Ujumbe wa Seleman Bungara '' Bwege'' kwenda kwa Zitto Kabwe

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
22,269
Reaction score
58,563
Mbunge wa zamani wa Kilwa Kusini Seleman Bungara 'Bwege' ameandika kwenye mitandao ya kijamii na kueleza kuwa masikitiko yake ya kutomuona Zitto Kabwe, Kiongozi mstaafu wa Chama cha ACT-Wazalendo.

"Tunajua Tundu Lissu ni rafiki yako wa karibu sana alipopigwa risasi 16 ulisafiri kwenda Kenya kumuona hukuishia hapo ukasafiri Mpaka Ubelgiji kwenda kumuona ila sasa LISSU yupo Gerezani Ukonga hujawahi kumtembelea wala Mahakamani hujawahi kwenda, huenda huna nauli ila hata "ku-tweet" tu na kusema KESI ya Lissu ni KESI ya MCHONGO hujawahi kama tatizo bando na nauli tushirikishe JAMHURI tutachanga, au hauchezi mechi za ndani?, kama na wewe ni shaidi wa kiboksi tujue.
 
Bwege amemtandika huyo dalali wa mafisadi kofi kama hili kupitia huo ujumbe.

Safi sana Bwege, mwingine yeye alihudhuria hadi dira ya CCM ila kwenda mahakamani hawezi , unafiki wa kiwango cha juu kabisa.
 
Huyo Zito na Mbowe wamekanywa kabisa maana wao ni project. Hivyo wakienda mahakamani ni kumtengenezea kick Lisu. Ukila hela ya shetani lazima uishi kifungoni.
Leo hii ndio akili yako imetambua kuwa hawa ni project CCM? Huko nyuma ulikuwa kibaraka mkubwa wa Mbowe
 
Aaachane naye tuu hana faida yoyote kwake
 
ama kwa hakika bwege ni bwege haswa,

huenda anatamani viongozi wote wa kisisa wawe kama yeye
 
Zitto mnafiki sana na ndo tayali keshajifia kisiasa.
Nikimfikiria Zitto wa mwaka 2007, unamwona ni mwanasiasa mwenye fikra pevu na muono wa mbali.
Tamaa ya madaraka, unafiki na kukubali milungula ndo kumemfikisha hapa.
 
Leo hii ndio akili yako imetambua kuwa hawa ni project CCM? Huko nyuma ulikuwa kibaraka mkubwa wa Mbowe
Naona muumini wa dhalimu magu unataka kujipunguzi stress. Tafuta uzi wowote niliokuwa namsifia Mbowe, ukiuupata nipigwe ban mwaka mzima. Kisha mimi nitakuonyesha post zangu kibao nilivyopinga upuuzi wa Mbowe wa kumleta tapeli Lowassa ndani ya cdm. Na kupinga yeye kuwa mwenyekiti wa cdm zaidi ya miaka 10. Ushahidi wangu upo wazi humu humu jf.
 
Zitto anaogopa kumuudhi mfadhili wake. Kajamaa kana roho ya kichawi kabisa.
 
Madhalimu huwaoni mpaka umsingizie Magu? Weka hapa nyuzi za kumpinga Mbowe we kibaraka mkubwa ili tupate ushahidi
 
Madhalimu huwaoni mpaka umsingizie Magu? Weka hapa nyuzi za kumpinga Mbowe we kibaraka mkubwa ili tupate ushahidi
Weka ww nilipomuunga mkono maana ndio umenituhumu. Yaani utuhumu ww, nidhibitishe mimi?
 
Hivi Bwege alimtembelea Lissu Nairobi? Alikuwa anaonekana Mahakamani wakati wa kesi ya Mbowe? Angeachana na Zitto kwa sababu sasa hivi si mwanachama mwenzake.

Kama kumtembelea Lissu ndio kigezo cha uzalendo, basi Mheshimiwa Rais ni kinara maana alimtembelea akiwa Nairobi na Ubelgiji.

Amandla...
 
BWEGE mwenye AKILI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…