SI KWELI PreGE2025 Ujumbe wa Maria Sarungi mtandao wa X, asema John Heche anakiangamiza chama

SI KWELI PreGE2025 Ujumbe wa Maria Sarungi mtandao wa X, asema John Heche anakiangamiza chama

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
photo_2025-07-29_09-00-59.jpg
photo_2025-07-29_09-01-06.jpg
photo_2025-07-29_09-01-11.jpg
 
Tunachokijua
Maria Sarungi ni mwanaharakati kutokea Tanzania, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za binadamu, utawala wa kisheria unaozingatia misingi ya kidemokrasia ambapo pia amekuwa akitumia mitandao ya Kijamii hasa mtandao wa X.

Siku za karibuni kumekuwapo na taarifa nyingi zisizo za kweli zikisambazwa mtandaoni kumhusu Maria Sarungi akihusishwa na CHADEMA, pamoja na viongozi wa chama hicho. Rejea hapa, hapa na hapa.

Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa Facebook wamekuwa wakisambaza ujumbe unaodaiwa kuchapishwa na Maria Sarungi kupitia mtandao wa X, huku ukitumika utambulisho wa grafiki za Mwanahalisi, Mwananchi na Jambo TV kusambaza taarifa hiyo.


Je, ni upi uhalisia wa ujumbe huo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key words search) umejiridhisha kuwa ujumbe huo haujaandikwa na Maria Sarungi kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa X, bali ni wa kutengenezwa na wapotoshaji.

Pia grafiki zilizotumika kusambaza taarifa hiyo ni za kughushi kwani hazijachapishwa na vyombo hivyo (Mwanahalisi, Mwananchi, na Jambo TV)​
Back
Top Bottom