Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
UJUMBE MAALUMU KWA VIJANA MNAOONA MAISHA MAGUMU!
Anaandika Robert Heriel!
Sipendi kusema mafanikio yangu ni yapi, na wengi watataka kuniuliza nina mafanikio gani mpaka niwe mshauri kwao. Sipendi kuyataja mafanikio yangu Kwa sababu hayatawasaidia Jambo lolote, lakini nitatoa Siri ndogo Sana ya kupata mafanikio katika maisha ambayo ukiijua hiyo umefanikiwa!
Vijana wengi wanalalamika hawana mitaji, wengine wanalalamika hawana connection ya kupata kazi. Wengine hawana kazi Wala kibarua.
Nataka kukuhakikishia, hata ukipewa mtaji wa mamilioni ya pesa kama huijui Siri hii kamwe huwezi fanya lolote na hizo pesa, hujaona baadhi ya watu wakifilisika licha ya kuwa na mitaji mikubwa, hujaona! Hujaona watu wenye kazi lakini kutwa kulalamika.
Niliwahi kuandika Makala Fulani humu kuwa; kabla ya kuyatafuta maisha mtafute Mungu wako Kwanza. Na Leo narudia tena kabla hujaanza mikakati yoyote Ile ni lazima umtafute Mungu wako. Super-natural power ni muhimu Sana katika kufanikiwa.
Asije akakudanganya Mtu yeyote, ati kuna mtu anayeweza kufanikiwa pasipo Mungu hakuna mtu wa hivyo hapa Duniani. Wanakudanganya hao.
Asilimia kubwa ya watu waliofanikiwa Duniani wanaamini katika miungu.
Nimekaa na watu wenye vipato vya juu kabisa, Nina marafiki zangu ambao ni Wazee Kama Baba zangu ambao ni matajiri mno WA level za kimataifa, wote wanaamini katika miungu.
Iwe miungu ya Dini za wageni au miungu ya kiutamaduni.
Vijana kuamini mungu sio kupoteza muda makanisani au misikitini, kuamini mungu wako ni kumheshimu, kumfanya namba moja, na kujua anataka ufanye nini.
Watu watakuambia ooh! Kuna Majambazi sijui wahuni wamefanikiwa na hawamuamini Mungu, sio kweli hakuna jambazi anayejielewa na aliyefanikiwa asiyemuabudu mungu, lazima awe na mungu iwe wa jadi au mungu wa wageni kutoka nchi za mbali.
Na hawa waliofanikiwa hawaoni aibu kutambulisha miungu yao, hata mama anaenda Kwa waganga WA kienyeji, utamsikia akijivunia Jambo hilo kuwa yeye kwake Hilo sio shida. Kuwa na chale kwake sio aibu.
Ili ufanikiwe itakupasa ufanye mambo mawili tuu, nayo ni:
1. Umheshimu mungu wako bila kujali wengine wanasema nini juu yake na juu yako.
2. Uheshimu watu.
Hilo la Kwanza ni muhimu kuliko.
Lakini Vijana wa sasa Kwa kujawa na ujinga utashangaa;
1. Kanisani haendi na hamuamini mungu wa Kanisa licha ya yeye kuwa Mkristo.
2. Msikitini haendi na hamuamuni mungu WA msikitini licha ya kuwa Muislam
3. Kwa mganga haendi licha ya kuwa anaamini Sana Uchawi.
Embu niambie kijana wa namna hii anatokaje kimaisha?
Hana nguvu iliyonyuma yake inayomuongoza na kumlinda. Unafikiri atafanikiwaje?
Kazi kufuata mkumbo tuu!
Usidanganywe na Wale wanaosema Wazungu sijui hawaamini katika mungu HAO ni waongo, hawawajui vizuri hao Wazungu, wala hawawajui hao waarabu au wachina. Na kitu kimoja cha uhakika ni kuwa Mzungu hawezi kutaka umjue.
Siri nimewapa, usifanye lolote bila kumshirikisha mungu wako, kumtanguliza Mungu Kwa Jambo lolote lile ni Dalili ya kumtegemea, kumheshimu, na kumfanya yeye ndiye the top.
Sio ufanye alafu ndio umshirikishe mambo yakikuendea kombo.
Kanuni inasema; ukimfanya Mungu wako WA Kwanza, naye atakufanya wa Kwanza, ukimuweka namba mbili naye atakufanya vivyohivyo.
Uwe na Ratiba, utaratibu na kanuni WA namna utakavyokuwa unakutana na mungu wako.
Sio ukutane naye kiholela Kama wahuni wawili wenye mazoea ya kipuuzi.
Jiwekee Ratiba iwe ya Kula baada ya masaa kadhaa au siku kadhaa utakuwa unakutana na mungu wako.
Katika mwaka ujue kabisa mwezi Fulani tarehe Fulani ni siku maalumu ya kumtolea Sadaka Mungu wako iwe Kwa kuwapa wahitaji msaada, iwe Kwa kutoa harambee kwenye makanisa au misikiti n.k.
Uwapo kwenye maombi kuwe na mazingira maalumu. Na yawe katika Usafi na adabu ya Hali ya juu
Sio unaomba mungu mahali pachafu pananuka nawe hata hujali.
Kama utaweza uwe na vazi maalumu la ibada, Kwa ajili ya kuwasiliana na mungu wako. Haijalishi na munhu yupi lakini ikiwa unaamini ndiye mungu wako basi Mheshimu.
Utakase moyo wako, kisha mwili alafu baadaye iweke wakfu nyumba yako(izindike), sio unajenga nyumba alafu unaingia Kama vile pango au kiota cha Ndege, mahali pako pa kazi iwe ni Ofisi binafsi au umeajiriwa, patakase kila ukifika, kabla hujaanza kazi au kumhudumia mteja yeyote omba mungu wako, itakase ofisi yako, na iombee ulinzi.
Hivyo utakuwa umemheshimu Mungu, naye Mungu atakuheshimisha lakini baada ya hapo kanuni ya pili inasema waheshimu watu.
Ukishaheshimiwa na Mungu kuna Ile unaona watu wanakushobokea, wateja wanamiminika, usianze kuleta kiburi Bali waheshimu na wape lugha nzuri.
Hakikisha wateja wako wakifika ofisini mwako waone ishara au Dalili ya uwepo wa mungu wako, Kama ni Muislam waone Quran au zile zana za kiislam Kama Tasbihi sijui kama nimepatia, Kama ni Mkatoliki waone Biblia ya Rozali, au msalaba WA Yesu, au kama ni mtu wa utamaduni waone vitu vya utamaduni Kama chungu, au tunguli, au Jambo lolote linalotambulisha mungu wako.
Usiwe na hofu kuwa wateja ambao sio waamini wa mungu wako wataondoka, sio kweli, anayeleta wateja sio wewe, wala sio Duka lako, bali ni mungu unayemuamini.
Kwa Sisi wafanyabiashara tunajua kuwa hatujui Leo ni mteja gani atakuja, tunaishi Kwa Imani tuu kuwa wateja watakuja lakini hatujui watakuwa kina Nani. Ndio maana biashara bila mungu haiwezekaniki Kabisa, Kwa sababu kinacholeta wateja ni miungu Ile tunayoiamini.
Achana na hao wanaokuambia biashara ni Sayansi sijui elimu.
Hakuna mfanyabiashara yeyote utakayemsikia akisema Maneno hayo, isipokuwa watu wasiofanya biashara.
Ukimsikia mtu anakuambia hivyo, mwambie nikupe mtaji wa shilingi ngapi, na muda gani ili ufanye biashara na kuniletea faida pasipo kutegemea miungu! Mwambie aweke vitu vyake rehani alafu mpe mtaji uone Kama atakubali.
Sio ajabu ukashangaa wasomi wengi waliosomea biashara na uchumi wakishindwa vibaya kwenye biashara Kwa Sababu wanajua umbo la nje tuu la biashara, umbo la ndani hawalijui.
Au wasomi wa kilimo nao ni hivyohivyo tuu.
Fanya hivyo siku zako zote za maisha yako.
Usipofanikiwa niite Mimi zumbukuku, mpuuzi na muongo.
Nimemaliza! SABATO NJEMA!
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam