Ujumbe kwa TFF na Uwanja wa CCM Kirumba

Ujumbe kwa TFF na Uwanja wa CCM Kirumba

Governor of Bettors-GB

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2013
Posts
10,568
Reaction score
9,710
Kwanza nawapongeza sana TFF kwa kuamua mechi kuchezwa mwanza.
Pia napongeza sana AZAM TV kwa kutuletea mechi hiyo Live.

BALL BOYS na idadi ya mipira:
Hili tatizo
Nikiangalia ni kwamba mpira ukitoka nje unachukua muda mrefu sana kuwa kurudishwa uwanjani.
Na tatizo lipo wazi ni kwamba Ball boys ukiwaangalia wote hawana mipira mkononi.Kwa tafsiri hiyo ni kwamba wanasubiria mpira utoke ndio waukimbize waurejeshe uwanjani.

Hili siwalaumu TFF ila ni wasimamizi wa Mkoa kuanzia uwanja hadi chama cha mchezo cha mkoa.
Maana TFF sio kwamba isimamie watu kama watoto wadogo hadi kwenye vitu kama hivi.
Kwa ufupi uwanjani mipira ya urejeshwaji uwanjani hakuna.

La pili ni kwamba ball boys hawakuwa trained,yaani wameokotwa tu,ili mradi wanajua kurejesha mpira uwanjani.
Nimeona mmoja yeye mpira wa kuweka kwenye goli,yaani karibu ya goli kwa mbavuni iwe rahisi kipa kuuona,yeye akaweka,nyuma ya goli.
Ningeomba wajifunze jinsi ball boys wa Mapinzuzi Cup walivyofanyakazi kwa umahiri wa hali ya juu.Na hata mechi za uwanja wa Taifa na Azam Complex huwa wamejipanga vizuri.

Kila sekunde inayopotea kwenye mchi kwa mpira kuwa nje ile ni mali.

Magari Kujaa uwanjani
Hili tatizo limekuwa ni mazoea kwa viwanja vyetu.
Eneo la running way katika uwanja ule ni ndogo sana na hata kama ingekuwepo.Huwezi kuweka gari ndani ya uwanja wa mpira.
Hii ni mechi ya Kimataifa,na inatizamwa sehem kubwa duniani.
Inasikitisha kwamba kiongozi mkuu wa TFF na team yako ya uongozi mnashuhudia suala hili.
Sasa sipati picha kwamba FIFA nao wanaangali hali hii,sijui inakuwaje wanavyotuelewa.

Ningeomba tubadilike,na yote hayo ni uongozi wa Uwanja wa CCM kirumba.
Viongozi wengi wa viwanja hivi ni wa analogia,wazamani kweli na mentality zao ni zile zile za kuruhusu hadi muuza mahindi aingie nayo uwanja na jiko lake.
Sasa naomba uongozi wote ubadilike na usifanye kazi kimazoea
 
Ujuaji mwingi na bila shule na kupeana uongozi bila tahaluma ndo sababu, kama mkurugenzi wa uwanja huo angekuwa na shule na training ya kutosha asingeruhusu haya ila kuchaguliwa kishkaji kwa kuangalia ulaji ndo tatizo,
NB:TFF, CLUB za YANGA na SIMBA wote hawa wapuuzi wanafanya mambo kwa maslai yao mpira wa Tanzania hauwezi kuendelea kwa sababu izi mana TFF wanapata pesa kwa team mbili tu SIMBA na YANGA ndo maana macho yao yote ni uko wanasahau team zingine kwa kuwa haziingizi mapato, hawa jamaa hawasheria madhubuti za kukuza soka hawana njia mbadala wakuongeza wazamini
 
uwanja mdogo wautanue iwe mt 120 @ 90 hapo utapendeza utakuwa wa kimataifa
 
Uwanja wa CCM Kirumba hauna Mkurugenzi bali una Meneja ambaye ni John Tegete.

John Tegete ni kocha mkuu wa timu ya Toto Afrika inayoshiki ligi daraja la kwanza.

Siku Taifa Stars "maboresho" ilipocheza CCM Kirumba, John Tegete alikua Kilimanjaro akiiongoza Toto katika mechi yao na Panone FC.

Mkuu Zanzibar Spices nadhani sasa unaweza ng'amua kwanini mambo siku hiyo yalikuwa shagalabagala [ovyo ovyo].. na nadhani yataendelea kua hivyo kwasababu msimamizi mkuu wa uwanja kila siku yupo mikoani akiipigania timu yake ipande ligi kuu.

cc Mphamvu Makoye Matale mtoto wa maskini Deo Corleone wakimataifa
 
Last edited by a moderator:

Sembo hii kweli kali,hapa umenifumbua macho.
Yaani Kiongozi wa Team ndio anaongoza uwanja.
Na Mechi kubwa kama ile,yeye hata uwanjani hayupo.Na kwa Tafsiri hiyo ni kwamba kama Toto ikipanda Daraja basi kila siku atakuwa safarini.
Hapa nadhani kuna haja ya kuajiri Menega alie huru na aise na uongozi kwenye Team.
Sasa kama team yake inataka kuhujum uwanja si rahisi tu?
 
Jamali Malinzi najua huwa anapita humu na hii hoja kaiona na ni hodari sana kujibu hoja.
Binafsi najua bado yupo kwenye majukum ya kuweka sawa madudu aliyoytakuta yakifanywa kwa mazoea.
Ila sie tunampa taarifa hizi kwa mapenzi yetu kwa Soka la nchi hii na kwa imani kwake kwamba anauwezo huo.Na pia tunatambua kwamba anamuda mfupi sana madarakani.
Ila hili tunampa muda kidogo ili aje atujibu kwa kina.
lakini namuomba akija atuambie lini Mzee Tegete ataachia uongozi wa uwanja kulingana na majukum yake ya team yake ya Toto ili tupate meneja huru wa uwanja.La sivyo tutashuhudia madudu mengi sana siku zijazo.
Chukulia mfano Uwanja mkubwa kama ule hauna Mkurugenzi,kwa tafsiri hiyo Meneja mzee Tegete ndio anavaa majuku yote.
Sasa kama Mzee tegete ni kiongozi Toto Africa na wkati huo ni Mkuu wa Uwanja huo,je zikipanda team mbili ligi kuu kutoka mkoa huo je siu ya DABI ya mecho za mkoa mmoja hali inakuwa,ukizingatia ushirikina ndio zetu.Na ule ni uwanja wa Serikali na team zote lazima ziutumie.
Ni Sawa na kusema kwamba Nyange Kaburu awe Meneja wa uwanja wa Taifa,hapo sipati picha.
Kwa ufupi TFF kama hamjamtoa basi subirini madudu zaidi,na sie sote mashuhuda na zama hizi mjue sio zileeee,AZAM TV inarusha kila nyago.
 
Sembo hii kweli kali,hapa umenifumbua macho.
Yaani Kiongozi wa Team ndio anaongoza uwanja.
Na Mechi kubwa kama ile,yeye hata uwanjani hayupo.Na kwa Tafsiri hiyo ni kwamba kama Toto ikipanda Daraja basi kila siku atakuwa safarini.
Hapa nadhani kuna haja ya kuajiri Menega alie huru na aise na uongozi kwenye Team.
Sasa kama team yake inataka kuhujum uwanja si rahisi tu?

Kweli Mkuu, inatakiwa tuepuke viongozi wetu kua na majukumu zaidi ya moja. Mf. umeamua kua kocha, umeneja wa uwanja mwachie mwingine.. n.k
 
Sembo hii kweli kali,hapa umenifumbua macho.
Yaani Kiongozi wa Team ndio anaongoza uwanja.
Na Mechi kubwa kama ile,yeye hata uwanjani hayupo.Na kwa Tafsiri hiyo ni kwamba kama Toto ikipanda Daraja basi kila siku atakuwa safarini.
Hapa nadhani kuna haja ya kuajiri Menega alie huru na aise na uongozi kwenye Team.
Sasa kama team yake inataka kuhujum uwanja si rahisi tu?
Zanzibar Spices, soka letu limeamili mfumo uliopo kwenye siasa zetu. Kama unavyoona mtu ni mbunge, waziri, mjumbe wa kamati ya bunge na wakati huo huo ni mjumbe wa bodi wa shirika la umma, ni baba wa familia, ni mume wa wake wawili na mchepuko wa wengine watatu.

KAtika mazingira kama haya tusitegemee ufanisi.

TFF kwao ni ngumu kusimamia viwanja vya mikoani endapo ule wao wa KArume waliojengewa na FIFA unawashinda.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom