Ujumbe kwa Waziri wa Madini, Mh. Anthony mavunde kutokana na mkutano na wanahabari leo

Ujumbe kwa Waziri wa Madini, Mh. Anthony mavunde kutokana na mkutano na wanahabari leo

TrueVoter

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2008
Posts
4,376
Reaction score
5,500
Ndugu Waziri Mavunde,
Salaam..

Nimefuatilia mkutano wako na wanahabari, najaribu kuweka yatokanayo..

1. Itafaa sana wakati mwingine kwa mikutano km hii iandaliwe kwa staili ya hybrid kuongeza ushiriki na pengine uwezekano wa kupata michango bora zaidi, km kweli mna lengo la kuongeza tija.

2. Stamico kazi inayowastahili kufanya kwenye sekta ya madini ni kuchimba makaa ya mawe au gesi tu..na kufua nishati kuwauzia tanesco, huko unakowaelekeza si sahihi mtaingia kwenye ufisadi muda si mrefu! Na hawana huo uwezo kifedha, ujuzi na uzoefu kuwepo kwenye kila aina ya madini hasa dhahabu, almasi, shaba, nk..achia sekta binafsi ichimbe dhahabu na madini mengine yote, usihadaike na hayo mafanikio unasema wameyapata..they r just bubbles!

3. Hadi sasa hakuna uhakika wa aina ya madini yaliyopo chini ya ardhi ya Tanzania, hii ni kwa sababu hakuna teknolojia stahiki kubaini madini hayo..badala ya kujenga hilo jengo ulilosema Dodoma, tafuta fedha mrushe satelaiti kusaidia utafutaji, ukadiriaji na uchimbaji madini, hili lilitakiwa liwe limefanyika juzi, bado mnarudia kufanya mambo mepesi mepesi kwa nini..? sayansi ya kupima udongo, madini, maji na rasilimali nyingine chini ya ardhi inahitaji teknolojia ya satelaiti na si hizi ramli mnazofanya!

4. Fanya mageuzi kwenye umiliki uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya madini, stamico hawawezi kuwa wabia..watafanya mambo mangapi?? Kwanini hamtaki kuruhusu mifuko ya hifadhi ya jamii, mifuko ya uwekezaji km UTT, vyama vya kitaaluma nk kuwa wabia kwenye uchimbaji mkubwa wa madini..? kuna shida gani..kila kitu stamico, nani hajui historia ya stamico, sasa hivi wamekuwa malaika..?

5. Nilitarajia mmefanyia kazi kuwa na mwelekeo wa uchimbaji madini kwa kuandaa ratiba ya uchimbaji kulingana na uwezo wa usimamizi na mahitaji ya nchi, huwezi ukawa na nchi kila mahali inachimbwa madini..dhahabu, almasi, tanzanite, shaba, graphite, coal, chuma, gesi nk nk na leo mnataja kutaka kuanza uchimbaji wa uranium, hivi nchi hii inakwisha kesho..? au hii generation ndio ya mwisho..? kwa nini kusiwe na mpango kuchagua baadhi ya madini na maeneo na kuchimba kwa kufuata ratiba..? mawazo na fikra za kutaka kuchimba madini yote yanayopatikana kwa wakati mmoja ni fikra za kimaskini kabisa na mufilisi! Achaneni na habari ya uranium kwa sasa! Chagueni angalau aina 5 au 6 za madini ya kuchimba kwa sasa kwa maeneo baadhi ndani ya miaka 10 inatosha, AKIBA HAIOZI!

6. Sijawahi kukubali kipaumbele cha tume ya madini ni kukusanya maduhuli..HAPANA! tume ni wasimamizi kugawa maeneo kwa kuzingatia uendelevu na mahitaji ya nchi sasa na badae..kwa mfano unawezaje kumpa kampuni ya wageni hasa wachina eneo la km za mraba 500 wachimbe ceramics, hivi mahitaji ya nchi ni ceramics peke yake..? vipi kama kuna madini mengine ndani ya eneo hilo..? vipi mahitaji ya viumbe hai..? si sahihi kabisa kuendelea kutoa umiliki maeneo makubwa kiasi hicho tena kwa wageni sababu tu eti wanalipia leseni..Hapana! badilisheni huo mtizamo..kuwe na ukomo kwa mgeni kupewa eneo la utafiti wa madini na kuchimba..nenda kwao china km utapewa hata sentimita moja!

7. Umetaja kutajengwa viwanda vingi Dodoma kwa umeme upi? Nini tatizo kuanza mradi wa bomba la gesi kuja Dodoma? Hivi unapopewa kitu huwa ni kwa ajili uwape wengine watumie au utumie wewe kwanza? Mnasubiri Uganda waanze mradi wa bomba la gesi kwenda Uganda au Kenya na nyinyi ndio mzinduke kuwa gesi inahitajika Dodoma..? Ni mambo ya kushangaza na kukera tpdc kuweka attention kutafuta mafuta igunga na kukataa kubuni mradi wa kuleta gesi Dodoma..ni mwehu tu anaweza kudhani ni sawa kwake kumwachia ndege mmoja aliye nae mkononi akaanza kukimbiza wawili porini!

8. Tengeneza kanuni ya unufaikaji uchimbaji madini kwa kila aina ya madini, sambamba na uchangiaji wake kwenye uchumi..kwamba km makadirio ya mchango wa sekta ya madini kwenye uchumi ni asilimia 20 kwa mwaka, tuambie kulingana na uwezo, upatikanaji na urahisi katika kuchimba madini dhahabu itachangia kiasi kadhaa, almasi pia, tanzanite, nk kwa kutaja thamani ya kila aina ya madini yatakayouzwa, mfano kutachibwa makaa ya mawe tani 10,000 kwa mwaka zenye thamani ya TZS. 1.0 billion kwa madini yote, mambo ya kusema jumla jumla si sawa kwa sasa.
9. Sikuridhika na majibu uliyotoa kwa muuliza swali kuhusu maeneo ya hifadhi kuruhusiwa shughuli za kuchimba madini..kwanza hakuna umbea km alivyosema sababu ni kweli serikali imeruhusu uchimbaji kwenye baadhi ya hifadhi, mfano hifadhi ya pori la kigosi wilaya ya bukombe. Acheni maeneo ya hifadhi kuendelea kuwa hifadhi, short like that sababu inaeleweka!
10. Mwisho, si sawa kusema leo siku ya kusema mafanikio tu bila kutaja changamoto, tuseme uko saw km unavyotaka wewe..tuambie lini siku ya kusema changamoto tujiandae!

Kila la heri!
 
Back
Top Bottom