Ujumbe wangu kwa Waziri Bashungwa na Rais; Ajira za Tamisemi zimejaa Urasimu na viashiria vya rushwa

ngebe

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2020
Posts
1,789
Reaction score
5,117
Ajira za Serikali ya awamu ya sita chini ya TAMISEMi zimejaa urasimu wa kutisha, ninapowaambia hapa kuna watu wa kada za uwalimu na Afya wanaendelea kuripoti kwenye vituo vya kazi kimya kimya bila ajira kutangazwa kwa , huu ni ufisadi na mianya ya rushwa bora niongee tu ijulikane.

Mimi nina uhakika 100% asilimia kwani kuna mwenzangu tumesoma chuo kimoja ila yeye nilimtangulia mwaka mmoja karipoti kituo cha kazi mwezi wa pili kwa kupigiwa simu hivyo hvyo, hii sio haki TAMISEMI kuna shida kubwa.

Waziri Bashungwa huu ujumbe umfikie na ausome, Watumishi wa Tamisemi sasa hivi wanafanya wanavyotaka, mimi ninachojua ajira hata kama ni mbili lazima zitangazwe watu waombe wafanye mchujo. Kwanini watu wapigiwe simu kimya kimya mbona haya mambo enzi za Magufuli hayakuwepo? hii ni mianya ya rushwa na connection.

Sijawai kuona mfumo wa ajira wa namna hii hata kwenye kampuni binafsi siku hizi haya mambo hayapo, bora TAMISEMi waache kusimamia mambo ya ajira wasimamie UTUMISHI.

Ajira zote bora zisimamiwe na Utumishi.

TAMISEMI kuna watu mule wanachafua taswira ya Serikali ya awamu ya 6.
 
Mkuu mwenyewe nilipigiwa sim tuu bila rushwa wala connection wakasema wametoa jina kwenye database yao, nikajua ni matapeli wananambia nikaripot kwenye kituo Cha kazi kumbe ni kweli. Kwahyo mda mwngne usilalamike siku yako nayo itafika
 
Mtoa maada hajui maana ya kanzidata
 
Mkuu mwenyewe nilipigiwa sim tuu bila rushwa wala connection wakasema wametoa jina kwenye database yao, nikajua ni matapeli wananambia nikaripot kwenye kituo Cha kazi kumbe ni kweli. Kwahyo mda mwngne usilalamike siku yako nayo itafika
ndo ajira hutokaga kwa staili hyo?
 
ndo ajira hutokaga kwa staili hyo?
Nadhan zile zilizotangazwa za elimu na afya Kuna ambao hawakureport kwa sababu mbalimbali, Sasa apo watatangaza tena wakati kuna watu kibao waliomba na majina yapo kwenye database yao?
 
Ajira za Serikali ya awamu ya sita chini ya TAMISEMi zimejaa urasimu wa kutisha, ninapowaambia hapa kuna watu wa kada za uwalimu na Afya wanaendelea kuripoti kwenye vituo vya kazi kimya kimya bila ajira kutangazwa kwa , huu ni ufisadi na mianya ya rushwa bora niongee tu ijulikane.

Mimi nina uhakika 100% asilimia kwani kuna mwenzangu tumesoma chuo kimoja ila yeye nilimtangulia mwaka mmoja karipoti kituo cha kazi mwezi wa pili kwa kupigiwa simu hivyo hvyo, hii sio haki TAMISEMI kuna shida kubwa.

Waziri Bashungwa huu ujumbe umfikie na ausome, Watumishi wa Tamisemi sasa hivi wanafanya wanavyotaka, mimi ninachojua ajira hata kama ni mbili lazima zitangazwe watu waombe wafanye mchujo. Kwanini watu wapigiwe simu kimya kimya mbona haya mambo enzi za Magufuli hayakuwepo? hii ni mianya ya rushwa na connection.

Sijawai kuona mfumo wa ajira wa namna hii hata kwenye kampuni binafsi siku hizi haya mambo hayapo, bora TAMISEMi waache kusimamia mambo ya ajira wasimamie UTUMISHI.

Ajira zote bora zisimamiwe na Utumishi.

TAMISEMI kuna watu mule wanachafua taswira ya Serikali ya awamu ya 6.
Mkuu pole, je ungepata mkuu kweli ungelalamika?
 
Mkuu mwenyewe nilipigiwa sim tuu bila rushwa wala connection wakasema wametoa jina kwenye database yao, nikajua ni matapeli wananambia nikaripot kwenye kituo Cha kazi kumbe ni kweli. Kwahyo mda mwngne usilalamike siku yako nayo itafika
Ni kwa sababu hajapigiwa yeye wala asingesema chochote
 
Mkuu mwenyewe nilipigiwa sim tuu bila rushwa wala connection wakasema wametoa jina kwenye database yao, nikajua ni matapeli wananambia nikaripot kwenye kituo Cha kazi kumbe ni kweli. Kwahyo mda mwngne usilalamike siku yako nayo itafika
wewe itakua uko Tamisemi, nyie ndio mnapigia watu simu za mchongo, unapiwa simu ndio utaratibu wa ajira huu?
 
Wala hakuna boss, alaf uko utumishi unaposema ndo kabisaa ukienda kufanya interview ukapass alaf nafasi ikawa imejazwa wakuweka reserve kwenye database then ikitokea tuu nafasi wala hawaangaiki unapigiwa sim tuu, ndo hao unaowaona inakuta washafanyaga usaili mda.
 
Mkuu mwenyewe nilipigiwa sim tuu bila rushwa wala connection wakasema wametoa jina kwenye database yao, nikajua ni matapeli wananambia nikaripot kwenye kituo Cha kazi kumbe ni kweli. Kwahyo mda mwngne usilalamike siku yako nayo itafika

Isije ikawa wewe ni mnufaika wa huo mchongo, umekuja kusafisha Hali ya hewa hapa.
 
Unatakiwa useme kile unachotakiwa kusema badala ya makona kona kibao. Wizara ya Tamisemi ni katone tu kuzungukwa na rushwa, serikali hii yote kwa ujumla hakuna hata pa kukimbilia. Kipindi cha Uhuru serikali ya hivi ingeshapinduliwa ila basi tu kwa leo ndo hivyo tena
 
Ukiona mtu kapigiwa simu nikwamba tarifa zake zipo mule na alisha fanyiwa usahili kwahiyo nafasi zikipatikana wanapigiwa wale ambao walisha fanyiwa usahili .... kwahiyo ndugu hapo hakuna cha connection wala kujuana ... wenyewe wanaita kazidata
 
Back
Top Bottom