Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Niliposikia Kenya na Tanzania wamefikia muafaka kuhusu kusafiri kwa ndege kati ya Dar es Salaam na Nairobi, nilidhani kwamba makubaliano haya yangehusu pia usafiri wa shuttle kati ya Arusha na Namanga. Kufika Arusha naambiwa hakuna kitu cha namna hiyo, bado wanaoruhusiwa kuvuka mpaka pale Namanga ni madereva wa malori ya mizigo tu.
Nimejiuliza sana kuhusu huu ubaguzi wa wazi kwa watu wa kipato cha chini. Hivi ina maana watu wenye uwezo wa kusafiri kwa ndege hao ndio wasio na Corona, na sisi wa daraja la barabara tunaonwa tutaeneza Corona?
Namsihi Waziri wa Mambo ya Nje Prof Kabudi aweke wazi hili na Wakenya. Ikiwa Kenya wameruhusu usafiri wa ndege kati ya Nairobi na Dar es Salaam, basi haina maana kuendelea kuzuia usafiri wa barabara kati ya Tanzania na Kenya. Tanzania haina ubaguzi kwa watu wake kuliungana na kipato chao, na Corona pia haijali unasafiri kwa ndege au shuttle.