Ujumbe wa "Kwa hisani ya watu wa Marekani" Lengo lake ni nini haswa?

Ujumbe wa "Kwa hisani ya watu wa Marekani" Lengo lake ni nini haswa?

Wanazuoni wetu na wanasaikolojia wetu wanaonaje juu ya hilo?
Na jee tuendelee kukubali uhuni huu?Je na sisi tunaeeza kuweka sharti juu ya andiko hili kulinda utu wetu?
Hamuwezi kubadilisha na hamko kwenye nafasi hiyo sababu anayetoa fedha ni mmarekani. Yeye ndio mwenye mamlaka na hiyo pesa, na mamlaka hayo yamesainiwa tiliwa sahihi na serikali yako.


Dawa ni moja tu, mpaka tutakapoweza kujitegemea ndio itawezekana.
 
kwa nini hatukubakia na mfumo wa zamani?
Na kwa nini tusirudie kwenye mfumo wa zamani?
Hatuwezi , why? Sababu wenye pesa ndio wameamua hivyo.
Na wao wanamatarajio kuona misaada yao inatumika vizuri.

And kubakia mfumo wa zamani, mfumo upi huo?
 
Hamuwezi kubadilisha na hamko kwenye nafasi hiyo sababu anayetoa fedha ni mmarekani. Yeye ndio mwenye mamlaka na hiyo pesa, na mamlaka hayo yamesainiwa tiliwa sahihi na serikali yako.


Dawa ni moja tu, mpaka tutakapoweza kujitegemea ndio itawezekana.
tukibadilisha itakuaje?unadhani haiwezekani kurejea hali ya awali kabla ya maandiko haya?
 
Miaka kadhaa ya nyuma hilo andiko halikuwepo ...why now na linalenga kuachieve nini?
Tatizo nini wenzetu wanapenda transparency sio kama Chadema ukiwaambia wekeni majina ya watu Na kiasi walichomchangia matibabu Lisu wanasepa.Wao wanaweka kibao kwa hisani ya watu wa Marekani alyechangia akienda aweza onyeshwa list nzima ya wachangiaji namba zao za simu walipo nk Chadema waambie waonyeshe hiyo list hata kama ulichangia hawakupi Na mwenye list ni mwenyekiti tu.Hakuna ulaya waweke tu hata wakijenga genge la kuuza nyanya la elfu nne.It is ok.
 
hiyo ndege iliandikwa kwa "hisani ya watu wa marekani" ???
Nope. According to msaada uliotolewa, pesa zimeandikwa kuwa zilitoka america.
Sasa hawawez kuandika kwenye ndege, ila waliandika kwenye makubaliano na ikulu ya tz. Wakati huo akiwa Mwalimu J.K.Nyerere.

Ila muda walivyokwenda wakabadilisha masharti yao. Na serikali imekubali ili ipate misaada lazima kwa "hisani ya watu wa maerekani itajwe".

Otherwise labda wakatae msaada.
 
kwani zamani ilikuwa haijulikani kuwa tunasaidiwa na marekani?
Serikali zetu haziaminiki...zinapenda sifa sana na kusema na pesa ya serikali... So ili kuondoa ukakasi huu inaandikwa kuwa ni msaada...
 
Hata hivyo umechelewa kulijua hilo ukitaka kujua piga hesabu ya miradi yote tangu kuanzishwa mpaka kujenga tasisi zao hapa na mabarozi yao ukienda makanisa makubwa kwa budgeti yetu ya waumini wana mfuko huo wa kujengea matawi nchini
Usipende kusifia usijo jua
 
tukibadilisha itakuaje?unadhani haiwezekani kurejea hali ya awali kabla ya maandiko haya?
Narudia tena hamko kwenye position hiyo. Mtabadilishaje wakati makubaliano yametoka kwake, serikali iliyasoma ika sign.
Maybe wao wenyewe waamue. Maana pesa ni yao, wao ndio wana mamlaka nayo sio sisi.
 
Mimi sielewagi kwa nini MAREKANI = UNITED STATES OF AMERICA
 
Petty mind, petty issues.
"Usiangalie ulipoangukia,tazama ulipojikwaa"
 
"Kwa hisani ya watu wa Marekani" misaada mnayopewa ni kodi zinazotokana na kodi wanazokatwa raia wa kawaida wa Marekani,.. hiyo ndio maana yake...
 
Bure ghali. Unapewa kila sharti lazima ukubali. Kujikubali kama taiga na uwezo pia hayatstupsta Haya masharti
 
Habari za jioni wadau.
Naomba niweke wazi kuwa mimi napenda nchi kama nchi ijitegemee kwa asilimia mia moja lakini pia natambua jambo hili laweza kuchukua muda kutokana na historia ya Taifa na harakati za kidunia zilizokuwepo na zinazoendelea kutokea.

Naamini pia katika kufikia lengo la kimaendeleo bado ni muhimu kupata msaada kutoka kwa wenzetu ambao walitangulia kimaendeleo.

Naamini pia njia bora na ya kweli katika kufikia uhuru wa kiuchumi,kifikra na kimaamuzi ni kupitia jitihada za watanzania wenyewe.

UKAKASI
Nimekuwa nikisikia au kushuhudia matangazo mbalimbali haswa katika sekta ya afya ambayo yanapenda kusisitiza matumizi ya maneno haya...

"KWA HISANI YA WATU WA MAREKANI"

Kwa maoni yangu maneno haya ni ya kudhalilisha mno na sielewi mantiki ya kubandika maneno haya pindi mradi unapopata msaada wa kutoka marekani.

Wakati mwingine kamradi kadogo tu kama vile ujenzi wa choo cha shilingi milioni 5 uatakuta haya maneno yapo tu.

Naamini Tanzania inapokea misaada mingi kutoka nchi mbalimbali lakini sijashuhudia sana maneno dhalili namna hii.

Je nia ya msaada wa marekani haiwezi kufikiwa hadi maneno haya yaandikwe?

Je kuna sheria nchini Marekani inayolazimisha maneno haya yaandikwe?kama ipo ni sheria ipi?

Je kuna vipengele vyovyote katika mkataba wa ushirikiano kati yetu na marekani kinachotaka maneno hayo yaandikwe?

Je wananchi wa Marekani wanapoteza nini maneno hayo yasipoandikwa?

Je Serikali haiwezi kuyapiga marufuku matumizi ya maneno haya ...mbona zamani tulipewa misaada na hakukuwa na aina hii ya maneno ya kudhalilisha?

Karibuni kwa mjadala.


KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!

Iulize serikali yako inayotembeza bakuli kila siku, huku wakirudia uchaguzi kwa bil 2, ila hawana uwezo wa kujenga hixho choo bila msaada wa wamarekani
 
Mbona nchi nyingi wanafanya.Miradi mingi ya wajapani nayo inaandikwa hivyo.China nayo ni hivyo.Korea ni hivyohivyo.

Kwa kuwa wamarekani wamejikita sana kwenye kampeni za kuelimisha jamii kupitia vyombo vya habari.Ndio maana unasikia hiko kibwagizo sana.

Lakini kuna visima vimeandikwa kwa msaada wa serikali ya Kuwait.Madarasa,madaraja yameandikwa kutoka kwa watu wa Japan etc

I hope mtoa mada ujaandika kwa chuki dhidi ya msimamo wa Marekani kwa madikteta wa Africa.
 
Kwa wamarekani kujinadi kwenye miradi wanayoitolea fedha ni sera yao kwenye Mambo ya nje, hata family foundation za marekani kama Melinda Gates, Weill n.k hufanya hivyo ....mfano CUHAS Bugando iliwahi kuitwa Weill Bugando University College of Health Sciences ili wapokee msaada wa Weill Family Foundation. Naamini umeelewa kuwa ni utekelezaji wake sera.

Hata TZ kule Sheri Sheri tumejinadi sana kwenye project tunazo wa fund... Kama hujui.
 
Back
Top Bottom