Maalim Raphael
Member
- Nov 23, 2018
- 94
- 202
Salaam wanajamvi!
Katika Mambo ambayo watu wa Kusini (Lindi na Mtwara) husemwa na kudhihakiwa ni utamshi wetu wa kipekee wa baadhi ya maneno yanayohusisha ncha ya ulimi kama vile; mwananke, ntoto, nti, nshale nk.
Wanaotucheka hudhani tunakosea utamshi sahihi wa lugha adhimu ya Kiswahili kumbe laa.
Katika bandiko hili, nawajuza kuwa si makosa kutamka hivyo bali utamshi huu ndio ujumi hasa. Ujumi ni hali ya kutumia maneno ya lugha fulani kwa ufundi na ustadi wa hali ya juu kwa lengo la kuburudisha na kuwavutia watu wengine. Utamshi wa namna hii, upo pia kisiwani Pemba na baadhi ya maeneo ya pwani ya Kusini ya Kenya.
Utamshi huo wa watu wa Kusini ndio mwepesi na pengine sahihi zaidi kilugha. Kwanini?
Kabla sijasema kwanini? Yafaa nidokeze kuwa; lugha ni matamshi au sauti kabla ya kuwa maandishi. Hata katika fasili za kutegemewa za lugha, sauti imepewa uzito kuliko alama za maandishi (otografia).
Kwa hiyo muhimu katika lugha ni utamshi kuliko uandishi. Na bora ya utamshi ni ule mwepesi usiochosha ala za sauti.
Baada ya kuwajuza hilo, sasa najimwaga uwanjani kujibu kwanini ni rahisi na pengine sahihi zaidi kutamka Ntu, mwananke na ntoto badala ya mtu , mwanamke na mtoto?
Kwanza, kifonolojia ni rahisi zaidi kutamka hivyo. Mfano, tulitazame neno ntu. Neno hili linaundwa na sauti tatu; /n/, /t/ na /u/.
Herufi mbili za mwanzo ni konsonanti zinazokaribiana kisifa kama ifuatavyo:
/n/ ni sauti inayopitia puani inayozalishwa kwa kukutanisha ncha ya ulimi na ufizi. Kwa hiyo /n/ ni sauti ya ufizi.
/t/ ni konsonanti inayopitia mdomoni, inayozalishwa kwa kukutanisha ncha ya ulimi na ufizi. Kwa hiyo kama ilivyo /n/, /t/ ni sauti ya ufizi. Ukifahamu hilo, utagundua kuwa kutamka ntu ni rahisi zaidi ya kutamka mtu kwakuwa sauti /n/ na /t/ zote mbili zinatoka kwenye ufizi kinyume na utamshi wa mtu ambapo /m/ ni sauti ya inayopatikana kwa kukutanisha mdomo wa juu na wa chini na /t/ ni sauti ya ufizi. Ni rahisi kutamka sauti mbili za /n/ na /t/ kwakuwa zipo jirani kuliko /m/ ambayo ni sauti ya midomo na /t/ ambayo ni sauti ya ufizi kwakuwa zipo mbali.
Mfano mwingine ni neno nke linaloundwa na sauti /n/ /k/ /e/.
/n/ tumeshaibainisha na /k/ ni sauti ya kaakaa laini ambayo hutamkwa kwa kukutanisha sehemu ya nyuma ya ulimi na kaakaa laini. Hivyo kutoka /n/ hadi /k/ unavuka kituo kimoja yaani ufizi—> kakaa gumu—>kakaa laini.
Ukitamka mke kutoka sauti /m/ hadi /k/ unavuka hatua mbili yaani, midomo—>ufizi —>kaakaa gumu—> kakaa laini.
Kwa hiyo kuna urahisi mkubwa kutamka nke kuliko mke.
Lugha ipo kwa kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano, sasa inapotokea namna nyepesi ya kutamka isichukuliwe ni uharibifu wa lugha. Kwakuwa huu pia ndio utamshi wa watu wa Pemba, nani atajipiga kifua kwamba yeye ni mlumbi wa Kiswahili kuliko Wapemba?
Naomba kuwasilisha.