mswahili,
nikuomba uwe mwangalifu na kauli na madai yako. siyo HAKI kuchanganya wachaga wote ktk hilo "kundi" la mama mkapa. wako waliopata kukuelimisha kwamba wachagga katika undani wao ni watu tofauti sana. hata katika lugha[warombo,wamachame,marangu,kibosho] hawaelewani 100%, wengine hawaoleani kabisa.
hisia unayoileta hapa ni kana kwamba kila mchaga ni tajiri mwenye uwezo, na amejaa dhuluma. tanzania ni nchi masikini, na umasikini huo haujachagua wala kubagua kabila pale tanzania.
naamini wewe umeishi dar na umeshuhudia jinsi vijana masikini wa kichaga wanavyohangaika kuchoma nyama, na kupiga viatu rangi. baadaye wanakusanya mitaji na kuanzisha viosk etc etc.
hali ya kuja mjini kutafuta maisha haipo kwa wachagaa tu. wapemba,wakinga,wahaya,wasambaa,wahaya,....wote hao wamekimbilia mjini kutafuta maisha kutokana na mabadiliko yaliyotokea vijijini kwao.
Ninachojaribu kueleza hapa ni kwamba wapo wachaga waadilifu wachapa kazi.