Ujumbe wa Lissu kwenda kwa Wajumbe kamati kuu huu hapa

mapessa

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
664
Reaction score
1,168
Kutoka Chadema Hq.
Ameandika Tundu Lissu.

Wajumbe wa Kamati Kuu salaam. Nimepokea barua hiyo kutoka viongozi wetu wa Njombe. Barua yenyewe inajieleza na mnaweza kuisoma na kuielewa wote. Pamoja na kwamba haijatumwa kwa wajumbe wote wa Kamati Kuu, sidhani kama ni sawa sawa kwangu kuikalia kimya.

Ukweli ni kwamba masuala haya yanafahamika humu, hata kama ni kwa njia zisizo rasmi. Kamati Kuu ni chombo cha chama chenye mamlaka makubwa kikatiba.

Lakini mamlaka hayo yana mipaka yake, sio unlimited. Mipaka hiyo ni Katiba yenyewe ya Chama na sheria za nchi hii. Kuna baadhi yetu tunaamini kwamba chochote kinachofanywa na sisi Kamati Kuu ni halali, bila kujali Katiba yetu inasema nini.

Baadhi yetu tunajificha nyuma ya maamuzi ya vikao vya Baraza Kuu, bila kujali mamlaka ya kikatiba ya Baraza Kuu kuhusu maamuzi hayo, na kufanya maamuzi tutakavyo sisi. Hii sio tu sio sahihi kikatiba, ni hatari kwa chama chetu. Kwenye chaguzi zinazoendelea kila mahali, secretariat ya Kamati Kuu na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu, wamefanya maamuzi mengi na makubwa.

Kimsingi, wajumbe wa secretariat wameendesha chaguzi za chama karibu katika ngazi zote hadi sasa.

Wajumbe wa secretariat wamepangua na kupanga safu za uongozi wa chama; wameengua wagombea wasiowataka kwa vigezo vyao wenyewe; wametengua maamuzi ya vikao halali vya chama wasiyoyataka; wameamua rufaa zilizotokana na maamuzi yao wenyewe, n.k.

Naomba tuulizane: je hivyo ndivyo Katiba yetu inavyotaka???

Malalamiko juu ya matendo haya ni mengi ajabu na yapo kwenye Kanda karibu zote. Ninaamini wajumbe wa Kamati Kuu mnayafahamu malalamiko haya, kama tunavyoyafahamu tulio viongozi wakuu wa chama.

Suala linalonitatiza mimi ni kwa nini tumeamua kuyaruhusu au kuyanyamazia. Tunayaruhusu au kuyanyamazia kwa ajili ya maslahi ya Chama kweli au ni kwa ajili ya maslahi mengine tusiyoyajua wengine.

Kumekuwa na matumizi ya nguvu kubwa sana, ya kifedha na kimadaraka, katika chaguzi hizi. Chama chetu kina matatizo makubwa ya fedha za uendeshaji wa shughuli za chama katika ngazi zote za chama.

Lakini katika chaguzi hizi kumekuwa na fedha nyingi ajabu. Mimi najiuliza hizi ni fedha zetu wenyewe, au ni fedha za Abduli na mama yake???

Fedha ni muhimu sana katika maisha ya binadamu na katika uendeshaji wa shughuli za chama. Lakini ni kweli pia kwamba sio kila pesa tunayoihitaji au kuitumia ni pesa halali, na sio kila matumizi hayo ni matumizi halali.

Tusije tukasahau kwamba pesa ndiyo iliyomuuza Yesu kwa watesi wake, na pesa ndiyo mojawapo ya silaha kubwa za maangamizi zinazotumiwa na watesi wa wananchi wetu na watesi wetu wenyewe miaka yote.

Tusije tukasahau maneno ya Mwenyekiti wetu kwamba katika vitu vyote vinne vinavyohitajika kushinda uchaguzi (au kuendesha chama) - wagombea, agenda, oganaizesheni , pesa - pesa ni hitaji la mwisho kabisa.

Sasa, kwa kinachoendelea kwenye chaguzi hizi, pesa inaelekea kuwa ndio hitaji la kwanza. Na tunaelekea kuamini kuwa pesa ni pesa, hata kama ni ya Abduli na mama yake.

Tusipokataa utamaduni huu mpya kwenye chama chetu, pesa hizi zitatutokea puani. Zitatuchafua na kutuharibia chama, kama ambavyo zimewachafua na kuwaharibia wa vyama vingine tunaowafahamu vyema.

Nawaombeni tusikubali uchafu huu kwenye chama chetu. Nawaombeni haya yanayoendelea kwenye chama kwenye chaguzi hizi tuyazungumze kwa undani na kwa uharaka unaohitajika.

Tusikubali kutishwa na kutishana hata humu kwenye Kamati Kuu. Tunaangaliwa, sio tu na watesi wetu wanaotutakia maafa, bali pia na wapenzi wetu wanaotutakia mema.

Tusikubali kukumbatia au kunyamazia uovu kwa sababu tu uovu huo umefunikwa na pesa au na madaraka. Nawaombeni tuyazungumze haya kwenye kikao rasmi cha Kamati Kuu.
Tundu Lissu
 
Adui muombee njaa kabla hakijashika madaraka rushwa imetamakaq ndio nyumbani kwao mafisadi wakubwa!
 
Lisu katupa dongo kwa mwenyekiti kisomi. Anafahamu kuwa mwenyekiti hutumia pesa kubaki madarakani na kusababisha yeye (Lisu) kushindwa kugombea uongozi wa chama.

Lakini namhakikishia kuwa mwenye tabia yake (hasa yenye masilahi na tumbo lake) huwa haachi. Tayari mwenyekiti ashandaa chawa wa kujifanya kumchukulia kadi ya kugombea, huku wengine wakisambaza ujumbe wa tuna imani na mwenyekiti, kamanda mkuu tuvushe nk.

Lisu ataishia kutupa madongo mitandaoni mpaka yamuangukie mwenyewe, lakin nafasi ya namba 1 wa chama haipati.
 
Bado siamini ujumbe huu Hadi Lissu atoe ufafanuzi kukubali au kuukana.
 
Umeandika Ujinga.

Tundu Lissu si wa level hiyo.

Anaendeles kuwanyosha hadi mshike adabu.

Twende Kamanda Lissu.
 
Tusikubali kukumbatia au kunyamazia uovu kwa sababu tu uovu huo umefunikwa na pesa au na madaraka. Nawaombeni tuyazungumze haya kwenye kikao rasmi cha Kamati Kuu.
Mi sijasoma habari yako ndefu kwa sababu moja tu: Nilitegemea kuona hiyo barua yenyewe umeiweka hapa; badala ya wewe mwenyewe mleta mada kuanza kupiga stori ndefu hapa.
Sasa sijui umeandika takataka gani humo ndani.
 
Lisu katupa dongo kwa mwenyekiti kisomi. Anafahamu kuwa mwenyekiti hutumia pesa kubaki madarakani na kusababisha yeye (Lisu) kushindwa kugombea uongozi wa chama.

Lakini namhakikishia kuwa mwenye tabia yake (hasa yenye masilahi na tumbo lake) huwa haachi. Tayari mwenyekiti ashandaa chawa wa kujifanya kumchukulia kadi ya kugombea, huku wengine wakisambaza ujumbe wa tuna imani na mwenyekiti, kamanda mkuu tuvushe nk.

Lisu ataishia kutupa madongo mitandaoni mpaka yamuangukie mwenyewe, lakin nafasi ya namba 1 wa chama haipati.
Lissu hana shida ya kuwa Mwenyekiti wa Chama kwa sasa !
Lissu na Mbowe ni damu damu hawawezi kugombanishwa NEVER EVER !!
 
Uzuri wa Lisu ni panga lenye makali kuwili, haangalii uovu umefanywa na nani, bali huuangalia uovu wenyewe.

Namkumbuka mzee Warioba alipohojiwa juu ya Lisu akiwa Rais. Akasema atakuwa kiongozi mzuri. Ila Lisu akiwa Rais, itabidi sote tujifunze kufuata sheria na katiba.
 
Na Watanzania kuvunja sheria na kuvunja Katiba huwa ni kitu cha kawaida sana kwao !
 
Lisu katupa dongo kwa mwenyekiti kisomi. Anafahamu kuwa mwenyekiti hutumia pesa kubaki madarakani na kusababisha yeye (Lisu) kushindwa kugombea uongozi wa chama.

Lakini namhakikishia kuwa mwenye tabia yake (hasa yenye masilahi na tumbo lake) huwa haachi. Tayari mwenyekiti ashandaa chawa wa kujifanya kumchukulia kadi ya kugombea, huku wengine wakisambaza ujumbe wa tuna imani na mwenyekiti, kamanda mkuu tuvushe nk.

Lisu ataishia kutupa madongo mitandaoni mpaka yamuangukie mwenyewe, lakin nafasi ya namba 1 wa chama haipati.
Unapakatwa ukiwa wap mkuu?!
 
Kutoka Chadema Hq.
Ameandika Tundu Lissu.

Wajumbe wa Kamati Kuu salaam. Nimepokea barua hiyo kutoka viongozi wetu wa Njombe. Barua yenyewe inajieleza na mnaweza kuisoma na kuielewa wote. Pamoja na kwamba haijatumwa kwa wajumbe wote wa Kamati Kuu, sidhani kama ni sawa sawa kwangu kuikalia kimya.

Ukweli ni kwamba masuala haya yanafahamika humu, hata kama ni kwa njia zisizo rasmi. Kamati Kuu ni chombo cha chama chenye mamlaka makubwa kikatiba.

Lakini mamlaka hayo yana mipaka yake, sio unlimited. Mipaka hiyo ni Katiba yenyewe ya Chama na sheria za nchi hii. Kuna baadhi yetu tunaamini kwamba chochote kinachofanywa na sisi Kamati Kuu ni halali, bila kujali Katiba yetu inasema nini.

Baadhi yetu tunajificha nyuma ya maamuzi ya vikao vya Baraza Kuu, bila kujali mamlaka ya kikatiba ya Baraza Kuu kuhusu maamuzi hayo, na kufanya maamuzi tutakavyo sisi. Hii sio tu sio sahihi kikatiba, ni hatari kwa chama chetu. Kwenye chaguzi zinazoendelea kila mahali, secretariat ya Kamati Kuu na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu, wamefanya maamuzi mengi na makubwa.

Kimsingi, wajumbe wa secretariat wameendesha chaguzi za chama karibu katika ngazi zote hadi sasa.

Wajumbe wa secretariat wamepangua na kupanga safu za uongozi wa chama; wameengua wagombea wasiowataka kwa vigezo vyao wenyewe; wametengua maamuzi ya vikao halali vya chama wasiyoyataka; wameamua rufaa zilizotokana na maamuzi yao wenyewe, n.k.

Naomba tuulizane: je hivyo ndivyo Katiba yetu inavyotaka???

Malalamiko juu ya matendo haya ni mengi ajabu na yapo kwenye Kanda karibu zote. Ninaamini wajumbe wa Kamati Kuu mnayafahamu malalamiko haya, kama tunavyoyafahamu tulio viongozi wakuu wa chama.

Suala linalonitatiza mimi ni kwa nini tumeamua kuyaruhusu au kuyanyamazia. Tunayaruhusu au kuyanyamazia kwa ajili ya maslahi ya Chama kweli au ni kwa ajili ya maslahi mengine tusiyoyajua wengine.

Kumekuwa na matumizi ya nguvu kubwa sana, ya kifedha na kimadaraka, katika chaguzi hizi. Chama chetu kina matatizo makubwa ya fedha za uendeshaji wa shughuli za chama katika ngazi zote za chama.

Lakini katika chaguzi hizi kumekuwa na fedha nyingi ajabu. Mimi najiuliza hizi ni fedha zetu wenyewe, au ni fedha za Abduli na mama yake???

Fedha ni muhimu sana katika maisha ya binadamu na katika uendeshaji wa shughuli za chama. Lakini ni kweli pia kwamba sio kila pesa tunayoihitaji au kuitumia ni pesa halali, na sio kila matumizi hayo ni matumizi halali.

Tusije tukasahau kwamba pesa ndiyo iliyomuuza Yesu kwa watesi wake, na pesa ndiyo mojawapo ya silaha kubwa za maangamizi zinazotumiwa na watesi wa wananchi wetu na watesi wetu wenyewe miaka yote.

Tusije tukasahau maneno ya Mwenyekiti wetu kwamba katika vitu vyote vinne vinavyohitajika kushinda uchaguzi (au kuendesha chama) - wagombea, agenda, oganaizesheni , pesa - pesa ni hitaji la mwisho kabisa.

Sasa, kwa kinachoendelea kwenye chaguzi hizi, pesa inaelekea kuwa ndio hitaji la kwanza. Na tunaelekea kuamini kuwa pesa ni pesa, hata kama ni ya Abduli na mama yake.

Tusipokataa utamaduni huu mpya kwenye chama chetu, pesa hizi zitatutokea puani. Zitatuchafua na kutuharibia chama, kama ambavyo zimewachafua na kuwaharibia wa vyama vingine tunaowafahamu vyema.

Nawaombeni tusikubali uchafu huu kwenye chama chetu. Nawaombeni haya yanayoendelea kwenye chama kwenye chaguzi hizi tuyazungumze kwa undani na kwa uharaka unaohitajika.

Tusikubali kutishwa na kutishana hata humu kwenye Kamati Kuu. Tunaangaliwa, sio tu na watesi wetu wanaotutakia maafa, bali pia na wapenzi wetu wanaotutakia mema.

Tusikubali kukumbatia au kunyamazia uovu kwa sababu tu uovu huo umefunikwa na pesa au na madaraka. Nawaombeni tuyazungumze haya kwenye kikao rasmi cha Kamati Kuu.
Tundu Lissu
Safi kabisa,Mafisadi papa yameigeukia chadema sasa,nilisema hapa watu kama grattan mukoba,mungai na Meya jacobo ni watu waliopandikizwa,nikatukanwa sana sababu mimi ni ccm, hawakujua kuwa mpinzani wako chambua mema yake sio kupuuza kila kitu.
 
Hii itakuwa imeandikwa na Lucas Mwashambwa! Yaani Tundu Lissu aropoke hadharani badala ya kupeleka hoja kwenye kikao cha Kamati Kuu? This is very low, kabisa itakuwa imeandikwa na zero brain Lucas Mwashambwa!
 
Back
Top Bottom