Ujumbe wa "Kwa hisani ya watu wa Marekani" Lengo lake ni nini haswa?

Mzungu anaweza kukushafua dakika chache kupitia media zake hadi zako au akajisifia yeye mpaka kwa media zako.
Kuhusu hawa watu kuna mambo na jiuliza sana hasa swala la afya mana kuna biashara zao wanaziendesha kupitia mwaya wa elimu yetu ndogo au kufata tu mkumbo.
Mfano (MATANGAZO YA KUSISITIZA UMEZAJI DAWA ZA ARV'S NI MKUBWA SANA KULIKO MATANGAZO YA WATU WAJIKINGE NA KUPATA HIV ZA UKIMWI) hata hivyo hivyo zaman kwenye malaria sema wameona soko la malaria siku hizi ni taifodi na U.T.I .

Naingiwa na mashaka kwa ule msemo wa kuwa ni ili ku promote uzati wa dawa zao
 
Tatizo nini
wenzetu wanapenda transparency sio kama Chadema
ukiwaambia wekeni majina ya watu Na kiasi
walichomchangia matibabu Lisu wanasepa.Wao
wanaweka kibao kwa hisani ya watu wa Marekani alyechangia akienda aweza onyeshwa list nzima ya wachangiaji namba zao za simu walipo nk Chadema waambie waonyeshe hiyo list hata kama ulichangia hawakupi Na mwenye list ni mwenyekiti tu.Hakuna ulaya waweke tu hata wakijenga genge la kuuza nyanya la elfu nne.It is ok.
Acha kudanganya. CDM huwa hawatoi orodha ya wachangiaji kuepusha malumbano. Wengi wa wachangiaji huwa ni wa kutoka CCM. Unataka mwenyekiti wenu aanzishe gubu nao? 😁😁😁😁😁
 
Habari za jioni wadau.
Naomba niweke wazi kuwa mimi napenda nchi kama nchi ijitegemee kwa asilimia mia moja lakini pia natambua jambo hili laweza kuchukua muda kutokana na historia ya Taifa na harakati za kidunia zilizokuwepo na zinazoendelea kutokea.

Naamini pia katika kufikia lengo la kimaendeleo bado ni muhimu kupata msaada kutoka kwa wenzetu ambao walitangulia kimaendeleo.

Naamini pia njia bora na ya kweli katika kufikia uhuru wa kiuchumi,kifikra na kimaamuzi ni kupitia jitihada za watanzania wenyewe.

UKAKASI
Nimekuwa nikisikia au kushuhudia matangazo mbalimbali haswa katika sekta ya afya ambayo yanapenda kusisitiza matumizi ya maneno haya...

"KWA HISANI YA WATU WA MAREKANI"

Kwa maoni yangu maneno haya ni ya kudhalilisha mno na sielewi mantiki ya kubandika maneno haya pindi mradi unapopata msaada wa kutoka marekani.

Wakati mwingine kamradi kadogo tu kama vile ujenzi wa choo cha shilingi milioni 5 uatakuta haya maneno yapo tu.

Naamini Tanzania inapokea misaada mingi kutoka nchi mbalimbali lakini sijashuhudia sana maneno dhalili namna hii.

Je nia ya msaada wa marekani haiwezi kufikiwa hadi maneno haya yaandikwe?

Je kuna sheria nchini Marekani inayolazimisha maneno haya yaandikwe?kama ipo ni sheria ipi?

Je kuna vipengele vyovyote katika mkataba wa ushirikiano kati yetu na marekani kinachotaka maneno hayo yaandikwe?

Je wananchi wa Marekani wanapoteza nini maneno hayo yasipoandikwa?

Je Serikali haiwezi kuyapiga marufuku matumizi ya maneno haya ...mbona zamani tulipewa misaada na hakukuwa na aina hii ya maneno ya kudhalilisha?

Karibuni kwa mjadala.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
Lumumba hakuna mwenye akili !
 
Mkuu hata mm yananikera sana,hasa haya ya kwenye mabango barabarani,mbya zaidi lile neno kwa msaada wa watu wa marekeni linakuwa na herufi kubwa,
 
Jombaa hiyo ni donor condition....ipo tied kwenye condition za kuipata hiyo fund iliyofadhili..mara nyingi huendana na branding..angalia zile logo zinavyopangwa kwenye bango au tangazo utaona inaanza na ya donor.

Hata nyinyi mkisaidia jirani mtasema kwa msaada wa watu wa tz...kama mkipenda.
 
Ni sharti linalolenga nini haswa?
Muache uongo kudanganya ndio maana wazungu wanawajuwa ulaghai wenu kwa wananchi.

Lazima waweke alama ili tujuwe kuna walipa kodi wa Marekani wametusaidia hiki na siyo kuwaacha wagonjwa wa akili kama Kibajaj waseme Magufuli ndio amefanya hivi.

Pesa za rambirambi ni za serikali lakini tunaambiwa katowa mtu fulani sasa usidhani wazungu ni wapuuzi kama wewe ulivyo.
 
Mimi sielewagi kwa nini MAREKANI = UNITED STATES OF AMERICA
Muungano wa majimbo ya Marekani.

Wana serikali za majimbo na Federal government. Au ni kipi hujaelewa hapo? Mfano jimbo la Alaska kijiografia unajuwa lilipo?
 
Jombaa hiyo ni donor condition....ipo tied kwenye condition za kuipata hiyo fund iliyofadhili..mara nyingi huendana na branding..angalia zile logo zinavyopangwa kwenye bango au tangazo utaona inaanza na ya donor.

Hata nyinyi mkisaidia jirani mtasema kwa msaada wa watu wa tz...kama mkipenda.
lengo lake ni nini haswa?
 
Mkuu hata mm yananikera sana,hasa haya ya kwenye mabango barabarani,mbya zaidi lile neno kwa msaada wa watu wa marekeni linakuwa na herufi kubwa,
Na ukiona magari ya kisasa yenye namba za DFP ujuwe ndio haohao usiowapenda ndio wametowa hayo magari kwa ajili ya miradi mbalimbali.
 
DFP haina shida na ukumbuke mfumo huu wa namba za magari ya miradi na ufadhili uliwekwa na watanzania wenyewe tena aliyehusika alikuwa mtanzania ambaye kwa sasa ni Rais wa JMT.
Mfumo wa namba hizi ni kwa hisani ya watu wa Tanzania!
Kumbuka nisichokipenda ni hiko kibwagizo ambacho siku za nyuma hakikuwepo lakini ilikuwa inatambulika tuna misaada kutoka USA.
 
Utakuta tangazo la kutangaza kondomu linakuja na hiki kibwagizo ukijaribu kutafakari yaani ni kama vile unafanya mapenzi kwa hisani ya watu wa marekani!!!
 
DFP haina shida na ukumbuke mfumo huu wa namba za magari ya miradi na ufadhili uliwekwa na watanzania wenyewe tena aliyehusika alikuwa mtanzania ambaye kwa sasa ni Rais wa JMT.
Mfumo wa namba hizi ni kwa hisani ya watu wa Tanzania!
Kumbuka nisichokipenda ni hiko kibwagizo ambacho siku za nyuma hakikuwepo lakini ilikuwa inatambulika tuna misaada kutoka USA.
Kama hukitaki hamia USA au jiue pambaf
 
Ni kwa nini mliwakubali USAID? Au tatizo ni lugha? Sasa kwenye mikataba ya Barrick si ndio mmeuza nchi kabisa?
DFP haina shida na ukumbuke mfumo huu wa namba za magari ya miradi na ufadhili uliwekwa na watanzania wenyewe tena aliyehusika alikuwa mtanzania ambaye kwa sasa ni Rais wa JMT.
Mfumo wa namba hizi ni kwa hisani ya watu wa Tanzania!
Kumbuka nisichokipenda ni hiko kibwagizo ambacho siku za nyuma hakikuwepo lakini ilikuwa inatambulika tuna misaada kutoka USA.
 
Ni sharti linalolenga nini haswa?
Nimewahi kufanya kazi na projects ambazo zimepata fedha kutoka kwa wafadhili mbalimbali mfano EU, NORAD etc Kabla hamjaanza implementation ni lazima mtengeneze kitu kinaitwa VISIBILITY PLAN, ambayo in short ni mpango wenu wa jinsi mtakavyotangaza au ku acknowledge kwa jamiii itakayonufaika na huo msaada fedha hiyo imetoka wapi. Visibility plan therefore will include kuweka logo ya mfadhili, Kama ni kwenye media lazima u mention source of funds etc.....
 
Back
Top Bottom