Ujumbe mzito toka kwa Ansbert Ngurumo kwa upinzania, sikilizeni na tafakari

Ujumbe mzito toka kwa Ansbert Ngurumo kwa upinzania, sikilizeni na tafakari

Chadema mkiona kuna mtu anataka kukivuruga chama fukuzeni mapema kabla hajawa kirusi ,kaondoka Mchungaji feki Msigwa mambo yapo fresh ,kaondoka Dr Slaa mambo bado mswano ,chama siyo mtu.
 
Ni kweli kwa 100%

Labda wewe huenda ndio haujui Ukweli kuhusu suala hili.
Kumbuka: Hata huyo Augustino Lyatonga Mrema naye pia hakuwa Mpinzani halisi, bali alikuwa Mamluki aliyepandikizwa huko Upinzani akitokea kwa wale jamaa 'wavaa Kaunda suti.' Tena Mrema alikuwa mmoja wa Wakufunzi wao mahiri huko kwa wavaa kaunda suti.
That's why utakumbuka kwamba Mrema ndiye alikuwa mtu/Kiongozi mkubwa zaidi wa kwanza kabisa aliyefanikiwa sana kuuvuruga Upinzani hapa Tanzania.
Niliwahi wasikia mrema na marando kwenye moja ya vipindi vya kitimoto enzi hizo wakitambiana rank zao ndani ya idara bya usalama, marando akidai alikuwa juu ya mrema kwenye idara

Ugomvi wao ulikuwa utumishi wa idara ya usalama ndani ya chama ndo ulikiuwa chama

Mfumo Wetu wa chama kimoja ndani ya vyama vingi na mabaki ya siasa za kijamaa bado unatutesa sana watz
 
Nyerere aliharibu hii nchi
Kiasi kwamba Leo akina samia na mchengerwa wanatumia mifumo hiyo hiyo kutuadhibu watz

Tumejaribubu kuachana na hii mifumo inashindikana
Nani atatuokoa

Mfano katiba ingeruhusu mgombea binafsi kusingekuwa na mgogoro kwenye vyama
 
Salama ya cdm ni Mbowe kufikia hatima ya uenyekiti wake. Iwapo Mbowe atashupaza shingo, hakuna namna cdm itaendelea kuwa taasisi imara.
Mbowe anaona kuliko aachie Uenyekiti afadhali chama kipasuke, yeye anaona hana cha kupoteza, na hii ndio hasara ya chama kumilikiwa na mtu mmoja
 
Salama ya cdm ni Mbowe kufikia hatima ya uenyekiti wake. Iwapo Mbowe atashupaza shingo, hakuna namna cdm itaendelea kuwa taasisi imara.
Kwa hali ilivyo sasa mbowe astasfu uenyekiti awapishe wengine waongoze chama

Kuna mtu anasema eti anahofia kuondoka kwa kuwa anakidai chama hela nyingi.

Mi nasema asamehe tu hayo madeni
Ndo utakuwa michango wake kwa chama
 
Ulitaka uwe wewe au?
Ni kweli ana mchango mzuri. "Aliyesimama aangalie asianguke" au asiwe chanzo cha wengine kuonekana wameanguka. Shida ni kwamba watu ambao always wako kwenye move (wanafanya hiki au kile) hawana nafasi ya kutafakari na kuona kama wanakwenda wanavyotakiwa kwenda au kuna sehemu inabidi waboreshe ili waweze kuwa effective zaidi. Watu wakikosa fursa ya kutafakari wanaweza kujikuta wameshaacha njia. Jana nilikuwa nasikiliza wachangiaji 'space' na niliweza kuhisi hiki anachokisema huyu mkuu. Experience aliyoipitia Tundu Lissu inampa ujasiri wa kusema mambo mbalimbali ndani na nje ya chama chake. Inabidi aangalie audience yake inapokeaje uwasilishaji wake. Ni wazi watu wengi (ndani na nje ya chama) wanaweza kuwa na imani naye. Ni yeye sasa kujua ni kwa jinsi gani anaweza kutumia fursa hii kujenga chama chake vs kujijenga mwenyewe na kuleta ufa kwenye chama. Mfano, uwasilishaji wake wa tuhuma za rushwa ndani ya chama angeweza kuufanya kwa namna bora zaidi kuliko alivyofanya. Viongozi wa Chadema inabidi wajifunze kuwa "prudent": 'acting with or showing care and thought for the future'.
 
Umemsikiliza Ngurumo? msikilize vema....... Lisu haezi kutengwa, awe macho na hao wanaompigia makofi kumtaka eti aanzishe chama chake kama mrema....msikilize ngurumo
.Mimi kama muumini wa siasa za upinzani Nimtake. Lissu awe mtulivu afuate katiba ya chama chake, asitoe matamko hovyo, tunamkubali, ni mkweli na tutamsupport
 
Mkuu retired lakini wakati mwingine tuitizame chanya minyukano, mikanganyiko na migongano kama ndo demokrasia tunayoihubiri Kila siku.

Lakini huenda ni wakati sasa Kwa jambo jipya la manufaa kwa upinzani na nchi linaenda kuzaliwa litakalo weka muelekeo mpya wa kisiasa

Nimekuwa nikiwashangaa upande wa ccm kutokuona migogoro ni dalili ya kufa kisiasa

Ukimtoa luhanga mpina simuoni mwanaccm aliye huru na mwenye mawazo huru wote ni makondoo

Si bunge si mahakama wote kimya huu utiii si afya hata kidogo

Lakini pia mkuu retired' katiba mbovu ya nchi ambayo hairuhusu mwanasiasa huru au mgombea binafsi ni kikwazo

Labda katiba ingeruhusu mgombea binafsi tungekuwa na wanasiasa huru wasiofungwa na vyama vyaonkama lissu na Mpina
 
Back
Top Bottom