.....maana nionavyo hapo pana mtego ikiwa watakaokataliwa watafika laki basi hata walioandikishwa nao watajiunga nao na kuzidi kupeleka hati za madai kunakohusika juu ya madai ya kuwepo kwa Taifa la Pemba ,au hamlioni hilo ?
Mkuu hayo hapo juu yawe ni maoni yako tu, hayawakilishi(wala yasionekane kuwakilisha,kuunga mkono,ku-comment ujumbe uliotelewa na Kurugenzi ya Uenezi ya CUF, wala
si msimamo wa chama cha wananchi CUF.
Chama kitaendelea kudai na kupigania haki na mabadiliko kwa njia na taratibu za kinchi kikiamini mabadiliko ya kweli yataletwa kwa kuwahamasisha wananchi kujua haki zao na njia sahihi ya kuzipigania haki hizo.
Kadhalika, kikiamini kuwa mageuzi ya kweli yanapatikana kwa gharama na jasho na kwa njia ya kushindana kwa sera na itikadi sahihi,bila ya kupigana na kugombana au kutengana kwa namna yoyete isiyokidhi maslahi ya wananchi na kukubaliana kama wananchi.
Kasumba na sumu za
kujitenga kwa Pemba zimeanza kutumiwa na "maadui" wa chama cha CUF(wanajuulikana) wakisaidiwa na
"vyombo vya usalama na Propaganda" ili kuipa jina baya CUF ionekane kuwa ni chama cha watu wa Upande fulani tu na si chama cha kitaifa kwa mujibu wa sheria, kinacholenga kuleta utengano wa jamii ya watanzania jambo ambalo si kweli.
Imesemwa kuwa ukitaka kumuuwa mbwa mpe jina baya. CUF imeanza kuwa na hadhari na kauli hizi zinazoelekea kutumiwa kujenga chuki kwa chama, wapenzi na wanachama wa CUF.
Sumu hizi zinatafutiwa mashiko kwa nguvu hasa suala la
baadhi ya wananchi wa Pemba kudaiwa kutaka kuwa na taifa lao lilipo ibuka, na kuihusisha CUF ambayo imeshatoa tamko kuwa
haihusiki na maoni binafsi ya wananchi na
si msimamo wa chama kwa kuwa kila mwananchi anayohaki na uhuru wa kutoa maoni yake kwa mujibu wa sheria na CUF inaheshimu uhuru huo.
CUF haiendeshwi na maoni ya watu wa kawaida wa mitaani bali ni chama chenye katiba, kanuni na miongozo yake iliyokubaliwa na vyombo sahihi vya chama kwa mujibu wa sheria za nchi, na kama kuhukumiwa na ihukumiwe kwa katiba na kanuni zake.
Wakati umefika sasa watu wasioitakia mema CUF waache kuihusisha na kauli na madai binafi ya watu wa kawaida kwa malengo ya kuidhofisha na kuhujumu umaarufu wa chama hicho kwa visingizio vya kipuuzi vya
ubaguzi, ukabila na
udini.
CUF ni chama cha wananchi wote(haki sawa kwa wote) na si chama cha mtu, watu, kundi la watu, jamii ya watu au eneo la watu fulani.
Haitakuwa busara na haki kuporoja mambo yasiyohusika na itikadi, mtazamo na sera na siasa za CUF.
Naomba ujumbe wa Maalim Seif Shariff Hamad usomeke, ueleweke na ufahamike kama ulivyo na kichwa cha habari hapo juu.
HAKI SAWA KWA WOTE.