Komenti za ajabu sana hizi.
Kwani ni lazima kuchagua upande?
Matokeo ya haya yanayofanywa na serikali ya awamu hii bila shaka tutayajutia hapo baadae tukishayaona matokeo yake ambayo hayapo sasa hivi, na watu wala hawajishughulishi kuzitambua athari zitakazotukabili, na hata bila kujishughulisha hata kuzichambua tu tuzijue.
Sisi tumekomalia kuwa ni matajiri, na wengine wote wanatafuta tu kuja kutuibia utajiri wetu. Na bado watu na akili zao wanaamini mambo kama haya.
Nchi haikatazwi kulinda mali zake, lakini nyakati hizi sio za kujitenga na dunia.
Hapo namwona Rwanda, Uganda, Kenya..., wote washirika wetu kwenye jumuia yetu ya Afrika Mashariki. Sisi tutakuwa soko la hawa wenzetu bila ya ubishi.
Hata tukiamua kuwa na TanzaExit yetu hatutafua dafu, tutakwenda wapi! SADC nako hapatatosha na huko AfCFTA tutauziwa tu na hawa wenzetu wanaojenga misingi ya uwekezaji imara katika wakati 'critical' kama huu.
BTW: Hivi 2019 tumepata FDI kiasi gani? Hata kutaja tu siku hizi inakuwa ni aibu?