You post exemplifies that!Maneno matupu bila ushahidi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
You post exemplifies that!Maneno matupu bila ushahidi
Ninachojiuliza ni kwamba hapo zamani tulikuwa tunafanyaje?Mbona fedha za Global fund inatosha tu kumention "GLOBAL FUND" Fedha za World bank,IMF na ADB hazina hizibmbwembwe za ajabu ajabu?Nimewahi kufanya kazi na projects ambazo zimepata fedha kutoka kwa wafadhili mbalimbali mfano EU, NORAD etc Kabla hamjaanza implementation ni lazima mtengeneze kitu kinaitwa VISIBILITY PLAN, ambayo in short ni mpango wenu wa jinsi mtakavyotangaza au ku acknowledge kwa jamiii itakayonufaika na huo msaada fedha hiyo imetoka wapi. Visibility plan therefore will include kuweka logo ya mfadhili, Kama ni kwenye media lazima u mention source of funds etc.....
Hata dawa za kupunguza makali ya VVU ni kwa hisani ya watu Wa marekani....unaubavu Wa kukataa kauli?Habari za jioni wadau.
Naomba niweke wazi kuwa mimi napenda nchi kama nchi ijitegemee kwa asilimia mia moja lakini pia natambua jambo hili laweza kuchukua muda kutokana na historia ya Taifa na harakati za kidunia zilizokuwepo na zinazoendelea kutokea.
Naamini pia katika kufikia lengo la kimaendeleo bado ni muhimu kupata msaada kutoka kwa wenzetu ambao walitangulia kimaendeleo.
Naamini pia njia bora na ya kweli katika kufikia uhuru wa kiuchumi,kifikra na kimaamuzi ni kupitia jitihada za watanzania wenyewe.
UKAKASI
Nimekuwa nikisikia au kushuhudia matangazo mbalimbali haswa katika sekta ya afya ambayo yanapenda kusisitiza matumizi ya maneno haya...
"KWA HISANI YA WATU WA MAREKANI"
Kwa maoni yangu maneno haya ni ya kudhalilisha mno na sielewi mantiki ya kubandika maneno haya pindi mradi unapopata msaada wa kutoka marekani.
Wakati mwingine kamradi kadogo tu kama vile ujenzi wa choo cha shilingi milioni 5 uatakuta haya maneno yapo tu.
Naamini Tanzania inapokea misaada mingi kutoka nchi mbalimbali lakini sijashuhudia sana maneno dhalili namna hii.
Je nia ya msaada wa marekani haiwezi kufikiwa hadi maneno haya yaandikwe?
Je kuna sheria nchini Marekani inayolazimisha maneno haya yaandikwe?kama ipo ni sheria ipi?
Je kuna vipengele vyovyote katika mkataba wa ushirikiano kati yetu na marekani kinachotaka maneno hayo yaandikwe?
Je wananchi wa Marekani wanapoteza nini maneno hayo yasipoandikwa?
Je Serikali haiwezi kuyapiga marufuku matumizi ya maneno haya ...mbona zamani tulipewa misaada na hakukuwa na aina hii ya maneno ya kudhalilisha?
Karibuni kwa mjadala.
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
wabunge wengi ni ccm tena wazee, vijana ni wachache ambao ni akina kibajaj hapo unategemea nini?Je wabunge wetu wanakubaliana na msemo huu? hawawezi kusema neno juu ya hili?
Jinga lao ebu tutafasirie ..."kwa hisani ya watu Wa marekani " kwa kiingereza kwanza kisha tujadili maana wenye kiswahili ni sisi...sijui mnalalamika nini mabazazi nyieNi sharti linalolenga nini haswa?
Hilo nalitambua vyema na kama unakubaliana na mimi zamani tulipokea msaada kwa zaidi ya asilimia hizo ila sikuwahi kusikia maneno hayo ya kuudhi au kujijweza.Mleta thread, tambua kuwa budget yetu ni tegemezi kwa kwa karibu asilimia 60. miradi mingi nchini ni ya fedha za hao wahisani. Tena ni kwa niaka mingi ipo hivyo.
Niliwahi kuuliza the same question maana hawa jamaa huwa wakali sana wakati wanapokuja kutembelea miradi huko field.... Mfano wakikuta mme print T-shirt, kofia, even slides presentation without acknowledging aisee inakuwa bonge la issue. Program officer wa nchi moja (ambaye fortunately alikuwa mbongo mwenzetu) akasema ni madharti ya nchi zao na kila siku yanabadilika, eti pia ni njia ya kuhakikisha pesa inatumiwa as intended.Ninachojiuliza ni kwamba hapo zamani tulikuwa tunafanyaje?Mbona fedha za Global fund inatosha tu kumention "GLOBAL FUND" Fedha za World bank,IMF na ADB hazina hizibmbwembwe za ajabu ajabu?
Na sio kwa hisani ya wananchi wa mataifa flani?
Hiki
Sasa wewe mbona unawapinga wa Marekani wanapojitangaza? Umejuaje kama si lengo na halikubaliki?Walikuwa wanajitangaza kibiashara na hilo ni lengo linalokubalika na kueleweka.
Sio mbwembwe bali ni halisi!Je agizo la kuandika hivyo lilitoka kwa wananchi wa marekani au ni mbwembwe za watawala wa huko?
wapi papa msofe!, ndama mtoto wa ngombe! salum matelephone! hii ni pesa walikuwa wanawapa wanamusic
mimi nahisi chanzo cha maneno haya mabaya watakuwa ni wabongo wenzetu wenye hulka ya kunyenyekea hata pasipostahili.Nimewahi kupokea misaada kadhaa kutoka kwa wamarekani nadhani wanachohitaji ni recognition kimaandishi zaidi mfano ni kuwaandikia appreciation letter ambayo atarudi nayo kuionesha huko alipochangisha fedha ili kujustfy matumizi na kuombea mchango zaidi.Niliwahi kuuliza the same question maana hawa jamaa huwa wakali sana wakati wanapokuja kutembelea miradi huko field.... Mfano wakikuta mme print T-shirt, kofia, even slides presentation without acknowledging aisee inakuwa bonge la issue. Program officer wa nchi moja (ambaye fortunately alikuwa mbongo mwenzetu) akasema ni madharti ya nchi zao na kila siku yanabadilika, eti pia ni njia ya kuhakikisha pesa inatumiwa as intended.
Wangebakia kama zamani angetokea dikteta mmoja akitoa msaada wa watu wa marekani angesema msaada katoa yeye.kwa nini hatukubakia na mfumo wa zamani?
Na kwa nini tusirudie kwenye mfumo wa zamani?
Ina maana haya maandiko yanatumika ndani ya udongo wa marekani?Wangebakia kama zamani angetokea dikteta mmoja akitoa msaada wa watu wa marekani angesema msaada katoa yeye.
Hujawahi kuona kodi za watanzania zinapelekwa sehemu kufanya maendeleo lakini vinatokea vidudumtu vinasema "jiwe katoa hela"?
Wenzetu wamepiga hatua kukwepesha ubabe kama wa "sipangiwi, sijaribiwi"
Siku zote ombaomba akizidisha kuomba, mwombaji anaanza kumkejeli hadharanizamani fedha hizo zilikuwa zinatoka wapi?mbona hakukuwa na maneno haya?
NdioIna maana haya maandiko yanatumika ndani ya udongo wa marekani?
Kuna haja ya kuendelea kuwa na udhalilishaji huu ambao hapo nyuma haukuwepo?