Ujumbe wa "Kwa hisani ya watu wa Marekani" Lengo lake ni nini haswa?

Hatulaumu misaada ila anayesaidia ndiye anayekuwa na kauli kubwa kwakuwa ndiye mwenye uwezo hivyo kwakuwa wewe ni mnyonge huwezi kukataa asiandike maandishi yanayomtambulisha kuwa ni yeye aliyekusaidia. Asipoandika unaweza ukaanza kujigamba kuwa ni nguvu zako kumbe ni msaada. Kuna mtu nilimsikia akisema anaomba mkopo na pesa za kulipa anazo. Sasa kama unapesa za kulipa unaombaje mkopo? Si utumie hizo pesa ulizonazo?
 
Eti utakuta ujumbe wa kuhamasisha kunawa mikono na sabuni umeletwa kwa hisani ya watu wa marekani
 
ili mijitu kama meko isije ikawadanganya wananchi kuwa ndio imeweka pesa pale. meko alikuwa muongo sana na mpotoshaji.. na kwa afrika hii mijitu ipo mingi sana
 

Miradi wanayoifadhili inamalengo mara nyingi ya kujijengea sifa kwamba ni watu wema.

Wamerekani ni wakatili na wanafiki sana ila wanajua kucheza na saikolojia ya umma. Wanakupiga kama walivyompiga Sadam kule Iraq na kuangamiza miundombinu za uchumi alafu ili kuwapooza wananchi wanajifanya kukusaidia kwa kuleta nguo, vyakula na hata huku wakiendelea kuibana serikali walioiweka madarakani kutoa kandarasi kubwa kubwa kama vile za ujenzi wa barabara, miundombinu ya umeme na mengine kama hayo kwa makampuni zao.

Wanaita, wanatengeneza janga ili waje kujifanya wanatoa msaada kumbe ni geresha.

Hakuna nchi dhulumati duniani kama Marekani.
 
Lengo usije baadae kutamba kuwa CCM ndio imefanya ivyo au Rais katoa fedha.
Ni RECOGNITION SIGNATURE
 
Conspiracy theories kama hizi kumbe bado watu wanaziongea!
Marekani sera yake ya nje iko wazi kuwa dunia ikiwa salama kiuchumi na kisiasa na wao watakuwa salama.
Huo mwingine ni utopolo tunawaachia wagonjwa wa Milembe waamini.
 
Kama hutaki maneno hayo, hicho choo cha 5M si ujenge mwenyewe..!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…