Waziri wa Afya, Jenista Mhagama amewataka wafanyakazi wa wizara hiyo kuhakikisha huduma za kibingwa za matibabu ya magonjwa mbalimbali zinawafikia wananchi wa hali ya chini bila ya kuwa na vikwazo vyovyote.
Waziri ametoa kauli hiyo jana Agosti 15, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na menejimenti na watumishi wa wizara hiyo mara baada ya kuapishwa kuitumikia wizara hiyo.
Rais Samia Suluhu Hassan alimteua Jenister juzi kuongoza wizara hiyo, kuchukua nafasi ya Ummy Mwalimu aliyeondolewa.
Soma Pia: Uteuzi: Lukuvi, Kabudi warejeshwa Baraza la Mawaziri, Ummy aondolewa Wizara ya Afya. TTCL, TAKUKURU zapata Mabosi wapya
Amewaeleza watumishi hao kuwa Serikali imefanya uwekezaji mkubwa wa vifaa tiba vya kisasa, kujenga majengo ya kisasa, kusomesha wataalamu na kuboresha masilahi ya wafanyakazi na kwamba jukumu lililobaki kwao ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za matibabu.
“Kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali yetu asilimia 95 ya huduma za matibabu ya kibingwa zinapatikana hapa nchini, hivyo ni jukumu lenu kuhakikisha uwekezaji huu unawafikia wananchi wengi zaidi waliopo ndani na nje ya nchi yetu,” amesema Waziri.