Ujumbe wa shukrani baada ya kufunga ndoa na kumaliza fungate

Ujumbe wa shukrani baada ya kufunga ndoa na kumaliza fungate

moto2012

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2012
Posts
2,309
Reaction score
1,552
Ingawa inaaminika siku hizi waowaji hawapo ila nawapa big up wale wote walitimiza tukio/tendo hili adhimu la kufunga ndoa, sitaki niulizwe kama nimepitia hii kitu au la, ila kwa hisani ya my waifu Preta, nitasoma maoni yenu ila sita jibu

Kifupi nimeshangazwa kutumiwa kaujumbe kafuatako na rafiki yangu kipenzi ambaye ndo amemaliza tu ka muda kake ka fungate, ka ujumbe kanasomeka hivi

"Familia mpya ya BW & Bi...............inapenda kuchukua nafasi hii kukushukuru wewe moto2012 kwa mchango wako wa hali na mali kufaniksha shughuli yetu, Mungu akubariki sana na akuzidishie pale ulipo punguza!" Mwisho wa kunukuu

Nimejiuliza maswali mengi ila hili la familia mpya, nimekosa majibu, najiuliza hivi familia nazo zinachakaa? Hivi mimi na Preta wangu ni famila kuu kuu? Vipi familia ya Mtambuzi na mama Ngina wake, nikakumbuka familia ya babu Asprini, nahisi hii itakuwa na viraka vingi sana, dadangu Fixed Point familia yako ipoje, Babu Dark City tuambie wewe yako ina hadhi ipi?
 
ha haaa, familia "mpya". watu wengi wanapenda kutumia hilo neno.
labda ni mpya sababu ndo wanaanzisha hiyo familia, ingawa "changa" nadhani ndo lingekuwa neno muafaka.
Mimi yangu ya shem wako naona imekomaa tu, ila kuchakaa noooooooooooooo, hatutegemei ichakae kabisa katika maisha yetu haya
 
Shem habari za masiku?
 
Famili chakavu ya mzee DC Dark City ..... haha haaa...!!!
 
Last edited by a moderator:
familia mpya, kila siku maneno mapya ....
 
Back
Top Bottom