, vilio na miito ya haki usipambane nayo! Ujue kuwa hizo ni kelele za Mungu mwenyewe! Hizo ni sauti kutoka kwa Mungu aliye Haki! Haki ndiye Hekima mwenyewe anayetajwa katika Biblia Takatifu kitabu cha Mithali 8:1-36.

Ewe mtu unayetetea na kupigania haki mahali popote, katika taasisi ye yote na katika mazingira ye yote! Usikatishwe tamaa unapoona sauti ulizozitegemea zikinyamaza; na wala usiogope kuona uovu ukijiimarisha zaidi katika jamii. Haki hahitaji umati wa watu katika kushinda mapambano na wala hahitaji jeshi ili kuwanyamazisha madui zake! Yeye Haki ni Wakati! Wakati wake ukifika, Haki hupita katikati ya matusi, kejeli, dharau, watesi, majeshi na umma wa watu na kisha kuanza kuhesabu mateka na kuitweka bendera ya ushindi! Wakati wa Haki ukifika, hata wale waliomtweza, waliopambana katika kumtusi, waliowaua na kuwanyamazisha watetezi wa Haki; wote kwa pamoja watapaza sauti zao kumshangilia Haki! Haki hana dini ingawa anawatumia watu wa dini na wasio wa dini katika kutangaza uwepo wake!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki
We shall overcome
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Maaskofu wa ukweli hao sio wachumia dini(wajasilia dini) kama yule aliyecheza video ya ngono na muumini wake
 
Huyu Askofu amejikana na Kuamua kumfuata Kristo kikwelikweli,maana ya kujikana Ni kuwa tayari kufa au kudhalilishwa.
Tofauti na wale Maaskofu walioamua kuipenda Dunia na kuwaacha kondoo wakiteseka.

Na huyu sasa ndiye anayestahili kuombewa kwa Mungu wetu aliye hai! badala ya wale wafilisti na ambao mikono yao imetapakaa damu za wakosoaji wao.
 
The arc of the moral universe is long but it bends toward justice -Rev Martin Luther King
 
Hii haki ndo hekima yenyewe aliyoomba mfalme suleiman..
 
Back
Top Bottom