Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Watu tumekaririshwa tu ukabila mbaya ukabila mbaya. Ukabila hauna ubaya wowote. Wanaopiga kelele kuwa ukabila mbaya ni wanataka watu wengi waje pamoja ili wawaibie na kuwatawala kirahisi.
Kunaanza Familia, Ukoo, kabila, taifa. Hakuna ubaya mtu kuwa mzalendo kwa familia, ukoo, au taifa lake. Lakini unapokuja uzalendo kwa kabila lake wanaita Ukabila! Ushahidi umeonyesha na unaendelea kuonyesha kuwa ukabila si rahisi kuisha kama ambavyo uzalendo wa watu kwa familia au koo zao si rahisi kuisha. Umeona viongozi wapatapo nafasi jinsi wanavyoyapendelea makabila yao?
Ule ni upendo kama mtu anavyopenda ukoo au familia yake. Yuko tayari kupora nchi na kutaabisha makabila mengine ili kabila lake lifaidike. Watu huwa wanajitoa sana kusaidia "Watu wao." Kila kabila lingekuwa na nchi yake kuna uwezekano mkubwa wa viongozi wao kuwa Wazalendo. Nchi nyingi zilizoendelea na kutulia watu wa nchi nzima ni kama kabila moja.
Nchi zenye watu wa makabila tofautitofauti zina taabika sana na ngumu kuendelea.