Habari za Zanzibar
JF-Expert Member
- Dec 18, 2024
- 651
- 433
๐จ๐ท๐๐บ๐ฏ๐ฒ ๐๐ฎ ๐ง๐ฎ๐ป๐๐ฎ๐ป๐ถ๐ฎ ๐๐ฎ๐๐ฎ๐๐ถ๐น๐ถ ๐๐ป๐ด๐ผ๐น๐ฎ ๐ธ๐๐ฒ๐ป๐๐ฒ ๐ ๐ธ๐๐๐ฎ๐ป๐ผ ๐๐ฎ ๐ ๐ฎ๐ท๐ถ ๐ธ๐ฎ๐บ๐ฎ ๐๐ถ๐๐ป๐ด๐ผ ๐ฐ๐ต๐ฎ ๐๐บ๐ฎ๐ป๐ถ
Ujumbe wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umewasili jijini Luanda, Angola kushiriki Mkutano wa 4 la Biennale ya LuandaโJukwaa la Afrika kuhusu Utamaduni wa Amani litakalofanyika Luanda, Angola, tarehe 22โ23 Oktoba 2026.
Ujumbe huo ukiongozwa na Mheshimiwa Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akimwakilisha Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, unajumuisha pia Mheshimiwa Jumaa Hamidu Aweso (Mb.), Waziri wa Maji na wataalam wengine. Kaulimbiu ya mkutano huo ni โKuimarisha Utawala wa Rasilimali Maji Inayovuka Mipaka barani Afrika kama Nyenzo ya Kuzuia na Kutatua Migogoro.โ
Majadiliano yatahusisha diplomasia ya maji na usimamizi wa rasilimali za maji zinazovuka mipaka; ushiriki wa jamii, wanawake na vijana; athari za mabadiliko ya tabianchi, uhamaji na migogoro; pamoja na uwekezaji katika miundombinu ya maji na kujenga uwezo. Pamoja na mambo mengine, Ujumbe wa Tanzania utatumia jukwaa hili kueleza mafanikio yake katika sekta ya maji, mchango wake katika kuimarisha ushirikiano wa kikanda na usimamizi wa pamoja wa mabonde, mito na maziwa.

Attachments
-
publer-1792993610977.jpg918.9 KB · Views: 6 -
publer-1792993614740.jpg394 KB · Views: 6 -
publer-1792993625237.jpg793.4 KB · Views: 5 -
publer-1792993623313.jpg1 MB · Views: 6 -
publer-1792993619861.jpg949.7 KB · Views: 6 -
publer-1792993616915.jpg1.1 MB · Views: 5 -
publer-1792993627920.jpg970.5 KB · Views: 6 -
publer-1792993630063.jpg890 KB · Views: 6 -
publer-1792993631845.jpg975.5 KB · Views: 6 -
publer-1792993633703.jpg881.3 KB · Views: 6