Ujumbe mzito wa Majizzo kwa Kitenge, Hando, Bdozen na Oscar Oscar

Ujumbe mzito wa Majizzo kwa Kitenge, Hando, Bdozen na Oscar Oscar

Half american

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
38,283
Reaction score
97,793
Ilikuwa wakati mzuri sana kufanya kazi na ndugu zangu Maulid Kitenge, Gerald Hando, B Dozen na Oscar Oscar.

Nitaendelea kuwashukuru na kuwaheshimu sana kwa mchango walioweka hapa #EFMnaTVE. Nawatakia mafanikio katika ajira zao mpya, mafanikio yao ni mafanikio ya tasnia na hiyo ni furaha yangu.

All the best ndugu zangu🙏🏻

#MuzikiUnaongea
Screenshot_20230423-153051_Instagram Lite.jpg
 
Hakuna media tanzania ingemuunga mkono Gerald kwa maoni yake yale dhidi ya serikali kwani kamwe hata kule Wasafi hawezi kuyatoa ! Uwezi ku survive kwenye business ukapambana na serikali ukashinda!
Kwa Tanzania wala haishangazi. Kwani Katiba ya nchi inampa umungu mtu na umiliki wa nchi Rais kama nyumba ya urithi wa baba yake.

By the way Aliyeyaongea hayo ni mwenye kituo au mfanyakazi tu!? Mwenye kituo angesema tu hayo ni maoni binafsi ya mtangazaji shida ingekuwa wapi hadi kuifanya kuwa big deal kiasi kile!? Au ni kweli kuwa mtaji wake inawezekana ni wa magumashi
 
Inawezekana walishinikizwa. Ila kama ni kujipendekeza kwa serikali walikosea sana maana yalikuwa maoni yake binafsi. Sasa mambo ya kudhalilishana eti tumeshamchukulia hatua kama kituo haikuwa poa aisee.

Kwanza nahisi hata kurudi efm alirudi basi tu kwa sababu kwenye bio yake instagram alifuta ktatikati ya ile ban kwamba anafanya kazi efm.
 
Kwenye ujumbe wake kuna uzi mwembamba sana kati ya maumivu na hasira kwambaaaaaali....
Huwezi kuondokewa na Magwiji Wanne ( 4 ) Kitenge ( Michezo ), Hando ( Mijadala ), Bdozen ( Muziki ) na Oscar ( Uchambuzi ) halafu ukaonyesha hujaumizwa na Kinafiki unatoa Sifa na kuwatakia Kila la Kheri huko Waendako.

Mwambieni Majizzo wenu Tajiri Diamond Platnumz wa Wasafi Media anajiandaa Kummaliza kwa Dada Bingwa wa Simulizi katika Redio za Tanzania Veronica Frank na ni Suala la muda tu.
 
Back
Top Bottom