Ujumbe kwa madereva gari za serikali, mtatumaliza huku mabarabarani

Ujumbe kwa madereva gari za serikali, mtatumaliza huku mabarabarani

Acheni tuu kuna siku nimepanda tunatoka kumsindikiza mwenye anabebwa humo airport...wakati tunarudi karibia roho initoke aisee cha kushangaza wkt tunaenda wala mwendo haukua kihivyo sijui huwa anacontroliwa sasa kurudi lol lol...hawana akili kabisa...na misifa mingiiii....
 
Haya magari ya serikali kwakweli yanakera sana huko barabarani. kwanza madereva wake wanaendesha kwa fujo, wanahatarisha usalama wa watumiaji wengine wa barabara, hawafwati alama na taa za barabarani, wanapita upande wowote wa barabara, wanapita kwenye njia za mwendo kasi, wanapaki sehemu yoyote wanayojisikia. Alafu Traffic police wanawaangalia tu.

ukiwachomekea wanakuletea ubabe. Kuna mmoja wa gari la jeshi alinifanyia faulo afrikana pale, nikamvizia nikamchomekea moja kubwa pale kunduchi mmbuyuni, akafunga breki kwa nguvu, tairi zikalia pale, almanusura agonge watu, akashuka akataka nishuke kwenye gari, nikakataa, nikawa nasubiri aje mlangoni kwangu, nimpe kubwa moja alafu nikajisalimishe polisi pale mtongani, yani sikuiyo nilikuwa tayari kwa lolote. Bahati alishtuka akarudi kwenye vieite lake jeupe akasepa. We mjeda kama upo humu unasoma hapa ujue una bahati sana, siku ile nlikua naondoka na wewe! Pimbi we! [emoji3][emoji3]



View: https://m.youtube.com/watch?v=ukznXQ3MgN0&pp=ygUUQmxvb2R5IGJhc3RhcmQgYml0Y2g%3D
 
Tatizo linaanzia boss anaishi makazi Ununio, Mbewe alafu Dere anakaa Kisalawe Pugu mchafu koga, Kisha gari lilale Ofisi kuu what do you expect? Wapewe nyumba karibu na mabiss wao at most around 5Km distance radius. Gari ilale kwenye office ya serikali iliyo karibu na Dere.
 
Hawa watu na hii tabia vyote kwa pamoja ni sikio la kufa halisikii tena dawa..labda mpk siku mwendokasi wao uondoke na baadhi ya roho zao ndo wataelewa
 
Back
Top Bottom