Uchaguzi 2020 Ujumbe wa wazi kwa mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu kuelekea uchaguzi mkuu

Uchaguzi 2020 Ujumbe wa wazi kwa mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu kuelekea uchaguzi mkuu

MWAISEMBA CR

Member
Joined
Apr 21, 2014
Posts
87
Reaction score
81
✳UJUMBE WA WAZI KWA MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CHADEMA, TUNDU LISSU KUELEKEA UCHAGUZI MKUU🆕

🔵From : Shujaa Charles Richard Mwaisemba (©️®️ M )
stmwaisembac@gmail.com
0712-054498/0759-420202

Kwanza kabisa nianze kwa kukupongeza sana sana niliposikia kuwa umefanya ibada ya shukurani Agosti 10,2020 katika Kanisa la mtakatifu Rita wa kashia lililopo Ikungi, Mkonoani singida kwa ajili ya Kumshukuru Mungu aliyekunusurisha na hatari ya mauti iliyotokea September 7, 2017 baada ya kushambuliwa na risasi 16 za SMG na kwa ajili ya kuwashukuru watanzania wote waliokuombea na kujitoa kwa hali na mali kwa ajili ya kunusurisha maisha yako.

Lakini jambo lililonifurahisha zaidi na kuwafurahisha Watanzania wengi, ni Roho yako ya msamaha uliyoionyesha kwa kuahidi kutokulipa kisasi mtu yeyote waliohusika na kufurahia kwa tukio hilo.Kwa Roho hiyo ya msamaha uliyoionyesha ni Roho ya Mungu kamili anayesamehe na kusahau maovu yetu ambayo itakupa kibali kikubwa hasa mbele za Mungu na Mbele za wanadamu.

Jambo la pili, nilolotamani kukuambia tunapoelekea katika uchaguzi mkuu wa 2020 ni kuepuka kushambuliia kundi lolote la watu au au taasisi zozote ambazo zinaonekana kama hazikuungi mkono au zinakupinga moja kwa moja, kumbuka nyuma ya taasisi hizo zina watu wengi nyuma yao ambao ndio wapiga kura na ambao hawapo upande wowote wa chama ila wataangalia reaction zenu juu yao na hivyo inaweza kupelekea si tu kukosa kura zao bali kukosa kibali hata kwa watu wa upande wako.

Inabidi kuwa makini sana kama si wewe basi timu kampeni zako, kuwaonya kutumia lugha za matusi au za kushambulia taasisi hizo hasa Taasisi za kidini au viongozi wa dini.Wanapowatukana au kuwashambia viongozi wa dini ujue vile vile umewashambulia waumini wao ambao hawatafurahia kuona viongozi wao wakivunjiwa heshima mbele ya jamii na hivyo inaweza kupelekea kupoteza kundi kubwa la watu ambao wangeweza kukusapoti hata kama viongozi wao wanaonekana wapo kinyume nanyi.Usishindane wala kuwajibu vibaya viongozi wa dini hilo litakupa credity kubwa katika uchaguzi huu.

Inakupasa kutumia nguvu kubwa kueleza sera na matatizo ya watu ambayo wanategemea kutatuliwa na serikali yenu ikiwa ikuchukua dola kuliko kutumia muda mwingi kujibishana na vikundi vya CCM au taasisi zinazowaunga mkono ambavyo vina lengo la kukutoa katika mstari wa kuwaelezea Ilani ya sera ya chama chenu mlichokusudia kuwafanyia watanzania.

Jambo jingine la mwisho, ninaloweza kukutia Moyo na kukuhakikishia ikiwa kweli Tume ya uchaguzi itakuwa Huru na haki na ikiwa utaplay smart kucheza na hisia za watanzania walio wengi, nafahamu unaweza kupata Ushindi tena kwa Kishindo bila shaka.

Nafahamu uwezo wako wa kujenga hoja, Uwezo wako wa kusimamia unavyoviahidi na kuvizungumza, Ujasiri wako wa kusema Ukweli bila kuwa na hofu ya chochote na nafahamu wewe ndio mtu sahihi kwa wakati huu mwenye uwezo wa kupambana na mtu aina ya Magufuli, ila fahamu Neno PASIPO YEYE(Mungu) , WEWE HUWEZI KUFANYA NENO LOLOTE(YOHANA 15:5:WARUMI 8:31), Tena fahamu BWANA ASIPOKWENDA NAWE KATIKA HATUA ZOZOTE, HUTAWEZA NA UTASHINDWA NA MAADUI ZAKO

Maana yangu ni Kwamba, Pamoja na uwezo wote ulio nao, umaarufu na ujasiri ulio nao, Pasipo kuonyesha kumtumaini Yeye Mungu katika kila jambo na kumuhofu yeye Mungu bado hatutaweza kushinda,Kumbuka ni Mungu ndiye anayempa mtu yeyote Mamlaka ya kutawala na Kumiliki (YOHANA 19:9-11)

Kumbuka watanzania, wanamtafuta Rais si tu mwenye uwezo wa kuwatoa katika ufungwa wa uhuru wao wa kujieleza,katika umsakini na ujinga na maradhi lakini zaidi sana wanatafuta Rais mwenye hofu ya Mungu ambaye ataweza kumtanguliza Mungu kwanza katika kila jambo kuliko kutumainia uwezo wake. Hivyo usipuuze ushauri au mambo yoyote yanayohusiana na Mungu kwa kufuata mfumo wa ulimwengu mzima unavyoendesha mambo yake.

Itakuwa ni jambo la ajabu sana ambalo utamsikitisha Mungu upeo, ikiwa Utapuuza Mambo ya Mungu na kuheshimu watumishi wa Mungu, Kumbuka si kwasababu wewe ni bora sana au una kitu cha ziada sana mpaka huyu Mungu asimamishe dunia kwa ajili yako kuuona MUUJIZA UNAOTEMBEA kwamba Upigwe Risasi 16 za SMG na bado uko hai, Bila shaka watanzania wamefahamu kuwa Mungu ana makusudi na wewe na nafikiri ndio Maana wengi wao wanamatumaini na wewe kuwa ndiye mtu sahihi unayeweza KULETA MABADILIKO YA KIMFUMO WALIYOKUWA WANAYAHITAJI KWA MIAKA MINGI.Ikiwa hutatambua kwanini Mungu kakuacha hai mpaka leo na kukuokoa na mauti ile basi utakuwa ni mtu wa ajabu sana kupata kutokea, ila kwa kuwa hapendi kuona yeyote anapotea bali wote wafikilie Toba hivyo naamini na hilo utalizingatia.

Mwisho kabisa nikutakie Mafanikio mema katika Kampeni mtakazozianza hivi karibuni na Mungu atakutangulia. Tunaiombea nchi yetu ipate Rais atakaweza kutupatia Katiba mpya, atakayeweza kubadilisha mifumo mibovu yote katika nchi hii,atakaweza kuruhusu uhuru wa habari na kujieleza, atakayeleta maendeleo ya watu kwanza, atakayeheshimu katiba yetu na mihimili yote, atakayeweza kusimamia rasilimali za nchi hii na Kupingana na rushwa kwa nguvu kubwa n.k.

Mungu akubariki.
 
Kama hatatubu ulaghai yeye na chama chake, waliotufanyia kabla ya ule uamuzi wa kubadili gia angani na kukubali chama kukodiwa kwa muda na EL anajidanganya tu. Hata kauli yake pale mlimani city kuwauliza wajumbe, Eti mliyaona mabilioni ya EL?" Ni kauli ya kitapeli na ulaghai, kwasababu wajumbe na wafuasi hatukuwepo wakati wa makubaliano yao na EL.

Kuuliza swali kama lile ni aina nyingine ya utapeli aliojifunza Ubeligiji/huko alikotoka kwenye matibabu na kufanya kampeni ya kuichafua Tanzania kimataifa. Mimi bado na mshangaa huyu mtu, ana akili timamu kweli? Unachafua nchi unayotaka upewe ridhaa ya kuwa rais wake ili ukishakuwa rais useme mimi ni malaika nimeshuka juu mbinguni nchi hii haina matatizo tena ama?

Wewe uliejitolea kumshauri mwambie yeye na wenzake watubu ule utapeli na ulaghai wao wa 2015. Mbili mwambie maadamu hawajatubu hadharani tukasikia kama tunavyosikia shukrani. Basi sadaka yake ya shukrani huenda ikawa chukizo kwa Mungu na ikaiamsha hasira ya Mungu zaidi.

Ni ulize alipo fika hapo kahama na maeneo ya jirani alikumbuka hata kusema lolote kuhusu yule alimaruhumu Mawazo, muhamga mwingine wa siasa zao za ulaghai.
 
Aanze kwanza kutubu yule MALAIKA MKUU mwizi wa trilioni 1.5!

Kwa nini pale Dodoma akiwa kwenye msafara wake, Lissu sehemu nyingine alikuwa akipungia mikono miti na watu waliokuwa kwenye mishe zao hawakuwa na time na yeye? Alilenga kuwapa mabeberu walio mtuma ujumbe gani?
 
Kwa nini pale Dodoma akiwa kwenye msafara wake, Lissu sehemu nyingine alikuwa akipungia mikono miti na watu waliokuwa kwenye mishe zao hawakuwa na time na yeye? Alilenga kuwapa mabeberu walio mtuma ujumbe gani?
Nakazia tena yule KIONGOZI MKUU WA MALAIKA, NA JIWE MKUU arudishe 1.5 trilioni kwanza!
 
Zaidi, kampeni yake iwe ya kijiji kwa kijiji na mtaa kwa mtaa. Bila hivyo itakuwa sana ngumu kwake. Magazeti, TV, radio zote haziruhusiwi kutoa habari zake. Azitumie vizuri siku 60 za kampeni. Nadhnai hilo analijua vizuri ndhio maana kaamua kutumia muda wa kutafuta wadhamini vizuri.
 
Back
Top Bottom