Ujumbe maalum kwa maaskofu na waumini wa KKKT

Ujumbe maalum kwa maaskofu na waumini wa KKKT

diana chumbikino

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
428
Reaction score
368
Kwa muda mrefu nimekuwa katika shuhuda kwa watu, ndani na nje ya nchi kuhusu mwenendo wa kanisa letu, viongozi wetu katika kanisa na hata kuhubiri mambo ambayo kwayo, KKKT limelelewa miaka mingi iliyopita.

Sishangai mabadiliko ndani ya kanisa, ila mabadiliko yanapokiuka misingi ya dini, imani, maadili na mafundisho yapasa kuyakemea bila kupepesa macho.

Nimewahi kusema juu ya mwenendo wa mchungaji wangu Samwel Pallangyo ambaye kwa sasa anataka kulichafua kanisa kwa sababu anataka kuwa ‘Yuda’. Ameshawishi kongamano lifanyike tarehe 29/12/2019 na litashirikisha ndugu zake waliompa fedha.

Kanisa linapoamua kufanya biashara za namna hii, linaharibu taswira ya kanisa la kikristo kwa ujumla.

Baba Askofu Dkt. Shoo upo, kwa nini yeye afanye vikao vya siri vya kutaka mageuzi ndani ya kanisa na nchi bila maaskofu wote kufahamu jambo hili?

Je haridhishwi na mkutano mkuu wa kanisa au halmashauri kuu? Tunapokutana makumira na kuyajadili mambo yetu katika kanisa mbona huwa hayasemi ambayo moyo wake unayataka?

Uratibu wa mambo kwa njia za siri kulihusisha kanisa lenye uongozi je, si shambi hiyo?

Kwa ambao bado hamjashirikishwa, jiandaeni.

Analitumikia kanisa na anatumikia chama cha siasa kupitia kanisa. Analipwa fedha, anashawishi waumini mmoja mmoja.

Miongoni mwetu tunalazimishwa kwa sababu fulani fulani bila kujali kwamba kanisani wapo waumini wa vyama mbalimbali.

Anahimiza kufuata msimamo wa chama cha siasa ambacho katibu wake mkuu amemuagiza ahakikishe KKKT inaunga mkono baadhi ya mambo yao, kama sio yote.

Kwa waliozaliwa kabla yangu, siamini katika mtazamo huu. Kama Mungu alipanga jambo kutokea, litatokea. Binadamu kulazimisha mambo ni ishara mbaya hasa mbele ya madhababu.

John Mnyika anapoanza kutoa maelekezo ndani ya kanisa la KKKT tena kupitia mchungani ambaye yupo chini ya viongozi wakuu wa kanisa katika ngazi ya usharika, jimbo na dayosisi ni ishara kwamba tuna watu ambao wanaweza kulitumia kanisa kutuvuruga.

Hebu tukumbuke kikao chetu cha mwisho pale Makumira, Baba Askofu utanisaidia, maeneo ambayo wengi waliyapigia kelele ni migogoro ndani ya kanisa.

Bila kujadili athari zake, Samweli anaingia nadhiri ya kuyatumia madhabahu kwa ajili ya kutakasa fedha ambazo zitaletwa kanisani kwa kazi za kaisari. Mungu tumpe yake na kaisari tumpe yake.

Sisi tulio katika kanisa tuna wajibu wa kuomba amani, utulivu na mshikamano wakati wote. Migawanyiko si jadi yetu, oneni kazi tunayopata katika maeneo yenye migogoro katika kanisa letu la KKKT. Hata Mungu akishuka leo, anaweza kutuhukumu kweli kweli.

Madai ya kisiasa yakianza kuingia kanisani tutawagawa watu. Huwezi kuingia katika ibada ya tarehe 1/1/2020 na kusema “sasa tunatangaza rasmi kuwa tunataka tume huru ya uchaguzi”.

Kanisa lina vipaumbele vyake, na vyama vya kisiasa vina vipaumbele vyake. Tujikite katika dhamira za kiroho kuliko dhamira za kimwili.

Hata waraka tunaoshiriki kuuandaa kama kanisa, tunaweza jitia doa jekundu katika vazi la theluji. Tarehe 1/1/2020 uwe mwanzo mwema wa mwaka 2020 lakini endapo tutakubali kutumika, tutaharibu kanisa.

Nawasihi sana viongozi wetu wote katika ngazi mbalimbali: wakuu sharika zetu, majimbo, dayosisi, mkutano mkuu na halmashauri kuu hebu mwaka 2020 uwe mwaka wa mapatano ndani ya kanisa na sio migawanyiko.

Tutunze nadhiri katika kazi yetu ya kanisa ili neema za Mwenyezi Mungu zishuke kwetu na vizazi vyetu, sasa na hata milele.

Mungu awabariki!

Msharika mwenzenu, KKKT - Usharika wa Arusha Mjini.
 
Hakika tahadhari ni muhimu sana maana shetani ameamua kupitia makanisani kuiletea nchi yetu machafuko. Maaskofu wamegeukia matumbo yao na kusahau wito wao. Mfano kauli za huyu Askofu wa Dayosisi ya Karagwe na huyu wa mwanakondoo
mwam1.PNG

bag.PNG
 
PUMBAFU KABISA WEWE.
YAANI JOHN MNYIKA ATOE AMRI KWA KANISA LA KKKT? TUACHE SIASA MAKANISANI KWANI HAO CHADEMA HAWARUHUSIWI KABISA KUKANYAGA MAKANISANI KWETU?

HIVI VYAMA VYA SIASA VIPO KIKATIBA TUVIPENDE NA TUVIHESHIMU. KAMA HATUVITAKI TUMSHAURI MWENYEKITI WETU NA RAIS WETU AVIFUTE SIO KUVICHUKULIA KAMA MAADUI KIASI HIKI.

ACHENI KUPANDIKIZA CHUKI KWA HIYO MBOWE AU MNYIKA AKIJA KANISANIA HARUHUSIWI HATA KUSALIMIA ILA WA CCM WAKIJA WAPEWE TU MICROPHONE?

MBONA MAKONDA AKIJA KANISANI ANAOMBEA HADI WATU NA HAKUNA ALIYELALAMIKA???

NARUDIA TUACHE SIASA ZA KIPUMBAVU, CCM TUMEPEWA MADARAKA TUWALETEE WANANCHI MAENDELEO TUACHE VISINGIZIO.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom